Vijana msidanganyike DINI Muhimu katika kuamua nani mke/mume

KWA HIYO UNATAKA KUTUAMINISHA KUWA DINI INAZIDI NGUVU MAPENZI?ACHA KUJIDANGANYA WEWE,MAPENZI NI ZAIDI YA MAKOMBORA YA MRUSI....

Huyo mapanki mwenyewe analegea kwa mkewe
Hujaelewa, tunaongelea dini kwa wale wanaojua dini na kuishika dini sio wanaoisikia na kufata mkumbo. Dini ni kitu kingine kabisa ndg yangu. Mapenzi ya upofu ndiyo hayatambui dini.
 
Religion
is a way of life to teach you how to love and do good to the... world. Religion....... without love is...... misleading. Some.... religions actively..... preach love towards.......nature, some preach love towards other human beings, some preach love towards animals. But every
religion celebrates love...
 
Nimekuwa interested na huu uzi lakn ukisema dini tunazungumzia ukristo na uwislamu hizo ndio dini mbili na wanaitikadi tofauti. Je? ukija kwenye swala la mkristo kwa mfano msabatho na mkatholoki mmoja wapo akibadili na kumfuata mwenzie hapo ni makosa kwani hyo wamebadili thehebu sio dini, je? hapo tatzo liko wapi kubadili dhehebu au dini au vyote ni makosa
 
MAPENZI YANA NGUVU SANA KIASI KWAMBA MTU NI RAHISI KUOA BILA KUJALI DINI LAKNI NI VYEMA KUMWOMBA MUNGU MAANA UKIPATA MKE WA DINI YAKO AKAWA ANAMJUA MUNGU KWELI KWELI KUNA UWEZEKANO MKUBWA SANA WA KUISHI KWA RAHA KULIKO MKIWA DINI TOFAUTI.
 
Mwanzoni mnapoanza mahusiano mnakua ninyi tu wawili , tatizo mnapotaka kusonga mbele katika uhusiano , mambo mengi yako attached, familiy background, hasa dini... na mkipuuza na mkasonga mbele mjue kunashida sana ... otherwise lazima mtumie msuli sana kama pesa kama mnayo ndio mnaweza shawishi baadhi ya wanafamilia waliochokja wasio na misimamo, lakini kwenye familia conservative hata wawe malofa kama mkwe si wa dini yao shida sana... mtaishi kwa shida sana na ikitokea mkagombana hata kidogo tu basi dini itaingia kama kisingizio kikuu... na mgogoro wowote mtakao kua nao kama wapenzi utaombewa dua na wazazi au ndugu ili uendeleee na hatimae mtengengane... in short blessing zero
 
Kabla ya hizo dini hatukuwa na dini zetu za asili??
Na kabla ya nguo hizi tunazovaa tulikua baadhi yetu tunavaa nguo na baadhi walikua wanatembea uchi kabisa,je tuishi kama zamani au tuvae nguo ambazo nyingi zililetwa na watu wamagharibi?
 
Swala la dini ni mtambuka... Kama ndoa ya dini tofauti ila familia zenye msimamo wa wastani hiyo ndoa itadumu na haitapata misukosuko... Kama familia zina misimamo mikali juu ya dini zao ni matter of time lazima jipu litazaa usaa... Mwanzo wakati Genye zikiwa juu hili laweza kuwa sio tatizo ila baada ya muda mkishaachana na genye na kuishi real life na ubinafsi ubinafsi ndipo kila mmoja atagundua dini yake ni bora kuliko ya mwenzie na watoto ndio hasa wanakuwa silaha za kupigana kwa kujazwa sumu na kuambiwa ubaya wa dini hii na hii lengo likiwa ni kuwateka.... Wanawake ni mahodari sana wa kujifanya wamepotezea dini yao ila ukweli usiopingika ni muda tu atarudi tena kwa nguvu kubwa hasa akishapata utawala ktk ndoa na hapo ndipo pa kujifunzia juu ya dini za wanandoa........
 
Uko sahihi sana mkuu, jirani yangu alioa dada wa dini isio yake, huyu jamaa ambae kwa sasa ametangulia mbele ya haki, wanae wote walikua wa dini yake, na hata masomo ya dini walisoma... bahati mbaya walipokuwa wanagombana na mkewe (huyu mdogo) maana jamaa alikua na wake wawili mmoja wa dini yake na mwingine wa dini nyingine... sasa bwana mkubwa huyu kila mara apokua anakhitlafiana na mkewe mama alitumia watoto kama silaha, akawa anawapeleka anakoabudu yeye kama kumkomoa mumewe.... bahati mbaya zaidi ilitoke jamaa akafariki pakatokea mzozo mkubwa sana wa kifamilia ...na mpaka sasa watoto wamehamia dini ya mama na wamesuswa na upande wa marehemu ( baba) shida tupu
 
Ndoa ni kupendana, maelewano na kuheshimiana. Hata kama mtakua dini moja kama hakuna upendo, maelewano na kuheshimiana still utaona Ndoa chungu
 
Kwa mujibu wa uislam

Hakuna ndoa kati ya muislam na asiyekuwa muislam(huo ni uzinzi tu) so kitendo cha wazinzi wawili kuishi pamoja hakihesabiwi kama ndoa kwa mujibu wa dini.
 
Back
Top Bottom