Vijana msidanganyike DINI Muhimu katika kuamua nani mke/mume

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,826
1,730
Vijana wamekua na ka msemo kuwa ...'' there is nothing can stop me from loving you'' nani kakwambia?!! usidanganyike kijana wangu kuoa mtu asiye kuwa wa dini yako ni kupoteza muda tu.... na leo nataka mjue kabisa sisi wazazi wenu yalitukuta haya tukachemka... mpende wa dini yako ili mfike mbali kimahusiano... marriage is about connecting two families ... haya yakusema ''darling niangalie mimi tu wazazi wakazi gani''? nikujidanyanya.... na wala mtu asikwambie nabadili dini kwa ajili yako hiyo ndoa itakua haina amani kabisa... nasema yalishatukuta sisi wazazi wenu.. tatizo lenu mnadhani sisi hatujapitia huko ... mnayofanya yote waanzilishi ni sisi... hakuna upuuzi mpya manfanya it is just a repetitions BANGE HAMJAGUNDUA NINYI!!!!
 
KWA HIYO UNATAKA KUTUAMINISHA KUWA DINI INAZIDI NGUVU MAPENZI?ACHA KUJIDANGANYA WEWE,MAPENZI NI ZAIDI YA MAKOMBORA YA MRUSI....

Huyo mapanki mwenyewe analegea kwa mkewe
 
Kwahiyo kabla hamjatongozana muulizane dini?
Yeuwiiiiii Ubaguzi ulioje

dini zenyewe zimekuja na Merikebu
Em mtupishe!!!
 
Nakubali asilimia 90%
Sio tu kwenye kuishi wewe na mwenza wako,,kuna kuwaza malezi ya kizazi chako.
Assume watoto unawalea maadili ya dini yako,akienda kwa bibi anafundishwa tofauti.
Ulishawaza ukiwahi kufa ukaacha watoto wadogo,misimamo yao ya dini itakuaje?!!
Tutauliza juu ya malezi ya watoto na muongozo tuliowapa hapa duniani..,sio dini tu jaribu pia kutafuta mke au mume mwema ili kizazi chako kinusurike na majanga haya ya dunia.
 
Dini ni imani.
Usifungiwe nira na mtu asiyeamini.... maana yake usiunganishwe na mtu asiye wa imani yako. Mapenzi huzaa ndoa, ndani ya kapu la ndoa huwezi kuweka vitu viwili tofauti. Haiwezekani kichwa kinaamini jua na kiwiliwili kinaamini mvua.

Enyi kizazi cha leo badilikeniiiii....tafakarini; jifunzeni acheni kukaza shingo.
 
Vijana wamekua na ka msemo kuwa ...'' there is nothing can stop me from loving you'' nani kakwambia?!! usidanganyike kijana wangu kuoa mtu asiye kuwa wa dini yako ni kupoteza muda tu.... na leo nataka mjue kabisa sisi wazazi wenu yalitukuta haya tukachemka... mpende wa dini yako ili mfike mbali kimahusiano... marriage is about connecting two families ... haya yakusema ''darling niangalie mimi tu wazazi wakazi gani''? nikujidanyanya.... na wala mtu asikwambie nabadili dini kwa ajili yako hiyo ndoa itakua haina amani kabisa... nasema yalishatukuta sisi wazazi wenu.. tatizo lenu mnadhani sisi hatujapitia huko ... mnayofanya yote waanzilishi ni sisi... hakuna upuuzi mpya manfanya it is just a repetitions BANGE HAMJAGUNDUA NINYI!!!!
Ndoa yangu ina miaka 18 na ni dini tofauti na mwenzangu
 
Back
Top Bottom