Vijana na mawazo ya fisi kutamani mkono udondoke ambayo yanachelewesha maendeleo yetu

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
kumekuwa na tabia ambayo nimeanza kuiona ambayo si njema kwa sisi vijana katika ufikiri na kujituma kwetu katika kulijenga taifa letu, tabia hiyo ni kujitoa ufikiri hasa pale kunapotokea migogoro ya kitaaluma na bila kujua wakae upande upi na matokeo yake hujikuta wakikaa upande ambao wanaamini watateuliwa wakiutetea

Masuala yanayohusu taaluma si ya kukaa na kushabikia kwa sababu huwezi jua suala hilo nani atakuwa sahihi na nani hatokuwa sahihi. hebu fikiria yule ambaye unamtetea akishindwa utakuwa katika nafasi gani ama itakusaidia nini zaidi ya kudharaulika.

masuala yanayohusu siasa na Rais ni ruksa kuwa na upande kwa sababu kwa mfano suala linalohusu siasa ni suala linalohusisha vyama vya kisiasa ambapo si rahisi kwa mtu kuficha hisia zake kwa chama anachokiamini na ndio maana siasa ndio taaluma pekee ambayo hata asiyeenda shule anaweza kushiriki kuifanya. pia suala linalohusu Rais au nchi ni lazima uwe na upande ili kuonesha uzalendo kwa nchi yako. Nami daima nipo upande wa nchi yangu, rais wangu na kwa upande wa kisiasa nipo upande wa CCM ila sina ushabiki kwenye masuala yahusiyo taaluma.

mambo haya yanayofanywa na vijana ya kuingilia migogoro ya kitaaluma kwa kuamini wanaweza kuteuliwa naweza kuyafanisha na mawazo ya fisi kungonja mkono wa binadamu udondoke na usidonde na hivyo kuendelea kubaki njaa kwa kushindwa kutafuta chakula.

vijana tufanye kazi kwa bidii ili kujenga taifa imara na lenye maendeleo na tuondokane na mawazo ya fisi ya kungonja mkono udondoke. vijana wengine wanashindwa kufikia malengo yao na ya nchi kwa kufanya kazi kwa kuamini watateuliwa hasa pale wanaposhabikia migogoro hata ile ya kitaaluma

uteuzi wako kama kijana ufanyike 'by default not by effort' hivyo utapata muda wa kujenga nchi yako kwa kufanya kazi kwa bidii na kutimiza ndoto zako na za taifa lako.
 
Back
Top Bottom