Vijana lazima tujifunze, aliye nacho huongezewa!

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,456
17,204
20211111_042855.jpg


Crdb bank wanampongeza makamu mwenyekiti wa bodi yao kuteuliwa kua mwenyekiti wa bodi ya ATCL.

Maana yake huyu ni mjumbe wa bodi 2 na nyingine nyingi, hapo posho za vikao sio za kitoto. Wakati huo huo ni mwalimu wa chuo kikuu.

Juzi mliona wajumbe wa Jakaya Kikwete Foundation, wengine DCB Bank wameteuliwa pia kua wajumbe wa tanesco na bado tena wengine wakateuliwa nafasi za wizara ya fedha na nyingine kibao.

Hii inatufundisha kwamba mwenye nacho huongezewa na asie nacho hata kile kidogo alichonacho hunyang'anywa. Na huu ndio mfumo uliopo sasa. Pia hao hao wenye nazo ndio watakaowapa nafasi watoto wao ana ndugu zao kuendelea kula keki ya taifa wakati vijana wengi mkilipwa elfu 10 kusifu na kuabudu mitandaoni.

Vijana lazima mbadilike, hii nchi ni yenu. Mkiendelea kutumika kwa kupewa elfu 10 na kusifia mitandaoni mtakufa makisini nyie na familia zenu mkiacha layer ya watu wachache na vizazi vyao wakila nchi miaka na miaka.

Shauri zenu.
 
Na mimi naungana na CRDB kumpongeza Prof. NEEMA MORI na pia nawakumbusha vijana wenzangu kufika hapo inawezekana.
 
Back
Top Bottom