Vijana kuweni wakweli,kwanini ujipandishe juu?Ona hii!!...

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,694
Huyu anasema hatarudia tena huu ujinga!,...Anasimulia....Walipokua wanaishi baba yake alimwomba jirani amfundishe udereva huyu dogo.....Anasema....Nakumbuka jion siku ya tukio alikua ameenda bar kupata moja baridi baada ya mikiki mikiki ya kujifunza kuendesha lori la mchanga huku nae akiwasaidia kazi ile!Wakati anakunywa,dada mmoja alinyanyuka kwenda kuwasha gari lake ili aondoke,mara gari likagoma kuwaka,kijana akanyanyuka kwenda kumsaidia na akafanikiwa,gari likawaka,yule dada akataka kumlipa jamaa akakataa badala yake akaomba namba ya simu,akapewa,dada akamuuliza kama anaishi maeneo yale jamaa akajibu 'hapana mimi huwa nakuja huku kukagua miradi yangu' jamaa baada ya wiki ya mazoea akarusha huku akidai ana miradi mingi.Siku ya 'noma' ikawadia,walipeleka mchanga saiti,wakiwa wanasawazisha mchanga na makoleo huku jamaa amechafuka 'kinoma' mwenye saiti akafika mara akasalimia,kumbe ni yule dada,yule dada alimtazama sana jamaa akataka kusema jambo akaghairi nadhani alifikiri amemfananisha.Dereva ambae ni mwalim wake akaharibu kila kitu alimwita kwa jina akisema"malizia fasta tunadaiwa tripu tano hapa"yule dada alimwambia jamaa"kumbe ni wewe nini kimetokea tena?"jamaa alishindwa kujibu akawa amepigwa butwaa,kisha yule dada akamwambia"tutaongea kwenye simu"jamaa anasema alizima simu wiki nzima.Siku hizi akiulizwa kazi anasema ya kweli!
 
sema ukweli siku hizi wadada hawaangalii hizo, ni mahaba tu kama pesa tunatafuta wenyewe
 
Sio rahisi hivyo,wanawake wakati mwingine bila uongo hamuendi,ila huyu alizidi!

Sio kama alizidisha, hivyo ndivyo inavyotakiwa, maana baadhi ya wadada wa siku hizi bila (Zaidi) ya fix hawakubali, formula zote zilikuwa sawa nafikiri alikosea wakati wa kuingiza data kwenye calculator..!
Mmh, ila sipati picha, jamaa atakuwa alikuwa mdogo zaidi ya piritoni...!
 
Usijidanganye! kwa nini uongope? kuwa mkweli tu. Uongo utakuumbua!
Tatizo msipodanganywa kidogo hamuelewi nyie,...yaani asikuongopee mtu ukitaka kuipua kifaa cha ukweli uongo kidogo ni muhimu saaaaaana,........sema isiwe too much...eti oooooooh_Mengi ni mwenyekiti wa makampuni yangu
 
madada acheni zenu,bila uongo kidogo hamuingiliki...haikua bahati yake ajipange tena atapata mwengine tu
 
sema ukweli siku hizi wadada hawaangalii hizo, ni mahaba tu kama pesa tunatafuta wenyewe

Hapo kwenye blue wenye mahaba ya kweli ni wachache..........
Kwenye nyekundu ingawa wapo wanaotafuta pesa wenyewe lakini pesa za wanaume wanazihitaji sana...
 
Hapo kwenye blue wenye mahaba ya kweli ni wachache..........
Kwenye nyekundu ingawa wapo wanaotafuta pesa wenyewe lakini pesa za wanaume wanazihitaji sana...
naunga mkono hoja...
 
Ujiko mtamu bana, asikwambie mtu, hasa kama unamtokea mwana JF mwenzio kwa kum-PM, ndio usiseme..............LOL
 
Alikomeshwa kweli kweli
hakukomeshwa, tena hajakosea jambo kwakuwa bado alikutwa kwenye mradi wake wa kujifunza gari. kwani huo siyo mradi?. labda kama alisema aina ya mradi anayofanya mahali pale na ikaonekana iko tofauti nahiyo alikutwa nayo. ni woga wake tu. yaani mimi ndo ningesalimiana na bibie kwa majidai yote, na bibie angenipa credit kubwa kwani nilikataa pesa yake, ili hali mradi wangu ni wa kichovu, ni ukomavu huo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom