The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,320
Hua nasema kila siku, CCM hata wakipewa miaka 700 hakuna kitu watatufanyia watanzania zaidi ya kutufukarisha. Miaka na miaka CCM inazalisha mafukara wa kutupwa wanaoitwa wanyonge ambao mbaya zaidi ccm inawatumia tena kama stepping stone kwenye uchaguzi.
Kijana wa Kitanzania kutegemea utatoka kwenye serikali hii ya Awamu ya 5 ya wanyonge ni ndoto za mchana.
1. Miaka 5 hakuna ajira na wala hakuna mkakati wa kuondoa tatizo la ajira, ccm watakuja na jibu jepesi tu kua tatizo la ajira ni la kidunia. Waliomaliza vyuo toka mwaka 2015 99% hawana ajira ya kueleweka, na bado serikali wala haina mkakati mahsusi kupunguza hili tatizo.
2. Ukitegemea biashara, biashara hazieleweki, hazifanyiki, ukipata mtaji wako unaisha kabla hujaanza biashara, mara osha, tra, ushuru halmashauri, tfda, serikali za mtaa, bwana afya, kote huko unatakiwa kulipa kabla ya kuanza kufanya biashara. Gharama za hizo leseni mtaji umekata kabla hujaanza biashara.
3. Ukipata pesa yako ujenge kibanda simenti mfuko 25,000 hadi 35,000, gharama za ujenzi ziko juu sana, nondo, mabati, vigae, mbao bei ghali kama vile tunaagiza kutoka Malaysia. CCM watakupa majibu mepesi kua miradi ya maendeleo ndio umepandisha bei simenti, hawana mikakati endelevu kama ilivyo kawaida yao. Hapa kijana usitegemee utatoboa.
4. Huwezi kununua gari, kodi za magari ni mara 2 ya bei ya gari, ccm bado wanaamini gari ni anasa na sio basic need. Karne ya 21 bado ccm wanaamini gari ni luxury goods hivyo iwe highly taxed, bado wana mawazo ya karne ya 19. Hapa kijana usitegemee utatoka. Ukijikongoja sana utaishia kununua kimkweche cha mwaka 2003 ama 2004, 16 years old car.
5. Mitaji haipatikani, ukisema ukakope benki riba juu sana, 20%-24% na biashara hazitabiriki hivyo utaishia kufilisika tu. Hawana mkakati wowote kufanya benki zishushe riba.
Kijana kama unategemea utatoka chini ya serikali ya ccm unaota ndoto za mchana. Ndio maana pamoja na ccm kutawala miaka 60, 80% ya watanzania ni mafukara wa kutupwa. Juzi waziri Mpango amakiri kua pamoja na kua tuko uchumi wa kati ila umasikini ni mkubwa sana.
Hii mada inaendelea.