Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Mada yangu inatokana na Swali nililoulizwa na Mwana JF mwenzetu WildCard katika moja ya mijadala yetu humu ndani; WildCard aliniuliza hivi:
Hili ni swali la msingi sana, hasa kwa Vijana wenye shauku to pursue career zao kwenye Siasa aidha kupitia CCM, Chadema au Vyama vingine; Ndio maana badala ya kumjibu WildCard kwa ufupi, nikaonelea nilipe uzito wake wa kipekee kwa kufungulia uzi wa mjadala;
Tumeshuhudia vijana wakimiminika kwa wingi kukimbilia kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa ndani wa Chama uliomalizika hivi karibuni; Kutokana na wingi huu wa vijana, CCM imekuwa ikijisifia sana kwamba ni chama chenye mvuto kwa Vijana, tena Wasomi; Je kuna ukweli gani katika hili?
Kabla sijaenda mbali na mjadala wangu, ningependa kwanza kuijadili kidogo MEDIA yetu Tanzania; Binafsi naamini kwamba MEDIA ni moja ya mihimili mikuu ya Dola (at least informally), pamoja na Bunge, Mahakama na Executive; Kutokana na uzito wake katika taifa, sekta ya MEDIA inatakiwa wakati wote isimamie ukweli, haki, uadilifu, na iwe ni mfano wa kuigwa katika jamii; Tofauti na haya, kwa kiasi fulani, kinachoendelea nchini ni Utamaduni wa baadi ya vyombo vya habari kufanyia mzaa mzaa suala la uongozi wa UMMA, hasa pale Magazeti Makubwa na Yenye Heshima na pia ushawishi katika Jamii yanapokuja na Vichwa Vya Habari kama vile: FULANI NA FULANI WAULA.; Ukisoma kwa undani unakuta ni habari za watu fulani fulani kuteuliwa kushika nafasi za UMMA;
Nabakia kujiuliza, Tangia lini Kupewa Uongozi wa Umma imekuwa ni Kuula? Hii inatuma ujumbe gani kwa watoto wetu wenye ndoto za ku-pursue careers in politics huko mbeleni? Jibu ni rahisi tu Uongozi wa Umma Ni kwenda Kula! Ni kwa mtindo huu, ajira ya umma sasa inakuwa treated kama vile ni Ajira Vodacom, Barclays, Tigo n.k; Nakumbuka nikiwa mtoto, ajira za Umma zilikuwa zinapokewa na wahusika kwa woga na wasiwasi mkubwa kwani walikuwa wanafahamu kwamba kilichotokea ni Rais au Mwenyekiti (Nyerere) kuwapa dhamana, sio fadhila; Isitoshe, teuzi zote zilikuwa zinafanywa siri kubwa, na ilikuwa ni kawaida kusikia umeteuliwa au umefukuzwa kazi aidha kwa kupitia Redioi au barua rasmi; Tofauti na miaka ile, miaka ya sasa mtu kuwa waziri, mjumbe wa kamati kuu CCM, mbunge (hata wa jimbo), balozi, unaambiwa mapema kabisa hata ukiwa kwenye baa;
Nikirudi kwenye yangu ya msingi inayotokana na Swali la Wildcat hapo juu, napenda kuijadili kama ifuatavyo:
Haya ni matokeo ya PERSONAL INVESTMENTS in Reciprocal Relations ambazo wengi ya Watu, hasa Vijana uwekeza kwa Viongozi wa CCM na Serikali yake, kama njia ya kufanikisha malengo BINAFSI - yani ya vijana hawa, malengo ambayo ni dhahiri hayawezi kufanikiwa nje ya CCM; Tutayaona malengo hayo punde; Hii ni tofauti na mtazamo wa kufanikisha malengo ya UMMA ambayo ni dhahiri yanaweza kufanikiwa kupitia Chama chochote Cha siasa, sio CCM Peke yake
Kwa vijana wengi, the sought goods (bidhaa wanazotafuta) hazina uhusiano na PUBLIC GAIN (wananchi), na badala yake uegemea zaidi on PRIVATE GAIN (matumbo yao na familia zao); Bidhaa hizi ADIMU ambazo hutafutwa na Vijana Wengi wanaokimbilia uongozi CCM ni pamoja na Prestige, Social Status & Wealth, ambazo nadhani tunakubaliana kwamba:
They have Scarcity Value - kwa maana ya kwamba they may be available, but they may not be accessible to many; Kutokana na sifa hii, ndio maana Vijana wengi hutumia kila njia to invest in relations na CCM, Viongozi Wa Chama Ngazi Wa Mbalimbali, na Viongozi wa Serikali ya CCM kwa ujumla wake, kama njia rahisi ya kupata Bidhaa hizi adimu;
Enzi za Mwalimu, CCM ilikuwa ina hazina kubwa sana ya Viongozi Bora kutokana na matumizi ya utaratibu wa Leadership Recruitment ambao ulikuwa unazingatia sifa za mhusika kama vile Elimu, Uzeofu, Ufahamu wa Chama, Uzalendo Kwa Taifa, Rekodi Safi katika jamii, Uadilifu, n.k; Miaka ya sasa, CCM imejaa Bora Viongozi (badala ya Viongozi Bora), kwani Chama kimeachana na Leadership Recruitment na kudandia mfumo wa Leadership Succession ambapo sifa kuu zimegeuka kuwa ni uwezo wa fedha, ukaribu wako au wa wazazi wako na viongozi wakuu wa Chama na Serikali ya CCM, Ukabila, na Udini (both ukristo na uislamu);
Mbali ya haya, tofauti na wakati wa Nyerere ambapo mtu alikuwa anapandishwa cheo kutokana na performance, integrity na patriotism, na mengineyo yenye maslahi kwa taifa, inaelekea kwamba nyakazi hizi vigezo vikuu ni pamoja na mtu kuwa ignorant (hata kwa makusudi), irrational, dishonest and stubborn (hasa in relation to wapinzani); Kutokana na hili, CCM ni nadra sana kutumia siasa za akili, kwani intellectuals hawapewi nafasi na badala yake, wenye kutamba ndani ya chama ni ideologues, demagogues and jesters; Na ni bahati mbaya sana kwamba hata intellectuals wanaofanikiwa kupenya ndani ya chama, most of them end up being ideologues, demagogues and jesters;
Kwa kumalizia, pengine ni muhimu nikajadili na kutofautisha Leadership Succession na Leadership Recruitment, japo kwa ujumla wake;
Leadership Succession
Succession ni mchakato unaohusisha transfer ya uongozi kutokea kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kundi moja kwenda kwa kundi lingine; Mafanikio ya mfumo huu hutegemea sana sheria zilizopo (relevant laws), historia ya jamii husika, na utamaduni wa jamii husika; Pale ambapo sheria na utamaduni unakuwa observed, leadership succession inaweza kuwa effective & peaceful; Lakini kwa ujumla wake, leadership succession katika nchi zetu Afrika kwa kiasi kikubwa imekuwa ni zao la crude political manipulations, maasi au mapinduzi ya kijeshi, kuliko a peaceful application of the constitutional process. Tatizo hili linachangiwa sana na the fact kwamba - Constitutionalism is not well founded in Sub Saharan Africa (hata Tanzania), na pia linachangiwa na tabia/utamaduni wa kufanya Politics iwe ni Supreme Kwa masuala mengine yote ndani ya taifa;
Leadership Recruitment:
Huu ni mchakato ambao hufuata utaratibu wa - identification, nurturing, education and training of youths ili waje kuwa hazina ya uongozi siku za usoni; Na ili mfumo huu ufanye kazi, ni lazima kuwepo na an enabling environment & supporting institutions na kwa utaratibu unao ongozwa na kanuni, sheria, & codes of conduct, whereby potential leaders (hasa vijana) wanaweza kuwa identified, attracted, nurtured and trained. Uwepo wa mfumo wa namna hii unasaidia sana kuvutia independent individuals wenye talent, elimu, upeo, Uzalendo, mwono (vision), mawazo na ambition to pursue political career kwa manufaa ya taifa lao;
Muhimu:
1. Kwa mazingira ya Sasa, sio lazima Vijana wa namna hii wapatikane kupitia UVCCM peke yake, bali wanaweza kuwa ni wananchi wa kawaida wasio na chama chochote, lakini they are motivated to play an active role in public affairs, kwa manufaa ya taifa lao la Tanzania;
2. Ingawa tatizo hili la Leadership Succession lipo practiced sana katika CCM ya nyakazi hizi, Jinamizi hili pia limeshaingia Chadema, na ni muhimu kwa Chadema kulifukuza Jinamizi hili kama kweli nia ya Chama hiki ni kuaminiwa na UMMA kuipokea Madaraka CCM aidha 2015 au Baadae;
Nikuulize jambo moja Mchambuzi: Kwa nini bado watu na akili zao timamu kabisa wanabanana kugombea nafasi za UONGOZI ndani ya CCM inayokufa kwa kasi hivi? Au hili linafanana na masuala ya ngono na ukimwi (nisamehe kwa lugha hii ya kuudhi)?