Vijana kugombea Uongozi CCM: Je, Wachofuata ni nini?

Mgaya D.W & Bongolander, nawashukuru kwa hoja nzuri, ntawarudia;
 
Viongozi vijana nchini Tanzania wamegawanyika katika makundi mawili. (1) Real Leaders and (2) Leaders Wannabees.

Aina hizo mbili za viongozi wanaweza kutofautsiha kama ifuatavyo:

Viongozi wa kweli huwa hawafukuzii, kufuata na kulazimisha uongozi. Badala yake uongozi huwafuata wao. Hata pale wasipotaka kuwa viongozi with time hujikuta wamewekwa katika nafasi ya uongozi na watu, mazingira au matukio. Mfano Mzuri wa viongozi wa kweli ni John Mnyika. Kijana huyu mdogo anaweza uongozi na popote alipo apende asipende hujikuta amewekwa katika nafasi ya uongozi na mazingira, watu au matukio.Leaders wannabees, on the other hand, hulazimisha, kupigania na kugombania uongozi kufa na kupona. Hawa ni wale watu wanaogombea kila uchaguzi unaotokea.

Hawa ni viongozi wanaohonga hela nyingi, kupigana kufa na kupona na kufanya lolote liwezekanalo ili kupata nafasi ya uongozi. Mifano michache ya leaders Wannabees ni William Malecela Le Mutuz na Shyrose Banji. Vijana hawa ni mfano mzuri wa Leaders Wannabees kwakuwa ni wao wenyewe tu wanaodhani wanaweza kuongoza na hivyo huwa wanagombea kila uchaguzi, hutumia muda na rasilimali nyingi kutafuta, kufukuza na kugombania uongozi kwa udi na uvumba.

Kwakiasi kikubwa hawa ni vijana wasiojijua wala kujifahamu wao wenye. Ni watu ambao wanashindwa kuelewa wao ni watu wa aina gani na hivyo wazingatie mambo gani katika maisha. Badala yake wao wanapoteza muda kwenye suala wasiloliweza la uongozi.

Utawezaje kuongoza nafsi nyingine wakati wewe mwenyewe huijui nafsi yako (kipofu anajaribu kuonyesha njia). Msomaji jiulize wewe mwenyewe, je unategemea jambo lolote la maana kutoka kwenye ubunge wa Shyrose Banji?

Viongozi wa kweli wana wafuasi (followers). Huwezi kuwa kiongozi kama huna wafuasi. Wafuasi hufuata viongozi wa kweli wapende wasipende. Leaders Wannabees, on the other hand huwa hawana wafuasi. Hata wanapolazimisha na kupata nafasi ya uongozi hakuna mtu yeyote atakaevutiwa kuwa mfuasi wao.

If anything huwa wanaishia kuwa na vibaraka(puppets) wanaojipendekeza kwao ili kujipatia mradi wao (tumikia kafiri). Mfano mzuri wa Leaders Wannabees -- wenye kundi la vibaraka -- ni Mfalme Suleiman wa Tanzania. Mzee huyu amezungukwa na kundi kubwa la vibaraka walioko busy kusema sawa mzee ili wajipatie mradi wao. Huyu Mzee ni mfano mzuri wa kiongozi feki asiye na wafuasi. Benno Malisa wa UVCCM ni mfano mwengine mzuri wa watu waliopata nafasi ya uongozi lakini wakashindwa kujipatia wafuasi kwakuwa hakuwa na uwezo, wala sifa ya uongozi.

Viongozi wa kweli wanasifa na uwezo wa kuongoza. Ukipata nafasi ya kuwajua viongozi wa kweli wewe mwenyewe utaona kuwa ni watu wenye sifa na uwezo wa kuongoza (Charisma). Ni watu jasiri, wasiofuata mkumbo, wenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu na kusimamia maamuzi yao.

Wakipewa nafasi ya uongozi, hufanya kazi zao kwa ustadi mkubwa unaoleta manufaa kwa wanaowaongoza. Leaders Wannabees on the other hand huwa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza. Wakipata nafasi ya kuongoza hufanya mambo yasiyo na manufaa na kuishia kujinufaisha wao binafsi. Ni watu dhaifu, wakufuata mkumbo, wasio na uwezo wa kufanya maamuzi magumu au kusimamia maamuzi magumu.

Viongozi wa kweli ni watu wanaosimama kwa miguu yao wenyewe kiuongozi (self made). Hawabebwi na majina, maGod Father au upendeleo. Leaders Wannabees on the other hand ni watu wasio na uwezo wa kusimama wenyewe (they are not self made). Ni watu wanaotegemea majina ya ukoo au wazazi. Na ni watu wanaopata upendeleo wa wazazi au ujamaa ili kukwea ngazi za uongozi .

Viongozi wa kweli watadumu na kuwa na maisha marefu katika Nyanja ya uongozi. Leaders Wannabees ni upepo tu- Wanakuja na kupita.

Unaweza kuchangia zaidi mjadala wa aina kuu mbili za viongozi vijana TZ kwa kufuata thread hii hapo chini

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/356432-aina-kuu-mbili-za-viongozi-vijana-tanzania.html

Ni kweli UVCCM ya sasa hivi siyo ile ya enzi za Mwl Nyerere pamoja na kwamba kichwa cha mada yako kinakuwa kama vile kina unazi fulani ndani yake hasa pale unapoleta chagizo la mchango wa 'WildCard' lililokupelekea kuleta mada.

Kitu ambacho kila mara kinakera ni jamii kuzidi kulinganisha mfumo uliopo na wa enzi za Mwl Nyerere. Halafu wana hitimisha kwa kusema wa enzi za Mwl Nyerere ulikuwa ni bora zaidi ya huu.
Dunia ya sasa siyo kama ile iliyokuwa enzi za Mwl Nyerere na Tanzania ndivyo hivyo. Political landscape has changed for better not just in Tanzania but in the whole world.

Jaribu kuangaza katika dunia ambayo imetuletea huu mfumo wa siasa za sasa na jibu utakalolipata ni kuwa, katika siasa hizi 'there's no free lunch' na 'charity' start at home kwa maana kuwa, primarily, watu wanaingia katika siasa siyo kwa mapenzi na utashi wa kuwatumikia wananchi kwanza bali hili linakuwa ni secondary choice. Na hii utaiona kwa wabunge wetu pia ambao kabla ya kuwa waheshimiwa, wengi wao maisha yao yalikuwa ni ya kipato cha chini kama siyo duni lakini baada ya kuingia kwenye siasa, kwa sasa ni mamilionea. Huu mfumo, hauna 'Mama Thereza'. Do you know, how many million if not billion dollar spend by people or companies on U.S.A politics to lobby politician or put their own people or did you heard about the scandal of MP in United Kingdom fiddling their expenses for their own gain. Point yangu ni kuwa, hili ni tatizo la siasa ambazo tunazi copy kutoka nchi za magharibi na haiwezekani kuliepuka labda tu turudi tena kwenye siasa za Mwl Nyerere.

Mazingira ya kisiasa ya wakati ule yalimuwezesha Mwl Nyerere kuwa na hiyo anasa ya Leadership Recruitment kwa sababu the guy was having absolute power in our country. Jamii haikuwa na jinsi bali kufuata yale aliyokuwa akiyaamini. Kushindwa kufanya hivyo ilikuwa ni tiketi ya kutengwa, kudhalilishwa na hata kutupwa gerezani. Don't be fooled to think and believe that every person who came through Mwl Nyerere Leadership recruitment alikuwa kweli ana hizo sifa naturally na kwa mapenzi, utashi na matakwa yake badala ya kulazimishwa na system ambayo ilikuwa hairuhu uhuru wa kibinadamu katika kujiamulia mambo yao.

Tuko kwenye system ambayo maslahi binafsi yanatangulizwa mbele na pale ambapo kuna maslahi au uwezekano wa kuwepo, watu ndio hukimbilia. It's true, demokrasia ya sasa ina 'scarcity value' kwa vile inabeba pia gharama binafsi na ambayo ina reward in terms Prestige, social status and accumulation of wealth. Namba ya watu watakaojitokeza kugombea Uchaguzi ujao wa ndani CHADEMA itatuonyesha kama jamii imeanza kuona kama kuna maslahi ndani ya chama au la. ndiyo maana hata heading yako hukuchagua UDP, TLP kiwe ndiyo kiini cha mazungumzo kwa vile ulijua kabisa hutapata watu wengi watakaoguswa na mada yako.

Ni wazo langu..
 
Uliyoyaongea yana ukweli lakini ndugu Mchambuzi bado anapoint zaidi katika hili. Kama ulivyosema wakati wa Nyerere sio wote walikuwa waadilifu by choice. Wengine walikuwa hivyo kwa kuogopa mkono wa chuma wa Mwalimu. Well kwa kuwa Mwalimu hayupo sasa haina maana watu waanze kuwa wabinafsi na wafujaji wa mali za umma au wachumia tumbo. Kwakuwa Mwalimu hayupo what we need now is a good governance system and the rule of law(invisible hand) kuendelea kuwalazimisha watu kuwa waadilifu kama wakati wa Mwalimu. That is what we need ili kuendeleza maadili serikali na katika sekta ya siasa (kama wakati wa Mwalimu)
 
Nakubaliana na wewe kwa yote uliyoyasema kwa kuongeza point zaidi,

Nafikiri baada ya kuingia kwenye huu mfumo mpya wa uchumi, Nchi ilitakiwa iwe na kiongozi mwenye msimamo mkali na mzalendo wa kweli katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya nchi kwa sababu nchi ilikuwa haijawa na sheria madhubuti za kukabiliana na soko huria. Matokeo yake, nchi iliingiliwa na crooks investor, corrupt government executive and transgressor politician. Matokeo yake, tunaona matabaka makubwa kati ya wenye nacho wachache na masikini wengi yameibuka kwa kasi.

Nchi iko mahali ambapo kwa sasa kikundi cha watu wachache wana influence government policy in our economy na kama watahisi kuna uwezekano wa oposition to take over, watahakikisha wanafanya kila linalowezekana kujipenyeza ili waendelee kuvuna zaidi kwa sababu wanasiasa wetu wengi walishakuwa wabinafsi wa kupindukia.

Angalia Mexico na tatizo la drug cartel. Those guys now are bigger than the Government kwa sababu waliachiwa na corrupt official wakajijenga.
 
Popote unapoona nina ushabiki unatakiwa kupajadili kwa hoja ili nirudi kwenye mstari, kama sisi tunavyosema kila wakati unapokuwa na hoja za kidini na maneno yenye kukashifu badala ya kujenga; Ni kawaida kupitiwa mara nyingine kwani sote nui binadamu na tuna emotions lakini ni muhimu pia kukubali kukosea; vinginevyo umeongea ya msingi sana katika bandiko lako, hasa zile sababu tatu kwanini vijana wengi hujikita katika siasa; hakuna sehemu ulipojadili kwamba kimsingi ni wanaenda kutumikia nchi, na upo sahihi katika hili; vinginevyo kimsingi ni for private gain, suala la public gain ni baadae, ingawa mwenzetu wakurogwa haoni hilo;

Kwanza kabisa ni KICHWA CHA HABARI CHAKO kinachobainisha kuwa Vijana kugombea uongozi CCM. Kwa mtu yoyote makini anakuona wewe ni mshabiki wa chama tofauti na CCM. Kwani siku hizi vijana wengi sana huko Tanzania wametokea kukimbilia kwenye Siasa mfano ulio hai ni kama Vijana wengi wabunge ambao sio CCM kama Zito kabwe, Mnyika, Mdee, Kafurila, Nasari etc. Kwa mfano huo tu unaona kuwa vijana sio tu wa CCM wanagombea uongozi ndani ya chama chao bali vijana mbalimbali wanatafuta uongozi kupitia vyama mbali mbali vilivyosajiliwa kisharia huko Tanzania.

Lakin kwa kukusaidia zaidi ni kuwa CCM siku hizi wameachana na ILE FARSAFA YA NYERERE kuwa VIJANA TAIFA LA KESHO. Kwani farsafa hiyo iliondoa sana vijana katika kugombea au haya upata uongozi mkubwa katika Chama chao.

Lakin la mwisho wachambuzi siku zote wanaanzia kwenye kichwa cha makala yako kabla kuangalia kile ulichobainisha, NAKUSHAURI BADILISHA KICHWA HICHO KISOMEKE VIJANA KUGOMBEA UONGOZI KATIKA VYAMA VYA SIASA, JE WANACHOFATA NI NINI?.

Kuhusu mitazamo yenu kuhusu mimi hilo si jambo la kushangaza kwani huko Tanganyika ile dhana ya UDINi imezidi kujikita na hata neno lenyewe UDINI linamaanisha uislam. Hivyo sitaweza hata siku moja kuikana iimani yangu na nitasema kweli daima.

Kama umechunguza maandiko yangu siku zote najibu kile ninachoulizwa na si vinginevyo. Kumbuka kuwa humu kuna mas'hala mengi, mzaha mwingi na hata kejeli nyingi. sasa kwa mtu makini anajibu kwa jinsi ulivyoulizwa mas'hala kwa mas'hala, kejeli kwa kejeli etc na kama utaona katika mada yoyote ile nimejibu mas'ala katika kitu serious naomba nijuze haraka niombe msamaha kwalo.

Huo ndio mtazamo wangu katika mada yako.

Uliyoyaongea yana ukweli lakini ndugu Mchambuzi bado anapoint zaidi katika hili. Kama ulivyosema wakati wa Nyerere sio wote walikuwa waadilifu by choice. Wengine walikuwa hivyo kwa kuogopa mkono wa chuma wa Mwalimu. Well kwa kuwa Mwalimu hayupo sasa haina maana watu waanze kuwa wabinafsi na wafujaji wa mali za umma au wachumia tumbo. Kwakuwa Mwalimu hayupo what we need now is a good governance system and the rule of law(invisible hand) kuendelea kuwalazimisha watu kuwa waadilifu kama wakati wa Mwalimu. That is what we need ili kuendeleza maadili serikali na katika sekta ya siasa (kama wakati wa Mwalimu)

Kila watu na zama zao. Enzi za JKN hakukuwa na utawala wa sharia bali JKN alikuwa ndio kila kitu.

Kwa kukusaidia mmommonyoko wa maadili kwa Tanganyika ulinza mwaka 1968 baada ya Azimio la Arusha la kutaifisha mali za watu na kuzikabidhi Serikali ambayo ilikuwa haijajitayarisha kuandaa watu wa kuendeleza mali hizo.

lakin mmommonyoka ulizidi zaidi mara baada ya kuleta Vijiji vya ujamaa yaani watu waliondolewa katika fertily areas na kuwekwa majangwani kwa ajili ya vijiji hivyo. Kwani vyote hivi vilisababisha njaa kubwa sana 1974 na uchumi kuporomoka kwa kasi sana sababu ya uzalishaji wa viwanda kushuka sana.

Kumbuka mtu akiwa na njaa ndipo ule uadilifu ukaanza kupotea na kuleta kitu kilichokuwa kinaitwa watu kujilimbikizia mali na kunza kwa biashara za ulanguzi.

Kilichokuwa kinapotea sio tu uadilifu lakin kubwa zaidi ni KUPOTEA KWA UZALENDO ambao wananchi waliokuwa nao kabla na baada ya ukoloni.

Hicho ndicho kinachoitafuna tanzania mpaka leo NI KUKOSEKANA KWA UZALENDO NA UADILIFU. lakin vyote chanzo cha JKN.

Kwanza kabisa ni KICHWA CHA HABARI CHAKO kinachobainisha kuwa Vijana kugombea uongozi CCM. Kwa mtu yoyote makini anakuona wewe ni mshabiki wa chama tofauti na CCM. Kwani siku hizi vijana wengi sana huko Tanzania wametokea kukimbilia kwenye Siasa mfano ulio hai ni kama Vijana wengi wabunge ambao sio CCM kama Zito kabwe, Mnyika, Mdee, Kafurila, Nasari etc. Kwa mfano huo tu unaona kuwa vijana sio tu wa CCM wanagombea uongozi ndani ya chama chao bali vijana mbalimbali wanatafuta uongozi kupitia vyama mbali mbali vilivyosajiliwa kisharia huko Tanzania.

Lakin kwa kukusaidia zaidi ni kuwa CCM siku hizi wameachana na ILE FARSAFA YA NYERERE kuwa VIJANA TAIFA LA KESHO. Kwani farsafa hiyo iliondoa sana vijana katika kugombea au haya upata uongozi mkubwa katika Chama chao.

Lakin la mwisho wachambuzi siku zote wanaanzia kwenye kichwa cha makala yako kabla kuangalia kile ulichobainisha, NAKUSHAURI BADILISHA KICHWA HICHO KISOMEKE VIJANA KUGOMBEA UONGOZI KATIKA VYAMA VYA SIASA, JE WANACHOFATA NI NINI?.

Kuhusu mitazamo yenu kuhusu mimi hilo si jambo la kushangaza kwani huko Tanganyika ile dhana ya UDINi imezidi kujikita na hata neno lenyewe UDINI linamaanisha uislam. Hivyo sitaweza hata siku moja kuikana iimani yangu na nitasema kweli daima.

Kama umechunguza maandiko yangu siku zote najibu kile ninachoulizwa na si vinginevyo. Kumbuka kuwa humu kuna mas'hala mengi, mzaha mwingi na hata kejeli nyingi. sasa kwa mtu makini anajibu kwa jinsi ulivyoulizwa mas'hala kwa mas'hala, kejeli kwa kejeli etc na kama utaona katika mada yoyote ile nimejibu mas'ala katika kitu serious naomba nijuze haraka niombe msamaha kwalo.

Huo ndio mtazamo wangu katika mada yako.

Una hoja ya msingi lakini una sahau kwamba hamasa yangu kuja na mada hii ni sio kitu kingine zaidi ya kujibu swali la wildcard kama uliamua kunisoma vizuri; Lakini wewe umeingia kwenye huu mjadala huu kama vile niliamka siku moja na kuja na wazo la kuja na mjadala kuhusu vijana na uongozi Tanzania; vinginevyo mjadala kuhusu vyama vingine na uongozi kwa vijana ni ruksa kuingia humu, ili mradi tufahamu kwamba chanzo chake ni swali muhimu la mwenzetu wildcard ambalo niliamua kulifanya kama kianzio i.e. kimbilia kimbilia ya watu wengi ccm kutafuta uongozi katika nyakazi hizi ambapo CCM inapumulia mashine; na pia majivuno ya viongozi wa CCM kwamba CCM ni chama ambacho ni kimbilio la vijana wasomi;

Hakuna aliyebisha kwamba vijana wanaenda vyama vingine, lakini wildcard hakuuliza swali hilo;
 
Uliyoyaongea yana ukweli lakini ndugu Mchambuzi bado anapoint zaidi katika hili. Kama ulivyosema wakati wa Nyerere sio wote walikuwa waadilifu by choice. Wengine walikuwa hivyo kwa kuogopa mkono wa chuma wa Mwalimu. Well kwa kuwa Mwalimu hayupo sasa haina maana watu waanze kuwa wabinafsi na wafujaji wa mali za umma au wachumia tumbo. Kwakuwa Mwalimu hayupo what we need now is a good governance system and the rule of law(invisible hand) kuendelea kuwalazimisha watu kuwa waadilifu kama wakati wa Mwalimu. That is what we need ili kuendeleza maadili serikali na katika sekta ya siasa (kama wakati wa Mwalimu)

Sawa sawa mkuu; ila changamoto kubwa tuliyonayo iwapo tutakuwa tunasubiria aje mwalimu Nyerere mwingine ni kwamba ni vigumu sana kupata mtu mwenye influence katika siasa za nchi na jamii kwa ujumla bila ya kujali itikadi ambae ataamua kwa dhati kabia not to profit from politics; Kinachotokea nyakazi hizi ni watukutafuta kukubalika na pia kuwa na ushawishi kwenye jamii ili wawe na nafasi nzuri zaidi ya kula na kula kwa muda mrefu; tuna mifano mingi ya viongozi wazee ndani ya ccm ambao walikuwa ni tumaini la kumpokea nyerere katika suala la kuwa na wazee wa kukemea na kusikilizwa, wote wamenunuliwa na wanatetea ufisadi; kama ulivyosema, uwepo wa RULE OF LAW ni muhimu sana,sio kama sasahivi ambapo kuna RULE BY LAW ambapo wenye kufaidika nayo ni wale wenye fedha au ukaribu na watawala wa nchi;

Lakini nani atasimamia hizo sheria katika nyakazi hizi ambazo tofauti na enzi za nyerere ambapo rushwa ilikuwepo maeneo mengine, leo imeingia hadi kwenye judiciary system; Mwalimu alizuia judicial corruption, ingawa kwingine alishindwa; Ni vigumu kubaini ni jinsi gani Judicial Corruption itaweza patiwa ufumbuzi; Ukienda kwenye mahakama za mwanzo kutafuta haki yako, hakimu mara nyingine hana hata kalamu, anaomba apewe na askari magereza; Ukitazama bajeti wanayopewa wizara ya sheria na katiba miaka nenda miaka rudi, utagundua jinsi gani serikali ya CCM haina nia ya kuondoa kero ya riushwa katika mfumo wetu wa mahakama; huu ndio ukweli;
 
Una hoja ya msingi lakini una sahau kwamba hamasa yangu kuja na mada hii ni sio kitu kingine zaidi ya kujibu swali la wildcard kama uliamua kunisoma vizuri; Lakini wewe umeingia kwenye huu mjadala huu kama vile niliamka siku moja na kuja na wazo la kuja na mjadala kuhusu vijana na uongozi Tanzania; vinginevyo mjadala kuhusu vyama vingine na uongozi kwa vijana ni ruksa kuingia humu, ili mradi tufahamu kwamba chanzo chake ni swali muhimu la mwenzetu wildcard ambalo niliamua kulifanya kama kianzio i.e. kimbilia kimbilia ya watu wengi ccm kutafuta uongozi katika nyakazi hizi ambapo CCM inapumulia mashine; na pia majivuno ya viongozi wa CCM kwamba CCM ni chama ambacho ni kimbilio la vijana wasomi;

Hakuna aliyebisha kwamba vijana wanaenda vyama vingine, lakini wildcard hakuuliza swali hilo;

Kama lilikuwa suala la WC basi ungemjibu hapo hapo katika bandiko hilo lakin ukiliandalia bandiko maalum lazima ubadilike kwani ulichotaka kubainisha hapo ni kitu kipana zaidi ya suala lake ni faida na manufaa kwa vijana na changamoto zao katika ajira za vyama vya siasa.

Waarabu tuna usemi mmoja. (nitauweka hapa kwa kimombo kwa faida ya wengi wasiojua kiarabu).

A right question is usually better than a right answer for a wrong question.

Ulitakiwa mkuu kumsahihisha kwanza suala lake na kumpa jibu ili litoe changamoto kwa vijana wote na faida kwa wote.

Kila la kheir. Tusonge mbele ammi.

Mgaya D.W,

Asante sana kwa mchango waku mzuri, na pia kwa kunitia moyo kwani inavyoonekana sasa ni kwamba kuna baadhi ya watu nimewashika pabaya; Na ndio maana nakubaliana na wewe moja kwa moja kwamba ‘huu ni mjadala mzuri lakini wengi hawatakubaliana na hoja zetu’; lakini hii haiwezi kutufanya turudi nyuma, tutaendelea kusema kwani nia yetu ni kujenga, sio kubomoa; Wapo watakaosema tuna wivu, lakini wanasahau kwamba pia kuna suala la malezi – mimi nimelelewa kuridhika na kwamna hakuna mtaji wa maana katika mwanadamu kama elimu, hata kama unaishi juu ya mti;

Mimi sikwenda shule kuja kuhongwa sigara, vocha, mafuta ya gari, hela ya bia, au cheo ili nijiunge na kambi Fulani kuitetea, huku huyo anaetetewa mara nyingine ni juha kabisa, hana lolote zaidi ya uwezo wake wa fedha au ukaribu na watawala; daima nimekataa kuwekeza kwa wapiti njia, bali kwa taifa langu; na kulitumikia taifa sio lazima uwe na cheo, kikitokea kwa njia ya haki sawa, kisipotokea, kuna njia nyingi sana za kujuenga taifa lako;

Kama ulivyojadili kwa ustadi mkubwa, tatizo la msingi ni kwamba nchi imeondoka kwenye RELI siku nyingi kwani hivi sasa inazagaa zagaa tu kwa mwendo wa Liwalo Liwe; Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii, tupo nje ya reli na ni kwa muda mrefu sasa; Ndio maana huwa nasema kwamba pamoja na mapungufu ya azimio la rusha, kwanini wale wanaolikebehi hawaji na kitu mbadala? Au mbadala wao ni nguvu za soko? Kama ni hii, basi wamepotoka kwani hata kwa demokrasia ambayo ni tajiri kuliko yote na mmoja wa waasisi wa soko huria na ubepari, wananchi wameamua kumchagua rais ambae ana dira ya taifa nje ya nguvu za soko – United States of Amrica na ni Obama;

Kisiasa tupo nje ya reli kwa maana ya kwamba wanasiasa wamejichukulia mamlaka yote, kwani hakuna kitu supreme Tanzania kuliko Siasa; Hata common sense ya uchumi imetupwa jalalani kwa nia ya kuachia siasa itawale; Na mbaya zaidi, katika siasa, suala la maadili halipo tena; Kiongozi anaheshimika na kupandishwa cheo au kupewa cheo akiwa na sifa hizi: irrational, arrogant, ignorant (hata kwa makusudi), stubborn, & dishonest;

Kijamii tupo nje ya reli kwa maana kwamba – pia hakuna maadili, sifa ya kiongozi ni pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa fedha wa kulala na wanawake wengi, kuwa na uwezo wa kugharamia starehe kubwa kubwa, uwezo wa kununuwa wapiga kura, n.k; Ndio maana viongozi wengi ni wahuni wahuni tu; Kama kuna hoja kwamba uhuni ni jadi ya mtanzania, angalau basi isiwe hadharani; Ni muhimu kwa viongozi kutenganisha maisha binafsi na maisha ya umma kwani wao sio waajiriwa wa Vodacom au Tigo bali watanzania;

Kiuchumi tupo nje ya reli kwa maana kwamba tofauti na miaka ya ujamaa, pamoja na mapungufu yake, uchumi ulilenga kuhudumia wananchi; leo hii uchumi unahudumia wawekezaji na wanasiasa wenye hisa au wenye kuwekewa asante kwenye mabenki ya uswsisi; Na ni hao hao wanapita pita majimboni au kwenye majukwaa eti wajibuni wapinzani kwamba tunatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM; Hivi kweli kama wanasiasa hawa wangekuwa wanaishi kwa huduma za miradi ya ilani ya uchaguzi wangekuwa na hali walizokuwa nazo leo? Za kutegemea maji, zahanati, elimu n.k zinazotolewa kupitia miradi hii?

Ilani ya uchaguzi haina maana zaidi ya kurudishia wananchi chao, tena in deficit kwani sana sana huduma hizi zinawasaidia tu waone siku inayofuata, sio wapae katika maisha yao; kwa maana nyingine – watanzania wanahitaji miradi endelevu na yenye kuwajengea capabilities to prosper into the future, sio miradi ya ilani ya uchaguzi just to see the sun the next morning wakiwa bado in the same state of despair and hopelessness; Inashangaza watawala wetu hawajiulizi kwanini wananchi wanazidi kuichoka CCM licha ya hizo ilani za uchaguzi kujenga hayo sijui mabarabara n.k;

Nikiwa bado kwenye suala la uchumi, uendeshaji wa uchumi ambapo siasa ndio imewekwa mbele, haitoa mfano mzuri kwa watoto na vijana wetu kwani na wao wanapata ndoto za kujaribu kuingia kwenye siasa siku moja na kuweka uchumi mikononi mwao badala ya kwa wataalam na vyombo husika; ndio maana ukiwa mitaani kusikiliza opinion za wananchi kuhusu mabadiliko ya mawaziri kwa mfano yakitokea, its common practice kusikia “AYAA WEEEE, Fulani kapelekwa Wizara ya Vijana? Ningekuwa mimi ningejiuzulu”, Na wanaanza kulaumu mamlaka ya uteuzi kwamba itakuwa huyo mteule pengine hawamtaki na wanamwondoa pole pole; Maana yao hapa ni kwamba uteuzi nyadhifa ya uwaziri n.k ni kwenda kula nchi, sio kutumikia nchi;

Umejadili suala la tatizo la ajira na jinsi gani linachangia vijana wengi kukimbilia kwenye siasa kupata angalau chochote; naelewa hoja yako ya msingi, lakini hii bado haibadilishi ukweli kwamba – malengo ya kuweka ajira sekta ya umma na ajira sekta binafsi hayafanani; Ni kweli kwamba mtu anatafuta ajira kutafuta returns to his or her education, kuhudumia familia yake n.k, lakini iwapo ajira hizi zingekuwa zinapatikana katika mazingira transparent, yenye kuweka maslahi ya taifa mbele, na kupitia recruitment badala ya succession, tungepata vijana wengi ambao wanatamani ajira za umma kama njia ya kutumia vipaji vyao na kujipatia riziki,lakini muhimu zaidi kuja kustaafu na sifa kubwa kuhusu mchango wao katika kujenga taifa;

Kwa sasa, vijana wapo busy zaidi searching for CONNECTIONS with the system kuliko SEARCHING FOR TALENT, na ndio maana ni humo humo tunapata viongozi vihiyo;
 
Kama lilikuwa suala la WC basi ungemjibu hapo hapo katika bandiko hilo lakin ukiliandalia bandiko maalum lazima ubadilike kwani ulichotaka kubainisha hapo ni kitu kipana zaidi ya suala lake ni faida na manufaa kwa vijana na changamoto zao katika ajira za vyama vya siasa.

Waarabu tuna usemi mmoja. (nitauweka hapa kwa kimombo kwa faida ya wengi wasiojua kiarabu).

A right question is usually better than a right answer for a wrong question.

Ulitakiwa mkuu kumsahihisha kwanza suala lake na kumpa jibu ili litoe changamoto kwa vijana wote na faida kwa wote.

Kila la kheir. Tusonge mbele ammi.

Nitaanzisha mjadala mwingine ambao utatokana na mawazo kutoka mjadala huu kwani ni muhimu sana tuanze na kuangalia CCM kwanza kwani hiki ndio chama chenye dhamana ya kuongoza nchi; hao vijana wa chadema, TLP n.k bado hawajapewa dhamana ya kuongozi nchi; Vijana wa CCM wanajadiliwa kwa sasa kwa vile chama chao ndio kinaunda serikali na kina mamlaka ya teuzi mbalimbali za kuhudumia umma; Jaribu kuangalia mjadala huu kwa mtazamo huo, sio tu kwa mtazamo wa vijana kuwa makatibu wa CCM mkoa n.k;
 
Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe.

Ahsantum
 
Kwanza kabisa ni KICHWA CHA HABARI CHAKO kinachobainisha kuwa Vijana kugombea uongozi CCM. Kwa mtu yoyote makini anakuona wewe ni mshabiki wa chama tofauti na CCM. Kwani siku hizi vijana wengi sana huko Tanzania wametokea kukimbilia kwenye Siasa mfano ulio hai ni kama Vijana wengi wabunge ambao sio CCM kama Zito kabwe, Mnyika, Mdee, Kafurila, Nasari etc. Kwa mfano huo tu unaona kuwa vijana sio tu wa CCM wanagombea uongozi ndani ya chama chao bali vijana mbalimbali wanatafuta uongozi kupitia vyama mbali mbali vilivyosajiliwa kisharia huko Tanzania.

Lakin kwa kukusaidia zaidi ni kuwa CCM siku hizi wameachana na ILE FARSAFA YA NYERERE kuwa VIJANA TAIFA LA KESHO. Kwani farsafa hiyo iliondoa sana vijana katika kugombea au haya upata uongozi mkubwa katika Chama chao.

Lakin la mwisho wachambuzi siku zote wanaanzia kwenye kichwa cha makala yako kabla kuangalia kile ulichobainisha, NAKUSHAURI BADILISHA KICHWA HICHO KISOMEKE VIJANA KUGOMBEA UONGOZI KATIKA VYAMA VYA SIASA, JE WANACHOFATA NI NINI?.

Kuhusu mitazamo yenu kuhusu mimi hilo si jambo la kushangaza kwani huko Tanganyika ile dhana ya UDINi imezidi kujikita na hata neno lenyewe UDINI linamaanisha uislam. Hivyo sitaweza hata siku moja kuikana iimani yangu na nitasema kweli daima.

Kama umechunguza maandiko yangu siku zote najibu kile ninachoulizwa na si vinginevyo. Kumbuka kuwa humu kuna mas'hala mengi, mzaha mwingi na hata kejeli nyingi. sasa kwa mtu makini anajibu kwa jinsi ulivyoulizwa mas'hala kwa mas'hala, kejeli kwa kejeli etc na kama utaona katika mada yoyote ile nimejibu mas'ala katika kitu serious naomba nijuze haraka niombe msamaha kwalo.

Huo ndio mtazamo wangu katika mada yako.

Mkuu Barubaru umeweka pointi moja nzuri sana ambayo inatupa mwanga mwingine. Unajua wazee wetu pia wengi wameacha taaluma zao ambazo naweza kusema ni za maana, au kama ingekuwa nchi nyingine nigesema za maana sana. Madaktari, wahandisi, wanajeshi, walimu, wafanyabiashara wote wanakimbilia kuogombea ubunge, vijana pia ni sehemu ya watanzania.

Kama serikali imezitoa maana taaluma zote na siasa imebaki kuwa taaluama pekee ya maana, hakuna vibaya kwa vijana kuingia kwenye siasa.
 
Bongolander,

Nashukuru sana kwa mchango wako kwenye bandiko namba kumi na nane; Hoja yako kuhusu harakati za uhuru na madaraka na mamlaka ya nchi ni ya msingi sana; Ndio maana Mwalimu katika TANU na RAIA (1962) anasema hivi kwa vijana wenzake wa wakati huo:

[…kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana na ufahari wa wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu, vilivyokuwa vimeshikiliwa na wazungu hapo zamani, tulitaka na mishahara pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo, bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, bila kujali maisha ya watu wetu…”]

Umetoa mfano wa waziri kijana ambae sijui ni yupi haswa lakini kichwani nafikiria at least watano katika kipindi cha 2005 – 2012; Lakini hoja yako ni ya msingi sana kwani katika hoja yangu ya msingi pia nilijadili kwamba vijana wengi (sio wote) hufuata scarce goods ambazo sasa inaaminika kwamba zinapatikana kwa urahisi zaidi kupitia Politics, na bidhaa hizi ni Prestige, Wealth and Social Status; Na inakuwa vigumu sana kwa vijana wengi (sio wote) kutofautisha utumishi wa umma na kutumikia maisha binafsi (familia n.k),

Mtu haukatazwi kutumia kipato chako kuendeleza familia yako na ndugu zako kwani that’s part of private returns to education, kinacho tatiza jamii ni pale masuala ya wealth accumulation, prestige and social status yanapokuwa ndio primary motivation ya kutafuta uongozi wa kisiasa; Na kinacho tatiza zaidi pale Vijana wasomi na wenye upeo na elimu yao nzuri kabisa wanapoamua kuwa mamluki wa siasa; Ukitazama vijana wengi, hawapo pamoja kujiweka sawa na kupanga mikakati jinsi gani ya kuikomboa nchi yetu kupitia, elimu zao, exposure yao, nyadhifa zao au ushawishi wao katika jamii, badala yake kutwa wao ni kukaa baa baada ya kazi kujisifia jinsi gani kambi yao ni bora katika kumpigia debe kiongozi fulani kuliko kambi nyingine;

Utamaduni huu umepokewa na vijana na utaendelea kurithishwa vizazi hadi vizazi na ndio maana binafsi sioni jinsi gani siasa za makundi, fitina na visasi zitakwisha ndani ya CCM;
 
Kama lilikuwa suala la WC basi ungemjibu hapo hapo katika bandiko hilo lakin ukiliandalia bandiko maalum lazima ubadilike kwani ulichotaka kubainisha hapo ni kitu kipana zaidi ya suala lake ni faida na manufaa kwa vijana na changamoto zao katika ajira za vyama vya siasa.

Waarabu tuna usemi mmoja. (nitauweka hapa kwa kimombo kwa faida ya wengi wasiojua kiarabu).

A right question is usually better than a right answer for a wrong question.

Ulitakiwa mkuu kumsahihisha kwanza suala lake na kumpa jibu ili litoe changamoto kwa vijana wote na faida kwa wote.

Kila la kheir. Tusonge mbele ammi.

Mwarabu na Siasa za Tanzania wapi na wapi bana. We Tipu tipu vipi bana.
 
Nakubaliana na wewe kwa yote uliyoyasema kwa kuongeza point zaidi,

Nafikiri baada ya kuingia kwenye huu mfumo mpya wa uchumi, Nchi ilitakiwa iwe na kiongozi mwenye msimamo mkali na mzalendo wa kweli katika utendaji na utekelezaji wa majukumu ya nchi kwa sababu nchi ilikuwa haijawa na sheria madhubuti za kukabiliana na soko huria. Matokeo yake, nchi iliingiliwa na crooks investor, corrupt government executive and transgressor politician. Matokeo yake, tunaona matabaka makubwa kati ya wenye nacho wachache na masikini wengi yameibuka kwa kasi.

Nchi iko mahali ambapo kwa sasa kikundi cha watu wachache wana influence government policy in our economy na kama watahisi kuna uwezekano wa oposition to take over, watahakikisha wanafanya kila linalowezekana kujipenyeza ili waendelee kuvuna zaidi kwa sababu wanasiasa wetu wengi walishakuwa wabinafsi wa kupindukia.

Angalia Mexico na tatizo la drug cartel. Those guys now are bigger than the Government kwa sababu waliachiwa na corrupt official wakajijenga.

Would it be correct kusema CCM sasa imegeuka kuwa a cartel political party and no longer a mass - based political party?
 
Would it be correct kusema CCM sasa imegeuka kuwa a cartel political party and no longer a mass - based political party?

CCM haijafikia hicho kiwango lakini pale chama kinapofungua milango ya rushwa kuwa ndiyo njia na kigezo cha utendaji wa shughuli zake, kiko njiani kuelekea huko. kibaya zaidi ni pale unapokuta viongozi wa chama na serikali ni walewale, kitu ambacho inakuwa hakuna hata kivuli au kioo cha viongozi wa serikali kujiangalia au kuangaliwa.

Pamoja na kwamba mimi siyo muumini sana wa siasa zilizokuwa za waasisi wa nchi yetu, lakini misingi waliyoijenga katika chama hicho ndiyo hiyo ambayo imejitahidi kukishikilia chama mpaka sasa kutofikia kiwango cha kuwa cartel political party, lakini kama chama kitaendelea kuimba tu nyimbo za kuwafariji wananchi (kujivua Gamba, uzalendo kwanza n.k) bila chenyewe kubadilika na ku walk the talk, siyo muda mrefu kitafikia kiwango hicho.

I just wish, nchi kuwa na chama au vyama vya upinzani madhubuti vyenye ku walk the talk ambavyo vinaweza ku set ajenda ambazo really matter to wananchi badala ya kuwa carbon copy ya CCM huku vikicheza ngoma ile ile ambayo CCM anaicheza.

Mchambuzi, samahani kwenda nje ya mada. Hivi ulishaona wapi katika nchi yenye viongozi wa kisiasa ambao wako serious wanabishana kuhusu kadi ya chama kwa wiki moja? ( umerudisha, sijarudisha, mwanachama, siyo mwanachama), really?

Hii tu utaipata Tanzania.
 
CCM haijafikia hicho kiwango lakini pale chama kinapofungua milango ya rushwa kuwa ndiyo njia na kigezo cha utendaji wa shughuli zake, kiko njiani kuelekea huko. kibaya zaidi ni pale unapokuta viongozi wa chama na serikali ni walewale, kitu ambacho inakuwa hakuna hata kivuli au kioo cha viongozi wa serikali kujiangalia au kuangaliwa.Pamoja na kwamba mimi siyo muumini sana wa siasa zilizokuwa za waasisi wa nchi yetu, lakini misingi waliyoijenga katika chama hicho ndiyo hiyo ambayo imejitahidi kukishikilia chama mpaka sasa kutofikia kiwango cha kuwa cartel political party, lakini kama chama kitaendelea kuimba tu nyimbo za kuwafariji wananchi (kujivua Gamba, uzalendo kwanza n.k) bila chenyewe kubadilika na ku walk the talk, siyo muda mrefu kitafikia kiwango hicho.

I just wish, nchi kuwa na chama au vyama vya upinzani madhubuti vyenye ku walk the talk ambavyo vinaweza ku set ajenda ambazo really matter to wananchi badala ya kuwa carbon copy ya CCM huku vikicheza ngoma ile ile ambayo CCM anaicheza.

Mchambuzi, samahani kwenda nje ya mada. Hivi ulishaona wapi katika nchi yenye viongozi wa kisiasa ambao wako serious wanabishana kuhusu kadi ya chama kwa wiki moja? ( umerudisha, sijarudisha, mwanachama, siyo mwanachama), really? Hii tu utaipata Tanzania.

Mkuu Ng'wamapalala,

Nakubaliana na hoja yako kimsingi, kwamba ingawa CCM bado sio cartel party lakini hakipo mbali; Ila ni muhimu pia nikasema kwamba, mwelekeo wa sasa upo zaidi kwenda kuwa a cartel party kuliko kurudi kuwa chama cha wananchi; Nitajaribu kufafanua:

Kuingia kwa uliberali (hasa kiuchumi) nchini pamoja na mageuzi ya kisiasa (vyama vingi) kumeipa CCM ya Mwalimu Dhoruba kali sana;Kubwa kuliko yote ni kifo cha STATE-PARTY, suala ambalo limepelekea vyanzo vikuu vya fedha kwa Chama kukauka, kwani miaka ya zamani, CCM ilikuwa inachota tu pesa BOT, Hazina, bila maelezo; Kwa sasa, haiwezi kufanya hayo tena na wala haiwezi kuzungusha bakuli kwenye parastatals za umma. Natamani utafiti ufanyike juu ya jinsi gani utamaduni huu ulichangia kuporomoka kwa uchumi, lakini hasa kumbebesha mlipa kodi deni la taifa ambalo wajukuu na vitukuu wao watarithi na kuachia tena wajukuu na vitukuu wao;

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi, CCM imelazimika kutafuta vyanzo vipya vya fedha, na ndio maana mwaka 1992, ilikuwa ni muhimu kwa CCM kuua azimio la arusha ili kukaribisha wenye pesa kukamata chama na kukiendeleza, whether ni kwa fedha zao halali au wizi serikalini na ufisadi, ili mradi mambo yaendee; kwahiyo CCM's de-ujamaaisation ya itikadi ya Ujamaa ilifungua milango kwa tyconization of CCM, na jinsi muda unavyozidi kwenda, taratibu Chama cha wakulima na wanfanyakazi kinageuka kuwa a Cartel Party, na binafsi sioni jinsi gani kitarudi kuwa cha wakulima na wafanyakazi, bali mwendo ni kwenda mbele kuwa a Cartel Party; Hizi elements tunaziona nyingi tu, na mifano yake ndio kama hiyo unayoitoa kwamba viongozi wamethibitika mafisadi, lakini chama kinawalinda;

Tujadili ukweli: Tofauti na miaka ya nyuma, wanasiasa wa leo (CCM) hawaoni aibu tena to wine and dine with tycoons, matapeli and the like kwani katika chaguzi za nyakati hizi, hawa ndio wakuwa sponsor; Wakati wa chama kimoja, hatukuwa tunasikia suala la financing of election campaigns na matukio ya rushwa kwa sababu ilikuwa ni jukumu la serikali na state parastatals to fund illicitly some of their favourite candidates; Leo hii, sources of funds have dried up, elections have become so expensive and its only the tycoons who can sponsor or run for office;Kwahiyo, nadhani nitakuwa sahihi nikisema kwamba CCM has transformed from being a mass - based political party, into a party of tycoons, and its heading towards becoming a Cartel Party, before it eventually collapses, and may be reborn again or be buried for good in the political graveyard of the country;

Mwisho naomba niseme kwamba vyama vya upinzani, media na intellectual commentators wamekuwa wanapiga sana kelele kwamba CCM kimeacha misingi yake ya chama cha wakulima na wafanyakazi na kuwa chama cha mafisadi n.k; Kwa kweli, what matters to the opposition and commentators (sio wote lakini wengi), is not the tyconisation of CCM bali wivu na tamaa ya kuwa katika nafasi ya CCM ya ku vandalize the state for private gain; How much they wish they were recipients of millions of dollars in Swiss accounts instead of CCM; After all, they too have ambitions to go to the state house, and start shifting resources of the state to their indigenous communities, as well as build palaces; Huu ndio ukweli;
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom