Vijana Mnatupeleka Wapi ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana Mnatupeleka Wapi ??

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Yona F. Maro, May 18, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  May 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Leo katika pita pita zangu nilinasa sehemu Fulani katika foleni eneo la ilala , tulikaa pale kwa muda mrefu kidogo karibu dakika 20 , magari hayaendi huku au kule , pembeni yetu kulikuwa na vijana wamepanda nyuma ya pick up , mbele yao wakina mama wako katika basi wanaenda katika msiba .

  Ghafla hawa vijana wakaanza kuimba Nambari wani eehh nambari wani ni CCM , si mnaona sasa , mikanga yenu mliyopewa hiyo wakati ule ? angalia sasa hii ndio barabara waliyoahidi , rudisheni mikanga yenu hii ndio CCM iliyowapa mikanga hiyo mkawachagua .

  Wale wakina mama hawakuwa na jibu lolote , lakini walikuwa wanaogopa sana manake vijana walikuwa na hasira walikaribia mpaka kushuka katika gari walilopanda wao waende kwa wale wakina mama waliovaa zile kanga .

  Hawa ni mfano wa vijana ambao kwa siku za karibuni wameonekana kulaumu chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla wakiona chochote mbele yao , nilitaka kuwauliza hivi ccm inahusika nini na mkandarasi aliyejenga barabara hiyo ? au ccm ndio walikagua barabara hiyo kabla yaijakabidhiwa ? yote hayo ni maswali ambayo nilitaka kuuliza .

  Ni sawa na wale vijana wengine waliotiwa nguvuni kwa tuhuma za kumzomea raisi mstaafu Benjamin William mkapa kwa sababu zao binafsi , au sijui hawa vijana wanalipwa au wanapewa kitu gani mpaka wanakuwa na ujasiri wa kudhalilisha wenzao kiasi hicho .

  Tabia hizi kwa kweli zinauzi na kukatisha tamaa sana , kama vijana wa leo ambao tunategemea wawe mstari wa mbele katika kujenga jamii bora zinazoangalia mbele kuanza kuzomeana njiani , kuimba nyimbo za ajabu ajabu , kuandamana katika mavyuo na mashuleni sijui kuchoma moto na kufanya vurugu nyingine .

  Kwa mtindo huu vijana wasitegemee kufika popote au kusikilizwa na mtu wowote , kama mawazo yao ni kuungwa mkono na vyama vya upinzani kama wale wananchi wa tabata dampo basi watafute mengine na kama kuzomea huku , au kuimba nyimbo za kashfa hizi zinafadhiliwa na upinzani au mtu wowote yule

  Waelewe nyimbo hizo na aina nyingine zozote za vitu wanavyofanya ni kuvunja sheria za jamhuri ya muugano wa Tanzania , na sheria ina mkono mrefu itakufuata popote ulipo na kukufikisha katika vyombo husika ili uweze kujibu tuhuma zinazokukabili

  Vijana sasa wafanye mengine kuna mengi ya kufanya zaidi ya kuzomea , kuimba nyimbo za kashfa , kuchoma moto shule , kufanya fujo mashuleni na sehemu zingine .
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,568
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Nilipokwambia kaburi la CCM linachimbwa we ukabisha na kuendeleza propaganda!
  Sasa umegundua lakini it took you a while!
  NI WAKATI WA KUWA UPANDE HURU WA WANANCHI!
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  May 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Bwana Mushi , Unavyosema Kaburi La Ccm Linachimbwa Hayo Ni Maneno Yako Wewe Kama Mwananchi Una Haki Ya Kusema Chochote Na Lolote Ili Mradi Usivunje Sheria Za Nchi Na Forum

  Mimi Pia Ni Mtu Huru Naandika Kile Ninachojisikia Na Kufurahia Na Kuweka Katika Jukwaa Hili , Katika Mailing List Zangu Na Sehemu Zingine Nyingi Tu Ambazo Hutu Husoma Mambo Kadhaa

  Kwa Maana Hiyo Basi , Usinifananishe Au Usiniunganishe Na Chama , Dini , Au Kikundi Chochote Kile Ambacho Mimi Binafsi Sijadhibitisha Kwamba Ni Mwanachama Au Nimewahi Kushiriki Chochote Walichofanya Au Kuwahi Kufanya

  Wewe Jibu Hoja Zilizo Mezani Na Mbele Yako

  Usiku Mwema
   
 4. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mkuu

  Naona sasa unaelekea kurudi kwenye kiwango chako. Lakini pia sikubaliani na wewe na sitakubaliana na wewe ktk hili. Hawa vijana kila kukicha wanasikia mazuri aliyoyafanya Mkapa akiwa Ikulu. Kwa njia moja ama nyingine yanaathiri maisha yao ya kila siku.

  Vijana hawana uwezo wa kumpeleka Mkapa mahakamani lakini pia wanauwezo wa kuzungumza. Mpaka sasa hakuna aliyetoa ushahidi kama kweli vijana walikuwa wakitaja kuwa Mkapa ni FISADI, Mkapa ni FISADI hila walisema FISADI.

  Ilikuwaje Mkapa akajua kuwa wanamsema yeye? Wakati kulikuwa na polisi, wapita njia wengine nk. Je anahisi kuwa yeye ni FISADI?. Je ni kweli alifanya Bussiness akiwa IKULU?.

  Mimi nafikiri bado ni makosa kuwahukumu vijana kwa sababu kwa kila sehemu watashinda kesi hii labda watumie udikteta ambao pia haiwezekani.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  May 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kumbe Huu Ni Uzishi Sikujua
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,307
  Trophy Points: 280
  Vijana Mnatupeleka Wapi ??

  TUNAWAPELEKA KWENYE UADILIFU, UWAJIBIKAJI, NIDHAMU NA UONGOZI BORA
   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2008
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Shy,

  Tufanye nini sasa kuhusu hili?
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  May 19, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kumbe 'CCM nambari wani ' ni wimbo wa ajabu siku hizi eeeh?

  Wewe Shy nani asiyekujua? Ukada wako wa kujipendekeza utakuumiza siku moja.
  Nimeona huo utumbo ulioandika hapo juu,nikafananisha na unavyojitangaza hapo chini eti Yona maro.............Ila nakuona mzushi na mnafiki tuu.Tafadhali usichafue taaluma za watu kama kiwango chako cha kufikiri kiko low hivi
   
 9. mwanakwetu

  mwanakwetu Member

  #9
  May 19, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Shy,
  Ploe sana na wenzio wanokelekwa na kuumizwa na mwenendo huu wa vijana siku hizi. Unauliza tunawapeleka? Hatuwapeleki bali tunaelekea kule mlikotuelekeza twende. Huwezi panda mahindi utarajie kuvuna mpunga wapi na wapi? Mkapa aliamua kujivua nguo mwenyewe alitegemea nini? watu wamwambie umependeza? Ni ukweli kwamba shida na tabu tunazozipata ni kutokana na serikali iliyopo madarakani ambayo inatokana na chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kilinadi sera na hao wakinamama pasipo kusikiliza sera wakakimbilia kanga ndio wametufikisha hapa sasa. CCM katika hili hawawezi kunawa labda kwa hekima tu ifikapo uchaguzi 2010 wanaojiona dhaifu na hawatoshi kusimamia sera za chama chao wakae pembeni wawapishe wenye uwezo. Tatizo lililopo CCM ni viongozi wenye dhamira ya kweli wengine walitaka kujaribu tu madaraka wayaone yanafananaje, wengine walitaka madaraka kujilimbikizia mali na wengine wanatafuta sifa tu. Si ajabu leo hata mtoto ukimuuliza anapenda kuwa nani atakapokuwa mkubwa atakwambia anapenda kuwa Mbunge si kwa sababu ya wito hapana ni kwa sababu wanamafao makubwa na hakuna kazi wanayofanya (Kunradhi sio wote). Narudia tena pole Shy kama hukulijua hili.
   
Loading...