Vijana Msijidanganye: Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana msijidanganye;

Ukiamua kujiajiri ni lazima uwe na nidhamu ya kazi (Self-Discipline) mara kumi (10) zaidi ya ulivyoajiriwa ndio utafanikiwa.

Nimeamua kutoa ushauri huu kwa maana kwamba, juzi nilikuwa nimepanda daladala ya kutoka Mnazi Mmoja huku Dar nikawa ninaelekea Kigogo kwenda kumsalimia rafiki yangu mmoja hivi, classmate wa Secondary School, aliyefiwa na baba yake weeks chache zilizopita.

Sasa mimi nilikuwa nimekaa siti ile ya nyuma kabisa maeneo ya dirishani kwa maana ndio pande zangu hizo ninazopendaga mimi, then kiti kinachofuata mbele yangu walikuwa wamekaa wasichana/wadada wawili ambao wanaonekana ni University graduates wa miaka ya hivi karibuni (mimi ni University Graduate wa miaka 11 iliyopita) alafu walikuwa wametoka kazini ila kuna changamoto moja ilikuwa imewakera wakawa wanapiga story kwa sauti kidogo bila kujua kama mimi ninawasikia.

Wale akina dada wakawa wanaambizana kuwa ni bora wajiajiri tu kwa maana kuajiriwa ni utumwa. Ukijiajiri unakuwa na nafasi kubwa sana ya kujitawala na unakuwa free sana kujipangia mambo yako uingie kazini saa ngapi na utoke muda gani tofauti na kuajiriwa katika ofisi za watu wengine ambao wanakupangia kila kitu cha kufanya.

Mimi ninaomba kuchukua wasaa huu kutuma salamu zangu za pole sana kwa vijana wenye akili kama za hawa akina dada wanaofikiri kwamba kujiajiri sio utumwa.

Ndugu zangu kujiajiri ni utumwa na kama unataka kuacha kazi ya kuajiriwa na kutaka kujiajiri kwa kudhani kwamba ukifungua biashara yako hautakiwi kuwa na nidhamu ya kazi, basi ni bora hiyo pesa uende uka-bet kwa mhindi labda zali linaweza kuwa lako ukafanikiwa lakini usifungue biashara yako.

Nidhamu ya kazi kwa aliyeajiriwa ni ile ile kwa hata wewe unayetaka kujiajiri. Usifikiri eti kwa kuwa wewe ndio boss basi ukitaka kuingia kazini hata saa 5 asubuhi basi sawa tu kwa kuwa biashara yako. Hapana ndugu yangu. Unapojiajiri wewe ndiye unayepaswa kuonesha nidhamu ya hali ya juu sana kazini ili uwe mfano wa kuigwa kwa wafanya kazi wako.

Wewe kama top boss ndiye unayepaswa kuwa panctual, yaaani kama reporting time ni saa 2 asubuhi, basi wewe ikifika tu saa 1:30, upo kazini. Kama hairuhusiwi kutupa takataka hata karatasi sakafuni boss ndiye anayepaswa kuwa wa kwanza kuonesha hilo na sio vinginevyo

Kijana kama unataka kuacha kuajiriwa na kuanza biashara yako kwa kufikiri eti ukiwa na chako ndio unapaswa kukosa nidhamu ya kazi, you are wrong na tafuta mambo mengine ya kufanya. Nakushauri nenda hata uka-bet. Yangu mimi ni hayo tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Uko sawa infantry soldier.

Discipline ya kujiajiri inapaswa kuwa kubwa kuliko hata ya kuajiriwa ili mtu aweze kufikia malengo ya kujiajiri.

Kama mtu anadhani kujiajiri ni kuwa huru peke yake bila kufanya kazi kwa nidhamu bado hajajua sababu ya kujiajiri
 
Kwanza ukijajiri hautoki kazini saa 11 pita kariakoo pita buguruni pita tandika utaona watu wana fight hadi saa 6 usiku ili watoboe na hyo ni 24/7 haina weekend hyo.

Shida motivational speakers wanalisha sana watu matango pori ila mambo sio easy kama wanavoropoka huko kwny vi semina
AJira hakuna unadhani option iliyobaki ni nini.
 
Back
Top Bottom