Vijana mliopo A-level: Technique rahisi nilizotumia kupiga Division One ya 3 form six bila kukesha darasani

CCNP Engineer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
462
1,276
Last week nilikua napitia matokeo ya madogo wa form six kwa Special Schools (Mzumbe, Tabora Boys, Kibaha na Ilboru) lengo ni kuhesabu One za Tatu yaani ni za kutafuta kwa tochi... Nimeambulia kuona moja tu ya dogo wa Mzumbe alokua T.O (dogo mwenyewe PCB, sijui PCM siku hizi wamerogwa na nani).

Huu ni ushauri kwa madogo ambao mpo Advance na mna munkari wa kupiga One Kali tatizo hamjui strategies zipi mtumie. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma sana na kufaulu. Kusoma sana sio kufaulu, bali kusoma kwa technique.

Mbinu nilizotumia kupiga One ya 3 bila kukesha darasani:

Target Audience:
Wanafunzi waliopo Advance (five na six) hasa PCM (shule za Private hawahusiki sababu wana walimu na miundombinu ya kutosha)

Malengo:
Weka malengo ya kupiga One Kali. Yaani kila somo lisome ukiwa na mind za kupata A. Ukijiwekea malengo ya kupiga A lazima utakua unasoma kwa focus.
Mie wakati naingia form five nikaweka malengo kuwa lazima nipige one ya 3 na niingie Top 3 kitaifa. Na ikawa hivo mwisho wa siku.

Timetable:
Sikua na fixed (defined) ratiba kama wenzangu walivokua wamebandika ndani ya matranka yao au ukutani pembeni ya kitanda. Mie nilikua nasoma kwa mood.
Nilikua na alternate kati ya Physics na Chemia. Napiga maswali ya Gravitation nikichoka nafunga kesho napitia Inorganic Chemistry.

Hesabu nilikua napitia kila siku nikitaka kulala (somo la kulalia). Mfano nikitoka class kupiga maswali ya Electronics narudi Dom nafungua pure II napiga maswali yangu 20 ya Complex Number then nalala.

Kuna wakati najikuta nasoma Physics hata week nzima (mfano napoamua kupitia Mechanics), yaani kifupi sikua na ratiba fixed, nasoma kutokana na nataka nikave topic zipi kwenye somo husika.

Achana na tabia ya kusoma kwa ratiba, soma kulingana na somo lipi topic ipi upo nyuma sana. Topic ipi hujapitia maswali mengi, topic ipi umeanza kusahau. Lazima upige One ya 3.

Kabla sijasahau: Mie usiku mwisho wangu kusoma ilikua saa nne. Mchana ndio muda wangu wa kupiga kitabu, giza likiingia tu basi nakua zoba. Usually ikifika saa tatu usiku kama sijaenda prepo basi siendi tena, napitia hesabu kitandani nalala.
But mchana hunikuti nafanya upuuzi (labda jioni kwenye jogging uwanjani).
Lazima upige One ya 3.

Twende kwenye masomo husika sasa:

Physics:
Vitabu nilivosoma mpaka napiga pepa: (Chandy, Nelkon na Roger Muncaster).
Katika somo unalotakiwa upitie vitabu vingi ni Physics. Lakini mie nilikua mjanja. Nilipitia vitabu ambavyo NECTA wanapenda kutoa maswali basi. Vingine nikaachana navyo.

Nilianza na Chandy, then nilipo kimaliza nikaja Nelkon (hiki hata sikusoma, bali nilifanya maswali yote ya mle sababu hakina maelezo mengi). Then form six mwishoni nikamalizia Roger (japo kina maswali magumu, nilijitahidi kufanya, yaliyonishinda nikaachana nayo)

Ukitaka kuelewa Physics basi soma Chandy (wahindi wanaeleza mpaka una enjoy), but ukitaka kufaulu Physics NECTA piga maswali karibu yote ya Nelkon na Roger Muncaster. NECTA wanapenda kutoa maswali kutoka kwenye Nelkon na Roger.

Practical za Physics zote nilifoji wakati wa pepa. Ukijifanya kupiga practical real hutomaliza muda hautoshi. Ukikaribia NECTA jifunze namna ya kufoji practical za Mechanics, Heat na Umeme.

Lazima upige One ya 3.

Chemistry:
Katika masomo yaliokua mteremko kwangu basi ni Chemistry. Kwanza kabisa ndio somo ambalo sikuwahi kabisa kusoma Vitabu. Niliishia kusoma Notes tu pamoja na kupitia Past Papers za NECTA.
Yaani nilikua nashangaa watu wanakomaa kusoma Ramsden usiku wa manane wakati Chemia ni mwendo wa notes tu unapiga banda. Practical zake ndio chai kabisa.

Kifupi ni kuwa ukitaka kupiga banda la Chemia with minimum efforts fanya hivi:
Soma notice za topic husika (mfano Electrochemistry), ukishaelewa chukua Review ya NECTA, pitia pepa moja baada ya nyingine kwa topic (achana na tabia ya kupitia pepa zima matopic yote utaloose concentration, nenda topic by topic).
Ukimaliza rudi tena kwenye notice, soma topic nyingine (mfano Organic) then njoo tena kwenye Review, fanya hivo hivo. Hadi umalize topic zote.

Practical za Chemia zote nilifanya real, sikufoji hata moja. Sababu praki za Chemia ni simple, sinafanyika ukifata procedure. Kifupi Chemia hutakiwi kukosa A au B+. Mie nilipiga A kali nikaongoza Chemia kitaifa form six yetu. Watu wamekomaa na mavitabu nikawakimbiza kama kawa.
Lazima upige One ya 3.
upload_2018-7-25_0-22-31.png




Advanced Mathematics:
Katika somo ambalo nilikua nasomea kitandani ni hesabu. Kwanza kabisa sikua na ratiba maalum ya kusoma hesabu. By the way hesabu hatusomi, bali huwa tuna solve.
Nilianzaga kukomaa na Tranter kubabake kikanishinda. Nikaachana nacho.
Nikakomaa na Pure I na II nikakomaa nazo na sikuwahi kusoma kitabu kingine chochote zaidi ya hivi viwili.
Style yangu ile ile, nasoma topic (mfano Integration) then nazama kwenye NECTA Review napiga maswali yote ya Integration mpaka yaishe. Nikimaliza natafuta another topic hivo hivo.
Lazima upige One ya 3.

Mwisho Kabisa:
Watu wanaamini kuwa ili ufaulu masomo ya sayansi kwa One kali lazima uende ukapige mapindi kwa tuition center za Dar (Mgote, Moody, Mtiga, Mbuga etc).
Hilo sio kweli, sio kweli, ni uongo.

Mie sikuwahi kusoma tuition yoyote Dar. Nilipiga mapindi ya vichochoroni tu.
Mengine tulifundishana na wenzangu shule. Na topic zingine niliamua kusoma mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kunifundisha (mfano Modern Physics, Static Electricity, Complex Numbers, Statistics).

Vijana acheni kulala, wekeni malengo ya kupiga One kali ili inapofika stage ya kuomba vyuo unak ua na wide selection ya kwenda chuo na course unayotaka.
Lazima upige One ya 3.

upload_2018-7-25_0-23-3.png

 
kwenye miti hakuna wajenzi.. yaani na ma AAA yako yote umeishia kuajiriwa serikalini kwa mshahara wa hazina... ma scholarship yote yaliyojaa duniani umeyaacha unahangaika na forex na mwisho wa siku unatapeliwa na wadogo zako kina ontario...

wahuni wana div 3 za mwisho tena za HKL ila ajira za maana kwenye mabalozi.. au wanajiajiri wenyewe wanagombania tenda na kupiga hela..

nashangaaga sana best students kuwaona udsm... ukikomaa kweli kweli na ukawa na washauri sahihi unatembea mapema sana.. bongo nyoso
 
Naam. Kwa hisia ulizoandika hapo juu, sina shaka kuwa form six ulipata Division III ya 17 (kidogo ulambe Four *****).
Uka apply UDSM pale CASS (siku hizi CoSS) course ya PSPA ukakosa admission sababu ya competition.
Kisha TCU walivotangaza second selection ukaamua kuomba SAUT tawi la Tabora ndipo ukabahatika.

hata chuo sijafika.. ila maisha nayoishi ni wachache sana wameyafikia.. mimi hata a level sijasoma.. niliishia o level tu then college ya kizushi kisha nikazama mtaani.. karibu sana tupambane kitaa.. huku hakuhitaji A za physics bali ni kujua kuusoma mtaa
 
Maana yake rahisi ni kuwa matokeo yako ya Form Four yalikua mabaya, ULIFELI.
Ndio maana ukaishia O level ukajiunga chuo cha kizushi. Mtu aliyefaulu hawezi kujiunga chuo cha kizushi.
Hukua na option. Umefuata maisha yanavokupeleka, na sio maisha yakufuate wewe unavopanga.

unajua kusoma chemistry ila hujui kuusoma mtaa.. utapata tabu sana... dunia ya sasa haitaki vyeti inataka skills na maujanja ya mtaaa
 
Maana yake rahisi ni kuwa matokeo yako ya Form Four yalikua mabaya, ULIFELI.
Ndio maana ukaishia O level ukajiunga chuo cha kizushi. Mtu aliyefaulu hawezi kujiunga chuo cha kizushi.
Hukua na option. Umefuata maisha yanavokupeleka, na sio maisha yakufuate wewe unavopanga.


kuna shule ukisoma hata ufeli vp huwezi feli kwa kukosa C tatu.. o level feza boys japo sikufaulu vya kutisha ila ningetaka a level ningeenda tu
 
kwenye miti hakuna wajenzi.. yaani na ma AAA yako yote umeishia kuajiriwa serikalini kwa mshahara wa hazina... ma scholarship yote yaliyojaa duniani umeyaacha unahangaika na forex na mwisho wa siku unatapeliwa na wadogo zako kina ontario...

wahuni wana div 3 za mwisho tena za HKL ila ajira za maana kwenye mabalozi.. au wanajiajiri wenyewe wanagombania tenda na kupiga hela..

nashangaaga sana best students kuwaona udsm... ukikomaa kweli kweli na ukawa na washauri sahihi unatembea mapema sana.. bongo nyoso
unaizungumziaje forex
 
Maana yake rahisi ni kuwa matokeo yako ya Form Four yalikua mabaya, ULIFELI.
Ndio maana ukaishia O level ukajiunga chuo cha kizushi. Mtu aliyefaulu hawezi kujiunga chuo cha kizushi.
Hukua na option. Umefuata maisha yanavokupeleka, na sio maisha yakufuate wewe unavopanga.
Sijui kwa nini umeamua kubisha na watu wenye akili ndogo mkuu, Sisi wengine ni member wa professional site kama stackoverflow kule kuna criteria za mtu kuchangia sio kile mtu anakua na iyo priviledge so huwezi kukuta upumbavu kwenye vitu positive. Kudos lakini naona umefuata njia ya mengi kureveal the thruth japo mara nyingi hua sio kweli kwa uzoefu wangu.
 
hongera sana mkuu,mimi nilisoma kwa kila namna lakini ilifika kipindi akili inaniambia ili somo uwezo wako nikupata F au D yaani kwa kifupi Mungu ametuumba kiakili uwezo tofautitofauti.
Yaani unasoma mpaka inafikia kipindi unaona somo halieleweki sawa na kusukuma mlima kilimanjaro
 
Naam. Kwa hisia ulizoandika hapo juu, sina shaka kuwa form six ulipata Division III ya 17 (kidogo ulambe Four *****).
Uka apply UDSM pale CASS (siku hizi CoSS) course ya PSPA ukakosa admission sababu ya competition.
Kisha TCU walivotangaza second selection ukaamua kuomba SAUT tawi la Tabora ndipo ukabahatika.
Sikua na mpango wa kucheka,but nimejikuta nacheka tu
 
Back
Top Bottom