Elections 2010 Vijana na wanaume watia fora wanawake wapungua-BBC

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Wawakilishi wa BBC wakihojiwa kutoka sehemu mbalimbali wamesema vijana wengi na wanaume ndio waliojitokeza ikilinganishwa na wanawake.

Baadhi ya sababu zilizotolewa na wanawake ni kukatishwa tamaa na mategemeo waliyopewa uchaguzi uliopita, kutishwa na waume wao kuwalazimisha kupigia chama cha waume zao hasa maeneo ya Kusini Mtwara na Songea Ruvuma, Kigoma nk.
 
ikimaanisha kuwa mwanamke tanzania bado hayupo huru kwenye maamuzi yake ...............anaendeshwa na mwanamme.
 
Waliwai sema vijana wanahudhuria mikutano ya Slaa hawajajiandkisha sasa CCM kazi wanayo
 
Ni kweli kituo changu vijana tulikua wengi sana na wanawake wachache mno.
 
Hata mimi kituo nilichopigia cha Shule ya msingi uwanja wa Ndege (Vituka Lumo) asubuhi mpaka mida ya saa 4 hivi zaidi ya approx 80% walikuwa wanaume. Labda kama wanawake wataenda baadaye.
 
Hii ndo inakuonyesha jinsi gani vijana walivyoamua kuleta mabadiliko. Sisiem watakiona cha mtema kuni safari hii
 
Hii ndo inakuonyesha jinsi gani vijana walivyoamua kuleta mabadiliko. Sisiem watakiona cha mtema kuni safari hii
mimi nimepigia pale shule ya msingi mlimani saa moja asubuhi watu walikuwa nyomi sio kawzida .rafiki yangu amesafiri toka dodoma kuja kupiga kura mpaka inatia moyo. Wapo madokta na maprofu wabishi lakini nimefika saa moja kasaro tano nimewakuta ktk foleni. Mabaliko yapo njiani masaa machache yajayo
 
Baadhi ya sababu zilizotolewa na wanawake ni kukatishwa tamaa na mategemeo waliyopewa uchaguzi uliopita, kutishwa na waume wao kuwalazimisha kupigia chama cha waume zao hasa maeneo ya Kusini Mtwara na Songea Ruvuma, Kigoma nk.

Haya wameyathibitisha vipi?
 
hivi wanaposema vijana wanamaanisha nini? nijuavyo mimi kijana anaweza kuwa wanamke au mwanaume. BBC wanadhani nchi zote zinatawaliwa na ma queen?
 
Wanawake wamekerwa sana na mama salma na pia ahadi hewa za jk. ccm wataota moto bila kuni, si waliwagawia kanga kibao? zimelipa?
 
Wamekerwa na kuahidiwa kubebwa kwenye bajaj kwenda kujifungua! Maneno ya Sophia Simba. Bora hawajapiga kwani wangemjazia tu JK!
 
Back
Top Bottom