Vijana Msijidanganye: Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa

Kwahio rafiki yako katoboa kwasababu anapata 100,000/- kwa siku?
Laki 1 si kubwa lakini pia sio ndogo
Inategemea

Ss mkuu mnataka kutuaminisha laki 1 kwa siku/milioni 3 kwa mwezi is nothing?na kwamba waliojiajiri wote wana uhakika na kupata hio laki kwa siku?.
 
Hujui raha ya kuwa boss hata kama unakua na nidhamu ya kutosha


Kujiajiri ndio njia bora ya kukuza ubongo na akili za kufika mbali.
Hii mada inahusu nidhamu katika kujiajiri siku za mwanzoni na sio debate kati ya kuajiriwa Vs kujiajiri. Full stop...
 
Hii mada inahusu nidhamu katika kujiajiri siku za mwanzoni na sio debate kati ya kuajiriwa Vs kujiajiri. Full stop...
Kila kitu kinahitaji nidhamu kikubwa ni kuamua na kuwa na nia. Hayo mengine ni ziada.

Kazi za kuajiriwa zinachosha asikuambie mtu. Energy unayotumia kwenye taasisi au biashara ua mtu ukiitumia kwenye mambo yako unafika mbali
 
NINARUDIA TENA KWA MARA NYINGINE, hii mada inahusu nidhamu katika kujiajiri siku za mwanzoni na sio debate kati ya kuajiriwa Vs kujiajiri. Full stop.
Kwenda huko usitupangie kama unaweza chukua mada yako nenda nayo chumbani kwako.
 
Laki 1 si kubwa lakini pia sio ndogo
Inategemea

Ss mkuu mnataka kutuaminisha laki 1 kwa siku/milioni 3 kwa mwezi is nothing?na kwamba waliojiajiri wote wana uhakika na kupata hio laki kwa siku?.
Mbona mnaruka kwenye conclusion. Napenda nijue kutoboa kipimo chake ni kipi? Ndio hio kupata kuanzia 100,000/- kwa siku? Mimi hata 10,000 kwa siku sipati nataka nijue tu ipi nipambane nitoboe.
 
Ni kweli hawako sawa and its okay.,

Kufeli na kufaulu ni matokeo tu..
My point was kwenye kujiajiri nako lazima uchague sio kila 'kujiajiri' utafanikiwa
Sio suala la kuchagua aina fulani ya kujiajiri ndio kufanikiwa. Mnaweza wote kufanya kitu cha aina moja mwenzio akafanikiwa wewe biashara ikafa.
 
Mbona mnaruka kwenye conclusion. Napenda nijue kutoboa kipimo chake ni kipi? Ndio hio kupata kuanzia 100,000/- kwa siku? Mimi hata 10,000 kwa siku sipati nataka nijue tu ipi nipambane nitoboe.
Hakuna kipimo cha kutoboa mana kila mtu ana ambition zake..,
(Japo zipo general za kibongobongo mfano kuwa na nyumba na gari)
Ndo mana hapo juu i even said mtu akijenga bungalow la mil100 ni sawa.,na mwingine akijenga ya mil 50 ni sawa pia huwezi jua ambition na mipango ya kila mtu...na salio alilonalo
Anaejenga ya mil 100 ukute ana mil150 benki ama kwenye asset zingine
Likewise anawekeza na kujenga...mana na kuna suala la 'taste' for things in life pia
 
Sio suala la kuchagua aina fulani ya kujiajiri ndio kufanikiwa. Mnaweza wote kufanya kitu cha aina moja mwenzio akafanikiwa wewe biashara ikafa.
Veryy very true
Na ndo mana ww mfanyabiashara unaweza kushindwa kutoboa ajirani ila wenzio wakapeta na wakawa na maisha mazuri kukuzidi pia.,
It can happen pande zote
 
Hakuna kipimo cha kutoboa mana kila mtu ana ambition zake..,
(Japo zipo general za kibongobongo mfano kuwa na nyumba na gari)
Ndo mana hapo juu i even said mtu akijenga bungalow la mil100 ni sawa.,na mwingine akijenga ya mil 50 ni sawa pia huwezi jua ambition na mipango ya kila mtu...na salio alilonalo
Anaejenga ya mil 100 ukute ana mil150 benki ama kwenye asset zingine
Likewise anawekeza na kujenga...mana na kuna suala la 'taste' for things in life pia
Hamna kipimo cha kutoboa? Okay..
 
Kwamba unahitaji research kujua kuwa Bongo mishahara ni midogo?! Dude please!
Inahitajika umachale na umakini mkuu ..ajira popote duniani haiwezi kukutoa labda ufanye savings ya hali ya juu. Tatizo hawaelewi hawa waajiriwa wetu hawaelewi japo ndo wateja wetu.
 
Na kweli kila mtu wa upande wowote anaweza akafanikiwa
Kujiajiri ni kuzuri ila sio kila kitu na sio fani ya kila mtu.,

Wapo watu kwenye ajira wanatengeneza hela zaidi ya watu wengi tu waliojiajiri maisha yao yote
Hao watu ni wachache kuliko walio wengi wanaopambana na mishahara duni. Huu ndo ukweli, kama umeajiriwa hakikisha unafanya juu chini uwe na biashara kabla Jua halijazama ..ajira ina mwisho wake biashara unastaafu ila kama una misingi mizuri itaendelea tu, ajira ukistaafu ndo basi tena.
 
Rafiki yangu ameajiriwa analipwa 100,000/= kwa siku. Hii mada inahusu nidhamu katika kujiajiri siku za mwanzoni na sio debate kati ya kuajiriwa Vs kujiajiri.
Mkuu hatubishani kabisa ..kuhusu ajira ni sawa kabisa, nikiangalia rafiki yako analipwa 100,000 kwa siku ambayo ni fixed, haipandi wala haishuki huyu huwezi kusema ana mafanikio kwa sababu siku ajira ikipotea na kama hakuwa na hiyo nidhamu ndo basi tena. Tukija kwa biashara kama ukipata icho kiasi haiwezi kuwa fixed, leo inapanda kesho inashuka ..kesho hupati kabisa lakini kama una nidhamu au hauna kabisa unapata fundisho makini. Mkuu kiukweli unaweza kuwa na kazi hata ya kulipwa milion kwa siku lakini usipokuqa na nidhamu iyo kazi ikapotea basi ujue hutopata iyo million tena. Ila kama una biashara na unapata million kwa siku na hukuwa na nidhamu biashara ikafa ..basi una chance nzuri ya kuweza kurudi na kuwa na nidhamu zaid. Na hii ndo faida mojawapo wa biashara. Hata kwangu mimi ni shahidi kabisa.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana msijidanganye;

Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa.

Nimeamua kutoa ushauri huu kwa maana kwamba, juzi nilikuwa nimepanda daladala ya kutoka Mnazi Mmoja huku Dar nikawa ninaelekea Kigogo kwenda kumsalimia rafiki yangu mmoja hivi, classmate wa Secondary School, aliyefiwa na baba yake weeks chache zilizopita.

Sasa mimi nilikuwa nimekaa siti ile ya nyuma kabisa maeneo ya dirishani kwa maana ndio pande zangu hizo ninazopendaga mimi, then kiti kinachofuata mbele yangu walikuwa wamekaa wasichana/wadada wawili ambao wanaonekana ni University graduates wa miaka ya hivi karibuni (mimi ni University Graduate wa miaka 11 iliyopita) alafu walikuwa wametoka kazini ila kuna changamoto moja ilikuwa imewakera wakawa wanapiga story kwa sauti kidogo bila kujua kama mimi ninawasikia.

Wale akina dada wakawa wanaambizana kuwa ni bora wajiajiri tu kwa maana kuajiriwa ni utumwa. Ukijiajiri unakuwa na nafasi kubwa sana ya kujitawala na unakuwa free sana kujipangia mambo yako uingie kazini saa ngapi na utoke muda gani tofauti na kuajiriwa katika ofisi za watu wengine ambao wanakupangia kila kitu cha kufanya.

Mimi ninaomba kuchukua wasaa huu kutuma salamu zangu za pole sana kwa vijana wenye akili kama za hawa akina dada wanaofikiri kwamba kujiajiri sio utumwa.

Ndugu zangu kujiajiri ni utumwa na kama unataka kuacha kazi ya kuajiriwa na kutaka kujiajiri kwa kudhani kwamba ukifungua biashara yako hautakiwi kuwa na nidhamu ya kazi, basi ni bora hiyo pesa uende uka-bet kwa mhindi labda zali linaweza kuwa lako ukafanikiwa lakini usifungue biashara yako.

Nidhamu ya kazi kwa aliyeajiriwa ni ile ile kwa hata wewe unayetaka kujiajiri. Usifikiri eti kwa kuwa wewe ndio boss basi ukitaka kuingia kazini hata saa 5 asubuhi basi sawa tu kwa kuwa biashara yako. Hapana ndugu yangu. Unapojiajiri wewe ndiye unayepaswa kuonesha nidhamu ya hali ya juu sana kazini ili uwe mfano wa kuigwa kwa wafanya kazi wako.

Wewe kama top boss ndiye unayepaswa kuwa panctual, yaaani kama reporting time ni saa 2 asubuhi, basi wewe ikifika tu saa 1:30, upo kazini. Kama hairuhusiwi kutupa takataka hata karatasi sakafuni boss ndiye anayepaswa kuwa wa kwanza kuonesha hilo na sio vinginevyo

Kijana kama unataka kuacha kuajiriwa na kuanza biashara yako kwa kufikiri eti ukiwa na chako ndio unapaswa kukosa nidhamu ya kazi, you are wrong na tafuta mambo mengine ya kufanya. Nakushauri nenda hata uka-bet. Yangu mimi ni hayo tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Umesahau kuweka tangazo la kuuza vitabu hapo mwisho mkuu
 
Back
Top Bottom