Vijana maelfu wachangamkia fursa 33 za ajira za mahakama. Serikali ifanye mapitio sera ya ajira.

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Nimeambiwa na rafiki yangu mmoja ambaye leo tar 11 Feb. 2018 alikwenda kwa KATIBU TAWALA wilaya mojawapo ya hapa mjini Dar es salaam.
Kasema ndani ya masaa 2 aliyoshinda hapo viwanja vya ofisi ya Katibu tawala amekutana na vijana wenzake kama 50 hivi waliopeleka ombi la kupitishiwa barua zao ili ziende TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA.
Sasa kama ndani ya masaa mawili vijana walikaribia hamsini, je, kutwa mzima walifika idadi gani?
Je, wiki moja watafika idadi gani?
Hiyo ni wilaya moja, au tufanye ni mkoa mmoja kwakuwa Dar ni jiji. Je, Tukijumlisha Tanzania yote tutapata idadi gani?
Sera ya ajira na vijana ipitiwe upya kwa haraka. Serikali na taasisi binafsi hasa NGOs waangalie namna ya kumkomboa huyu kijana.
 
Kama serikali hazifanyi mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kusimama na watu kuajiriwa na kujiajiri watarajie siku za mbeleni machafuko kutoka kwa kundi la vijana.
Mtu akitaka kuanzisha hata NGO au kakiwanda kadogo masharti yake sio ya kawaida. Mara NEMC, TFDA, Manispaa, TRA, BRELA, OSHA, TBS, Wizara n. k.

Haya Mambo wanayaona ila kwa kuwa baadhi yao bado wanapenyeza mtoto wa shangazi na mjomba nahisi hawaelewi somo bado, Yale ya Tunis kijana kujiwasha petrol bado yanakuja hapa kwetu.

Wanakomaa kuwaambia wajiajili, lakini mathalani mtu anamaliza chuo, bila mazingira wezeshi na uchumi huu, biashara ngumu, nani anaweza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom