Vijana Msijidanganye: Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa

Mkuu kipimo cha mafanikio ya waajiriwa ni kujenga tu..?
Hapana,
Nimezungumzia kujenga mana ulisema hamna wenye ajira waliojenga.,
Point was tuache dharau mafanikio yako popote kila mtu na rizq yake na juhudi zake
 
Uhalisia unaonesha, hakuna kilichokaririwa. Biashara zina mapato ajira zimejaa makato. Assume tu within five years of Magufuli hakuna mshahara umeongezwa.
Unajua unafurahisha sana

Na biashara ngapi zilifungwa kutokana na kudaiwa malimbikizo ya kodi?.
Kipindi cha corona je?.
Hamna kitu ambacho ni 'risk free'
 
Unajua unafurahisha sana

Na biashara ngapi zilifungwa kutokana na kudaiwa malimbikizo ya kodi?.
Kipindi cha corona je?.
Hamna kitu ambacho ni 'risk free'
Hizo no situational factors hata ajira nyingi zimepotea, hili janga la korona walioathirika zaidi ni employees hasa wale wakutegemea mshahara. Nazani wengi wamejifunza kuwa mshahara always hautoshi.
 
Kuhusu kodi hiyo sera mbovu za serikali, kodi zinakuwa nyingi kuliko mtaji wenyewe wa biashara. Lakini haiondoi ukweli kuwa nidhamu katika biashara kama alivyosema mkuu Infranity Solders, mapato yake ni makubwa kuliko nidhamu katika kazi.
Kama ukiweza kuhamisha shilingi 1000 kutoka kwa jirani yako kila siku, utakuwa na nafasi kubwa sana ya kutoboa. Maana pesa unazohitaji zipo kwenye mfuko wa jirani yako. Ukiwa kwenye ajira utategemea mfuko wa boss ili uishi.
Unajua unafurahisha sana

Na biashara ngapi zilifungwa kutokana na kudaiwa malimbikizo ya kodi?.
Kipindi cha corona je?.
Hamna kitu ambacho ni 'risk free'
 
Sometimes boss ndiye anakuwa mtu wa mwisho kutoka ofisini wakati huo wafanyakazi wengine woooote wamekwishafika makwao.
Hii CUlture ipo Japani; Mzee wangu alipata kuwa Mkuu wa Idara ya Innovation Kwenye Kampuni moja ya Majenereta huko; Sasa kwasababu sisi Tulikuwa huku Tz, yeye akawa anavuta kwenda home maana ataboeka; Wafanyakazi wakawa hawatoki;

Mpaka kuna siku ndo alikuja Kufahamu kwamba Japani kama Bosi wako hajatoka wewe huruhusiwi kutoka; na ndivyo huwa wanafanya hivyo; ikabidi sasa awe anatoka mapema, ili watu nao waende zao.

Umenikumbusha hiyo; Japo inaweza kuwa out of Mada
 
Daah hongera sana mkuu, kuajiriwa mi nakulia timing tu, huku sio mmh

Bora kujiajiri hata ukijitesa ni ya kwako na utapata uchungu zaidi ili upanue biashara yako na kufanya vitu vingine vya kupata pesa
Kuajiriwa boss wako anakupimia mshahara wako
Japo kila kitu kina faida na hasara
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana msijidanganye;

Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa.

Nimeamua kutoa ushauri huu kwa maana kwamba, juzi nilikuwa nimepanda daladala ya kutoka Mnazi Mmoja huku Dar nikawa ninaelekea Kigogo kwenda kumsalimia rafiki yangu mmoja hivi, classmate wa Secondary School, aliyefiwa na baba yake weeks chache zilizopita.

Sasa mimi nilikuwa nimekaa siti ile ya nyuma kabisa maeneo ya dirishani kwa maana ndio pande zangu hizo ninazopendaga mimi, then kiti kinachofuata mbele yangu walikuwa wamekaa wasichana/wadada wawili ambao wanaonekana ni University graduates wa miaka ya hivi karibuni (mimi ni University Graduate wa miaka 11 iliyopita) alafu walikuwa wametoka kazini ila kuna changamoto moja ilikuwa imewakera wakawa wanapiga story kwa sauti kidogo bila kujua kama mimi ninawasikia.

Wale akina dada wakawa wanaambizana kuwa ni bora wajiajiri tu kwa maana kuajiriwa ni utumwa. Ukijiajiri unakuwa na nafasi kubwa sana ya kujitawala na unakuwa free sana kujipangia mambo yako uingie kazini saa ngapi na utoke muda gani tofauti na kuajiriwa katika ofisi za watu wengine ambao wanakupangia kila kitu cha kufanya.

Mimi ninaomba kuchukua wasaa huu kutuma salamu zangu za pole sana kwa vijana wenye akili kama za hawa akina dada wanaofikiri kwamba kujiajiri sio utumwa.

Ndugu zangu kujiajiri ni utumwa na kama unataka kuacha kazi ya kuajiriwa na kutaka kujiajiri kwa kudhani kwamba ukifungua biashara yako hautakiwi kuwa na nidhamu ya kazi, basi ni bora hiyo pesa uende uka-bet kwa mhindi labda zali linaweza kuwa lako ukafanikiwa lakini usifungue biashara yako.

Nidhamu ya kazi kwa aliyeajiriwa ni ile ile kwa hata wewe unayetaka kujiajiri. Usifikiri eti kwa kuwa wewe ndio boss basi ukitaka kuingia kazini hata saa 5 asubuhi basi sawa tu kwa kuwa biashara yako. Hapana ndugu yangu. Unapojiajiri wewe ndiye unayepaswa kuonesha nidhamu ya hali ya juu sana kazini ili uwe mfano wa kuigwa kwa wafanya kazi wako.

Wewe kama top boss ndiye unayepaswa kuwa panctual, yaaani kama reporting time ni saa 2 asubuhi, basi wewe ikifika tu saa 1:30, upo kazini. Kama hairuhusiwi kutupa takataka hata karatasi sakafuni boss ndiye anayepaswa kuwa wa kwanza kuonesha hilo na sio vinginevyo

Kijana kama unataka kuacha kuajiriwa na kuanza biashara yako kwa kufikiri eti ukiwa na chako ndio unapaswa kukosa nidhamu ya kazi, you are wrong na tafuta mambo mengine ya kufanya. Nakushauri nenda hata uka-bet. Yangu mimi ni hayo tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
umbea wa watu kwenye usafiri wa umma unaleta huku..jitathmini
 
Naona huu mjadala watu wanaufanya kishabiki, imekuwa ligi Kati ya walioajiriwa vs waliojiajiri
Mtoa mada alikuwa na lengo zuri tu Wala sio kuwakatisha tamaa watu kujiajiri, Ni kuwa kujiajiri hasa pale mwanzo sio kitu rahisi Kama unataka kukua kimaisha kweli

Faida kubwa ya kujiajiri kunakupa nafasi ya kujikuza we mwenyewe kadri uwezavyo badala ya kumtegemea bosi afurahishwe na wewe akupandishe cheo na kujipangia ratiba zako mwenyewe

Lakini hili linakuja na price yake pia, hasa pale mwanzo unatakiwa uwe na nidhamu kubwa ili kukuza huo mradi wako na kujijengea reputation nzuri kwa wateja wako (brand)

Kuajiriwa pia sio vibaya unaweza kupata kazi nzuri inayolipa vizuri na ukawa unakua kikazi na kipato pia, lakini hata hili linahitaji nidhamu pia
Lakini kwa sababu kuajiriwa kunakuwa na misingi tayari iliyowekwa na mwenye hiyo taasisi, aliyeajiriwa hana kazi kubwa sana, yeye ni kuendeleza tu pale palipofikiwa na hiyo taasisi iliyomuajiri
Tofauti na anayeanza from scratch kujiajiri mwenyewe

Wewe mabosi wengi hawapendi kulipa mishahara mizuri ili ubaki level ile ile na likizo hawakupi
Bora ujitese mwenyewe hata huumii moyo vile kuliko unamtajirisha mtu
 
Wewe mabosi wengi hawapendi kulipa mishahara mizuri ili ubaki level ile ile na likizo hawakupi
Bora ujitese mwenyewe hata huumii moyo vile kuliko unamtajirisha mtu
Ni kweli kabisa. Ajira hata uwe na nidhamu ya fedha kubwa kiasi gani kama unaishi kwa mshahara unateseka tu. Bora uteseke lakini kwa siku una uhakika na faida kadhaa kutokana na hustle zako.
 
kutoboa unamaanisha nini? Maana nawajua watu wengi tu, wameajiriwa hawana miaka hata 10 kazini, wamejenga na wana usafiri, hii haimaanishi kuwa hakuna ambao wanasota, Lakini pia nawajua wengine waliaojiajiri ambao wanasota zaidi pia,
Mambo hayapo black and white kama manvyotaka kuifanya kama ligi ya Simba na Yanga
Kuajiriwa inategemea umeajiriwa wapi na huko kujiajiri inategemea umejiajiri kwenye nini na mtaji wako ni kiasi gani
Umemaliza kila kitu na thread ifungwe
 
Wewe mabosi wengi hawapendi kulipa mishahara mizuri ili ubaki level ile ile na likizo hawakupi
Bora ujitese mwenyewe hata huumii moyo vile kuliko unamtajirisha mtu
kujiajiri sio kitu rahisi na guarantee ya kufanikiwa mkuu, wapo wanaojiajiri na wanaangukia pua

Ndio maana ikiitwa job interview maelfu ya watu hujitokeza

Ndio maana mtoa mada kasema kujiajiri kunahitaji dedication zaidi hasa kwa anayeanza kuliko kuajiriwa
 
kujiajiri sio kitu rahisi na guarantee ya kufanikiwa mkuu, wapo wanaojiajiri na wanaangukia pua

Ndio maana ikiitwa job interview maelfu ya watu hujitokeza

Ndio maana mtoa mada kasema kujiajiri kunahitaji dedication zaidi hasa kwa anayeanza kuliko kuajiriwa

najua unasema kweli Lakin bora kujaribu kotekote
 
Bora kujiajiri hata ukijitesa ni ya kwako na utapata uchungu zaidi ili upanue biashara yako na kufanya vitu vingine vya kupata pesa
Kuajiriwa boss wako anakupimia mshahara wako
Japo kila kitu kina faida na hasara
True

Mi kwenye kujiajiri hata sioni hasara asee

Naona mafaida lukuki
 
Back
Top Bottom