Vijana Monduli waapa kumfuata Lowasa popote atakapokwenda

Kilasi Mkuu

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
2,325
719
Katika taarifa ya habari Channel ten vijana wamesema wanajiandikisha kwenye daftari la kudumu ili kumuunga mkono Lowassa.

Wanasema wanajua amekatwa lakini wao watashikamana na baba yao Lowassa.

Kwa ujumla wake tukiongezea na mkolezo wa Kingunge japo yeye Lowassa hajasema kitu kwa sasa hali ni tete ndani ya CCM .

Ule umati wa Lowassa ulikuwa mkubwa mno kwa nchi nzima, huwezi kuuzima kwa kumweka tu Magufuli tena kwa kukiuka taratibu.

Mimi naiona hali hiyo kama hali ileile ya muda kuwadia wa kifo cha CCM.

Kiukweli miaka yote CCM hawajawahi kutofautiana kwa kiasi hiki. Maana Kingunge anasema mtu alikuja na majina yake tu na kuyapenyeza kamati kuu.

Naona mtu mwenyewe atakuwa JK tu maana hupenda mambo ya kienyeji kama alivyo kuwa akiendesha Nchi.
 
Huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono, mkono ukabaki salama. lazima ama ufyekwe na mafuriko ubaki kilema, au uzame mzimamzima.
 
Ccm wamemuujumu Lowasa wetu tusikubali.Pombe akija kwetu azomewe na kufukuzwa hatutaki mgombea wa mfukoni.Lowasa na Kingunge pambana mpaka kinuke
 
Ccm wamemuujumu Lowasa wetu tusikubali.Pombe akija kwetu azomewe na kufukuzwa hatutaki mgombea wa mfukoni.Lowasa na Kingunge pambana mpaka kinuke
Tatizo kuna watu wanajifanya wao ndiyo wananchi,yaani wao ndiyo Watanzania zaidi kuliko wengine
 
Magufuli hatumtaki ni mgombea wa mfukoni.Hana hekima ni mropokaji alituambia tupige MBizi.Kikwete asitupangie wa kumchagua.CCM ni yetu sote
 
Tatizo kuna watu wanajifanya wao ndiyo wananchi,yaani wao ndiyo Watanzania zaidi kuliko wengine

Kwani viongozi wa juu wa magamba si ndiyo wamiliki halali wa hii nchi, sisi wengine ni wakimbizi.

Jana Kingunge alinishangaza sana baada ya kusema hii nchi ni yetu sote.
WanaCCM wachache wamejitwalia mamlaka ya kumiliki nchi yao TZ na yeye akiwa mmojawapo sasà leo anakuja kukataa, alinishangaza sana.

Kilichobaki ni wauwane TU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom