Uchaguzi 2020 Vijana kuweni makini kwa ahadi za uongo kutoka Vyama vya Upinzani

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Baada ya kufuatilia hotuba nyingi za Vyama vya Upinzani ninapenda kuwasihi vijana kuwa na tahadhari kwa ahadi zisizoweza kutekelezeka.

Nikianzia suala la ajira ni tatizo la sehemu kubwa duniani watu wamepoteza kazi kwa hali mbaya ya kiuchumi pamoja na tatizo la ugonjwa huu wa COVID19 ulipojitokeza.

Suala la kusema kuwa wakishika madaraka wataruhusu wananchi wataruhusiwa kwenda kuishi kwenye hifadhi ni la upotoshaji mkubwa kwani tukiruhusu utekelezaji huo ina maana utalii utakufa.

Ninatoa mfano nchi ya Misri 2011 wananchi walimuondoa madarakani Rais Hussein Mubarak kupitia chama cha Muslim Brotherhood baada ya chama hicho kutoa ahadi nyingi zisizoweza kutekelezeka kufika mwaka 2013 wananchi hao hao waliiingia mitaani kupinga hicho chama matokeo Jeshi la nchi hiyo likatwaa madaraka tena.

Tumeona hapa majirani zetu Kenya baada ya kuiondoa KANU madarakani na kupata katiba mpya leo wakenya wanaikumbuka KANU kwani Ufisadi na ukabila umekuwa mkubwa sana kufikia kuhatarisha umoja wa nchi hiyo. Katika uchaguzi wa mwaka 2007 wananchi kupitia vyama hivyo vilipigana vita vya kikabila na maelfu ya wananchi walipoteza maisha.

Kwa mustakabali wa nchi yetu Tanzania bado CCM ni chama pekee kinachoweza kuipeleka nchi katika uchumi mzuri na umoja wa kitaifa.

Tusijaribu kufanya kosa kubwa la kutoipigia kura CCM na haswa Rais Magufuli ambaye ameleta mageuzi makubwa ndani ya chama hicho na serikali kwa ujumla.
 
Ukosefu wa ajira nchi hii haujasababishwa na corona, upo miaka yote hasa hii ya Magufuli. Kwanza corona Tanzania haipo, sasa hizo ajira zimepoteaje wakati corona haipo?

Ccm kwa miaka zaidi ya 60 imeshindwa kuleta maendeleo leo hii ndio ilete maendeleo?

Magufuli amefanya kitu gani? Kununua ndege na kujenga madaraja? Leo hii karne ya 21, miaka 60 ya uhuru unakuja kutuambia madaraja na ndege ndio mabadiliko ya maendeleo? Wakoloni walifanya haya miaka zaidi ya 60 iliyopita.

Ccm ambayo imekua ikitoa ahadi zisizotekelwzeka kwa miaka 60 unaizungumziaje? Mfano ahadi ya 50m kila kijiji?

CCM hata ipewe miaka 500 haina mbinu mpya tena ya kutuvusha kutoka sehemu moja kwenye nyingine. Hapo ilipofika imefika mwisho.
 
1.wewe ni nani hata utufokee vijana?
2.Mageuzi ndani ya chama yanatuhusu nini sisi?
3.Mambo ya Misri usituambie kabisa
4.Hakuna anayesema kutakuwa na ajira 100%,mmefanya mambo ya hovyo yaliyopelekea kupungua kwa ajira

#USITUFOKEE
Vijana hamtaki kabisa kufokewa.
 
1.wewe ni nani hata utufokee vijana?
2.Mageuzi ndani ya chama yanatuhusu nini sisi?
3.Mambo ya Misri usituambie kabisa
4.Hakuna anayesema kutakuwa na ajira 100%,mmefanya mambo ya hovyo yaliyopelekea kupungua kwa ajira

#USITUFOKEE
Mkuu sikufokei ila nimetoa mfano hai kwa nchi ambazo zimepitia njia mnayotaka kutupeleka
 
Ukosefu wa ajira nchi hii haujasababishwa na corona, upo miaka yote hasa hii ya Magufuli. Kwanza corona Tanzania haipo, sasa hizo ajira zimepoteaje wakati corona haipo?...
Sasa huyo anayeishi Belgium anaweza kutekeleza ahadi hizo kweli ama anataka atulete matatizo halafu asepee
 
Kijana La kuambiwa na Lisu Changanya na akili zako .Lisu ana uongo wa kufa mtu

View attachment 1560044

Mgonjwa wa akili wewe,

1. Hiyo ndege ya kwake Lisu? Je ukiiuza utajenga viwanda vingapi?

2. Ndege alizonunua maguli zimechukuwa budget ya shilingi ngapi?, tungeamua kujenga viwanda vya nguo tungepata vingapi? Direct employment kiwanda kimoja 4000 workers bado madreva, mama lishe, wachuuzi nk

3. Sasa hivi hiyo midege alonunua Maguful inaingiza kiasigani? Je kunamanufaa yoyote?

Mjinga mkubwa wewe.
 
Mbona Magufuli alitudanganya milioni hamsini kila Kijiji, Ajira na nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi lakini mpaka Leo anamaliza miaka yake mitano milioni hamsini hatujaziona, Ajira Hakuna tokea 2015 na wafanyakaz hajawajapandishiwa mishahara tokea 2015?

Ulitakiwa kutueleza uongo wa Magufuli kwanza ili tusimchague Tena maana kashatudanganya tukampa hivyo hatupaswi kurudia kosa Tena.
 
Back
Top Bottom