Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Nafikiria kundi kubwa la watu ambao wako mtaani hawana ajira hasa wale vijana wetu waliotoka vyuoni ,kwa takribani miaka 3 sasa. Wamepiga kelele, wamelia ,wamesononeka, wameandika kwenye mitandao ya kijamii mpaka imefikia mahali sasa wameamua kunyamaza wao wenyewe. Kimya kama hawapo mtaani.
Nimeshuhudia vijana wengi sana ambao ni degree holder, wameanza kulima kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia pump za petrol au diesel, wanafundisha shule private, wanachoma chips, kufyatua matofali nk. Kuna wale wengine ambao wako kwa wazazi, mjomba/shangazi, wifi au shemeji. Huku vyeti vyao vikiwa kwenye bahasha za kaki.
Ukitembelea mabonde mengi ya umwagiliaji, unakutana na degree za Engineering, Sociology, Accounts, nk..vijana wameungana ilimradi mkono uingie kinywani.
Kuna vijana hawaamini kama watakuja kuzitumikia taaluma zao.
Mtaani vijana wanapata shida sana. Kuna kijana nilikutana Mae ameniomba hela ya sabuni na vocha, TZS 2,500. Nikampatia elfu 50. Kijana kapauka sana. Nimemwahidi kufanya nae kazi za projects zangu akiwa anakaa kwangu ili aanze kujijenga na kupata mizizi yake.
Swali ambalo najiuliza, hivi ni kweli wasomi wote chini tumeshindwa kuwabeba vijana wetu mtaani ambao wengi wana vyeti vyao vizuri? Mpaka ajira za serikali jamani?