Vijana kugombea Uongozi CCM: Je, Wachofuata ni nini?

Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Mada yangu inatokana na Swali nililoulizwa na Mwana JF mwenzetu ‘WildCard’ katika moja ya mijadala yetu humu ndani; WildCard aliniuliza hivi:

Nikuulize jambo moja Mchambuzi: Kwa nini bado watu na akili zao timamu kabisa wanabanana kugombea nafasi za UONGOZI ndani ya CCM inayokufa kwa kasi hivi? Au hili linafanana na masuala ya ngono na ukimwi (nisamehe kwa lugha hii ya kuudhi)?

Hili ni swali la msingi sana, hasa kwa Vijana wenye shauku to ‘pursue career’ zao kwenye Siasa – aidha kupitia CCM, Chadema au Vyama vingine; Ndio maana badala ya kumjibu WildCard kwa ufupi, nikaonelea nilipe uzito wake wa kipekee kwa kufungulia uzi wa mjadala;

Tumeshuhudia vijana wakimiminika kwa wingi kukimbilia kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa ndani wa Chama uliomalizika hivi karibuni; Kutokana na wingi huu wa vijana, CCM imekuwa ikijisifia sana kwamba ni chama chenye mvuto kwa Vijana, tena Wasomi; Je kuna ukweli gani katika hili?

Kabla sijaenda mbali na mjadala wangu, ningependa kwanza kuijadili kidogo MEDIA yetu Tanzania; Binafsi naamini kwamba MEDIA ni moja ya mihimili mikuu ya Dola (at least informally), pamoja na Bunge, Mahakama na Executive; Kutokana na uzito wake katika taifa, sekta ya MEDIA inatakiwa wakati wote isimamie ukweli, haki, uadilifu, na iwe ni mfano wa kuigwa katika jamii; Tofauti na haya, kwa kiasi fulani, kinachoendelea nchini ni Utamaduni wa baadi ya vyombo vya habari kufanyia mzaa mzaa suala la uongozi wa UMMA, hasa pale Magazeti Makubwa na Yenye Heshima na pia ushawishi katika Jamii yanapokuja na Vichwa Vya Habari kama vile: “FULANI NA FULANI WAULA.”; Ukisoma kwa undani unakuta ni habari za watu fulani fulani kuteuliwa kushika nafasi za UMMA;

Nabakia kujiuliza, Tangia lini Kupewa Uongozi wa Umma imekuwa ni Kuula? Hii inatuma ujumbe gani kwa watoto wetu wenye ndoto za ku-pursue careers in politics huko mbeleni? Jibu ni rahisi tu – Uongozi wa Umma Ni kwenda Kula! Ni kwa mtindo huu, ajira ya umma sasa inakuwa treated kama vile ni Ajira Vodacom, Barclays, Tigo n.k; Nakumbuka nikiwa mtoto, ajira za Umma zilikuwa zinapokewa na wahusika kwa woga na wasiwasi mkubwa kwani walikuwa wanafahamu kwamba kilichotokea ni Rais au Mwenyekiti (Nyerere) kuwapa dhamana, sio fadhila; Isitoshe, teuzi zote zilikuwa zinafanywa siri kubwa, na ilikuwa ni kawaida kusikia umeteuliwa au umefukuzwa kazi aidha kwa kupitia Redioi au barua rasmi; Tofauti na miaka ile, miaka ya sasa mtu kuwa waziri, mjumbe wa kamati kuu CCM, mbunge (hata wa jimbo), balozi, unaambiwa mapema kabisa hata ukiwa kwenye baa;

Nikirudi kwenye yangu ya msingi inayotokana na Swali la Wildcat hapo juu, napenda kuijadili kama ifuatavyo:

Haya ni matokeo ya PERSONAL INVESTMENTS in Reciprocal Relations ambazo wengi ya Watu, hasa Vijana uwekeza kwa Viongozi wa CCM na Serikali yake, kama njia ya kufanikisha malengo BINAFSI - yani ya vijana hawa, malengo ambayo ni dhahiri hayawezi kufanikiwa nje ya CCM; Tutayaona malengo hayo punde; Hii ni tofauti na mtazamo wa kufanikisha malengo ya UMMA ambayo ni dhahiri yanaweza kufanikiwa kupitia Chama chochote Cha siasa, sio CCM Peke yake

Kwa vijana wengi, the sought goods (bidhaa wanazotafuta) hazina uhusiano na PUBLIC GAIN (wananchi), na badala yake uegemea zaidi on PRIVATE GAIN (matumbo yao na familia zao); Bidhaa hizi ‘ADIMU’ ambazo hutafutwa na Vijana Wengi wanaokimbilia uongozi CCM ni pamoja na Prestige, Social Status & Wealth, ambazo nadhani tunakubaliana kwamba:

They have ‘Scarcity Value’ - kwa maana ya kwamba – they may be available, but they may not be accessible to many; Kutokana na sifa hii, ndio maana Vijana wengi hutumia kila njia to invest in relations na CCM, Viongozi Wa Chama Ngazi Wa Mbalimbali, na Viongozi wa Serikali ya CCM kwa ujumla wake, kama njia rahisi ya kupata Bidhaa hizi adimu;

Enzi za Mwalimu, CCM ilikuwa ina hazina kubwa sana ya Viongozi Bora kutokana na matumizi ya utaratibu wa Leadership Recruitment ambao ulikuwa unazingatia sifa za mhusika kama vile Elimu, Uzeofu, Ufahamu wa Chama, Uzalendo Kwa Taifa, Rekodi Safi katika jamii, Uadilifu, n.k; Miaka ya sasa, CCM imejaa Bora Viongozi (badala ya Viongozi Bora), kwani Chama kimeachana na Leadership Recruitment na kudandia mfumo wa Leadership Succession ambapo sifa kuu zimegeuka kuwa ni uwezo wa fedha, ukaribu wako au wa wazazi wako na viongozi wakuu wa Chama na Serikali ya CCM, Ukabila, na Udini (both ukristo na uislamu);

Mbali ya haya, tofauti na wakati wa Nyerere ambapo mtu alikuwa anapandishwa cheo kutokana na performance, integrity na patriotism, na mengineyo yenye maslahi kwa taifa, inaelekea kwamba nyakazi hizi vigezo vikuu ni pamoja na mtu kuwa ignorant (hata kwa makusudi), irrational, dishonest and stubborn (hasa in relation to wapinzani); Kutokana na hili, CCM ni nadra sana kutumia siasa za akili, kwani intellectuals hawapewi nafasi na badala yake, wenye kutamba ndani ya chama ni ideologues, demagogues and jesters; Na ni bahati mbaya sana kwamba hata intellectuals wanaofanikiwa kupenya ndani ya chama, most of them end up being ideologues, demagogues and jesters;

Kwa kumalizia, pengine ni muhimu nikajadili na kutofautisha Leadership Succession na Leadership Recruitment, japo kwa ujumla wake;

Leadership Succession
Succession ni mchakato unaohusisha transfer ya uongozi kutokea kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kundi moja kwenda kwa kundi lingine; Mafanikio ya mfumo huu hutegemea sana sheria zilizopo (relevant laws), historia ya jamii husika, na utamaduni wa jamii husika; Pale ambapo sheria na utamaduni unakuwa observed, leadership succession inaweza kuwa effective & peaceful; Lakini kwa ujumla wake, leadership succession katika nchi zetu Afrika kwa kiasi kikubwa imekuwa ni zao la ‘crude political manipulations’, maasi au mapinduzi ya kijeshi, kuliko ‘a peaceful application’ of the constitutional process. Tatizo hili linachangiwa sana na the fact kwamba - Constitutionalism is not well founded in Sub Saharan Africa (hata Tanzania), na pia linachangiwa na tabia/utamaduni wa kufanya Politics iwe ni ‘Supreme’ Kwa masuala mengine yote ndani ya taifa;

Leadership Recruitment:
Huu ni mchakato ambao hufuata utaratibu wa - identification, nurturing, education and training of youths ili waje kuwa hazina ya uongozi siku za usoni; Na ili mfumo huu ufanye kazi, ni lazima kuwepo na an enabling environment & supporting institutions na kwa utaratibu unao ongozwa na kanuni, sheria, & codes of conduct, whereby potential leaders (hasa vijana) wanaweza kuwa identified, attracted, nurtured and trained. Uwepo wa mfumo wa namna hii unasaidia sana kuvutia independent individuals wenye talent, elimu, upeo, Uzalendo, mwono (vision), mawazo na ambition to pursue political career kwa manufaa ya taifa lao;

Muhimu:

1. Kwa mazingira ya Sasa, sio lazima Vijana wa namna hii wapatikane kupitia UVCCM peke yake, bali wanaweza kuwa ni wananchi wa kawaida wasio na chama chochote, lakini they are motivated to play an active role in public affairs, kwa manufaa ya taifa lao la Tanzania;

2. Ingawa tatizo hili la Leadership Succession lipo practiced sana katika CCM ya nyakazi hizi, Jinamizi hili pia limeshaingia Chadema, na ni muhimu kwa Chadema kulifukuza Jinamizi hili kama kweli nia ya Chama hiki ni kuaminiwa na UMMA kuipokea Madaraka CCM aidha 2015 au Baadae;
 
M

Mat.E

Member
Joined
Dec 28, 2010
Messages
66
Points
0
M

Mat.E

Member
Joined Dec 28, 2010
66 0
Ni dhahiri kabisa kinachofuatwa na kutafutwa kwa gharama zozote hata kufanya umafia na vijana hao ni ULAJI, wala si kukitumikia chama na watanzania! Ndiyo maana Wanapofanikiwa kupata hayo madaraka hufanya sherehe za KUFURU kwa kuwa WAMEULA!!
 
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
26,577
Points
2,000
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
26,577 2,000
Wapo vijana wachache wanaosimama CCM kwa mapenzi ya ndani, na wanapinga waziwazi kinachoendelea kule site,ni kama 1% ya vijana wa CCM,
  • 97% wakiongozwa na Nape ft Mwigulu wanajua wanachokitafuta kule, CCJ angevikosa, CDM angevikosa
  • 2% hawajielewi, wapo tu kama mapoyoyo, hawana sababu za msingi, hisia hawana na system imewatenga
 
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
834
Points
1,000
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
834 1,000
Kadiri siku zinavyozidi kwenda tunaona jinsi ambavyo CCM, kupitia mwenendo wake, inajitambulisha kama njia ya kutajirikia kirahisi, jambo ambalo linaonekana kuwa na mvuto sana kwa vijana wengi.

Media si chanzo. Media imedakia hili kutokana na CCM yenyewe inavyojiwasilisha mbele ya jamii. Si maadili kwa vyombo vya habari kuuza habari kwa namna inayochochea ufisadi; lakini ni CCM ndiyo inayohusika zaidi na hii promotion ya ufisadi.

Sipati picha Tanzania itakuwa ni jamii ya namna gani miaka kumi ijayo CCM ikiendelea kuwa madarakani kwa mwenendo huu!
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 0
Asilimia kubwa ya vijana wanatafuta opportunity, wanatafuta maslahi binafsi, wanatafuta jinsi ya kujitajirisha kwa haraka. Kuna njia nyingine lakini hii ni rahisi na ya uhakika. Wanaona wenzao waliofuata njia hii muda mfupi wakiwa juu kiuchumi! Kwa maoni yangu hawa ni zaidi ya asilimia 98.

Labda asilimia kama moja wanafuata ushawishi wa familia.

Nadhani ni chini ya asimia 0.5 wanaingia kwa nia ya kusaidia jamii. Na wakifanya hivyo ni ili wachaguliwe tena!

Jiulize utatoaje rushwa ili uchaguliwe kusaidia jamii? Anayetoa rushwa ni kwa manufaa yake
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Points
1,195
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 1,195
Kuna kijana mmoja ameingia 2011 ndani ya ccm akabahatika kuwa rafiki wa mtoto wa kigogo mkuu wa nchi leo hii ni katibu wa wilaya wa vijana wa ccm na tayari ni tajiri tu kwa mali ukiuliza kapata wapi jibu unakosa kwani anasafiri safiri kidogo kwenda nje!!
 
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
216
Points
170
Age
63
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
216 170
Kwani huko kwingine wanafuata nini pale wanapogombea? Hakika hili siyo swali kwa sababu kinachogombewa ni cheo au wadhifa hata huko kwingine na kwenyewe wanagombea vitu hivyo hivyo sasa chanzo cha swali kama hili unatokea wapi?
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Kwani huko kwingine wanafuata nini pale wanapogombea? Hakika hili siyo swali kwa sababu kinachogombewa ni cheo au wadhifa hata huko kwingine na kwenyewe wanagombea vitu hivyo hivyo sasa chanzo cha swali kama hili unatokea wapi?
Kwanini usichangie kwa kujibu swali au kujadili hoja hata kama una mawazo tofauti na badala yake unauliza swali la ajabu ajabu tu, wewe ndiye huyu katibu wa wilaya nini anayemzungumzia bangoo? Vinginevyo huko kwingine, kule kwingine, nimejadili hilo kwenye hoja yangu ya msingi; Huu mjadala ni straight forward;
 
SHIEKA

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Messages
8,276
Points
2,000
SHIEKA

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2011
8,276 2,000
Asante Mchambuzi, nimeipenda sana analysis yako ya Leadership succession na Leadership recruitment. Ni kweli kabisa ccm ni kinara wa Leadership succession wanaopewa uongozi ni vijana au watu wanaofahamika kwa viongozi wakuu. Halafu pia kuna hii dhana ya ' kuula'. Dhana hii imechangia kuua nchi yetu kimaendeleo. Mtu akichaguliwa kuongoza shirika au taasisi ya serikali anashangiliwa na jamaa zake na kuambiwa waziwazi kuwa 'sasa shida zako zote zimeisha' Matokeo yake atajilimbikizia mali na kuwa fisadi hatari. Hii ndo iliyouwa mashirika yetu mengi na mpaka sasa wizara na idara nyingi za serikali zinachechemea kwa kuumizwa na viongozi fisadi wapenda mali.Vijana wetu wakiona hivyo ni lazima watafute njia za kupenya kufika huko kwenye kuendesha Hammer na Vx8. Njia mojawapo ni kukimbilia chama ambacho kinatoa hizo fursa bila masharti magumu wala kufuatilia mienendo na maadili ya viongozi. Na kwa bahati mbaya sana chama hicho ni ccm.
Kwa hiyo naklubaliana nawer Mchambuzi kwa nini vijana wanakimbilia chaguzi za chama hicho.
 
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
216
Points
170
Age
63
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
216 170
Kwanini usichangie kwa kujibu swali au kujadili hoja hata kama una mawazo tofauti na badala yake unauliza swali la ajabu ajabu tu, wewe ndiye huyu katibu wa wilaya nini anayemzungumzia bangoo? Vinginevyo huko kwingine, kule kwingine, nimejadili hilo kwenye hoja yangu ya msingi; Huu mjadala ni straight forward;
Inawezekana swali lako lina unazi wa upande fulani inawezekana CDM kwanini hujahoji wale wanaogombea CDM au CUF wanatafuta nini hadi wewe ufikie hatua ya kuwauliza vijana wanaogombea CCM.Na wewe lazima ujiongeze na siyo kuuliza maswali ya kitoto wewe unajua kabisa pale CCM wanagombea vyeo kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Chama Chao,sasa wewe unakuja na swali la ajabu eti wanatafuta nini!!Na huu si mjadala bali umesukumwa na UNAZI wako.
 
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
216
Points
170
Age
63
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
216 170
Kwanini usichangie kwa kujibu swali au kujadili hoja hata kama una mawazo tofauti na badala yake unauliza swali la ajabu ajabu tu, wewe ndiye huyu katibu wa wilaya nini anayemzungumzia bangoo? Vinginevyo huko kwingine, kule kwingine, nimejadili hilo kwenye hoja yangu ya msingi; Huu mjadala ni straight forward;
Inawezekana swali lako lina unazi wa upande fulani inawezekana CDM kwanini hujahoji wale wanaogombea CDM au CUF wanatafuta nini hadi wewe ufikie hatua ya kuwauliza vijana wanaogombea CCM.Na wewe lazima ujiongeze na siyo kuuliza maswali ya kitoto wewe unajua kabisa pale CCM wanagombea vyeo kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Chama Chao na maendeleo ya nchi,sasa wewe unakuja na swali la ajabu eti wanatafuta nini!!Na huu si mjadala bali umesukumwa na UNAZI wako kwani wale ambao wapo kwenye vyama vya CDM.CUF mbona wapo wenye maisha tofauti baada ya kuingia kwenye nyadhifa mbalimbali ndani ya vyama vyao?We unafikiria kwamba Mwenyekiti wa BAVICHA anaishi maisha kama ya zamani? acheni kudanganyana hapa hakuna mtu anayependa kuishi maisha magumu,hakuna kijana asiyependa kujulikana bana aaah!!
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Inawezekana swali lako lina unazi wa upande fulani inawezekana CDM kwanini hujahoji wale wanaogombea CDM au CUF wanatafuta nini hadi wewe ufikie hatua ya kuwauliza vijana wanaogombea CCM.Na wewe lazima ujiongeze na siyo kuuliza maswali ya kitoto wewe unajua kabisa pale CCM wanagombea vyeo kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya Chama Chao na maendeleo ya nchi,sasa wewe unakuja na swali la ajabu eti wanatafuta nini!!Na huu si mjadala bali umesukumwa na UNAZI wako kwani wale ambao wapo kwenye vyama vya CDM.CUF mbona wapo wenye maisha tofauti baada ya kuingia kwenye nyadhifa mbalimbali ndani ya vyama vyao?We unafikiria kwamba Mwenyekiti wa BAVICHA anaishi maisha kama ya zamani? acheni kudanganyana hapa hakuna mtu anayependa kuishi maisha magumu,hakuna kijana asiyependa kujulikana bana aaah!!
Sawa mkuu, CCM OYEE!
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Asante Mchambuzi, nimeipenda sana analysis yako ya Leadership succession na Leadership recruitment. Ni kweli kabisa ccm ni kinara wa Leadership succession wanaopewa uongozi ni vijana au watu wanaofahamika kwa viongozi wakuu. Halafu pia kuna hii dhana ya ' kuula'. Dhana hii imechangia kuua nchi yetu kimaendeleo. Mtu akichaguliwa kuongoza shirika au taasisi ya serikali anashangiliwa na jamaa zake na kuambiwa waziwazi kuwa 'sasa shida zako zote zimeisha' Matokeo yake atajilimbikizia mali na kuwa fisadi hatari. Hii ndo iliyouwa mashirika yetu mengi na mpaka sasa wizara na idara nyingi za serikali zinachechemea kwa kuumizwa na viongozi fisadi wapenda mali.Vijana wetu wakiona hivyo ni lazima watafute njia za kupenya kufika huko kwenye kuendesha Hammer na Vx8. Njia mojawapo ni kukimbilia chama ambacho kinatoa hizo fursa bila masharti magumu wala kufuatilia mienendo na maadili ya viongozi. Na kwa bahati mbaya sana chama hicho ni ccm.
Kwa hiyo naklubaliana nawer Mchambuzi kwa nini vijana wanakimbilia chaguzi za chama hicho.
Wakurogwa anasema wanaenda kujenga nchi; Angalau angetumia neno 'baadhi' au 'wengi' kama mimi nilivyotumia neno hili kwenye hoja yangu ya msingi; Unajua tabia hii ya baadhi ya wana ccm wenzangu kama wakurogwa ndio watakuwa wanakanyaga wananchi na magari au malori barabarani siku chadema inatupokonya ikulu kwani kwao itakuwa ni kama vile CCM imeporwa uchaguzi; wanaishi maisha ya utopia, na ya CCM baba, CCM mama; Mimi ningeweza kabisa kuwa mpiga debe wa CCM kama yeye, tena nina mizizi mirefu tu kwenye chama hiki, lakini my intellect hainiruhusu nifanye hivyo, na namshukuru mungu kwa hilo; Otherwise I have chosen not to be a jester, ideologue or demagogue kama wakurogwa na wengine;

Tanzania kwanza, CCM baada;
 
Barubaru

Barubaru

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2009
Messages
7,160
Points
0
Barubaru

Barubaru

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2009
7,160 0
Hakika nimeupenda sana uchambuzi wako na ungekuwa na manufaa kwa jamii yote kama usingekuwa umeonyesha USHABIKI wa kisiasa ndanimwe.

Kumbuka katika Miiko ya uandishi wa habari ambao ni muhimili mkuu wa nne (usio rasmi) katika nchi zenye kufuata Rules of Law, utaona Mwandishi kazi zake kuu ni Kuielimisha jamii, Kuipasha jamii habari na kuiburudisha jamii. Na MWIKO MKUBWA SANA KWA MWANDISHI NI USHABIKI ambao ahali yangu umejikita kwayo.

Labda kwa kukusaidia zaidi huko Tanzania. Vijana wengi wanajikita katika siasa sababu kuu ni
1. Wamekosa kazi za kuajiliwa( Kani ilmu ya Tanzania inamwandaa mtoto akimaliza skuli/ Chuo kikuu) kuajiliwa na SIO Kujiajiri.
2. Kazi za Siasa kama Ubunge au hata udiwani ndio kazi inayolipa zaidi bila kutoa jasho (Angalia mishahara yao na marupurupu yao)
3. Zao la Chama kushika hatamu za uongozi wa nchi. Dhana hii imeweka wanasiasa juu kuliko mtu yoyote Serikalini.

Na La mwisho kutokana na ukosefu wa Kazi za Kuajiliwa huko Tanzania. Vijana wengi siku hizi wanajikita SIO tu Katika SIASA lakin pia wanajikita katika Sanaa za Music wa dance na Michezo ya kuigiza ili wapate Rizk.

Nakushauri.

kama utapunguza ama kuacha USHABIKI katika makala zako utakuwa mchambuzi mzuri sana.
 
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Messages
966
Points
250
M

Mgaya D.W

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2012
966 250
Mkuu Mchambuzi salam,
Binafsi nimependa sana majadala huu kuja kwa sasa na kwa kweli uchambuzi wako umeongozwa na hekima na busara uliyojaliwa na Mwenyezi Mungu na hivyo kujitahidi kumfanya kila mwenye kuhitaji kuelewa akuelewe bila shida yoyote.

Labda niende moja kwa moja ktk mada yako,uchambuzi wako ktk Leadership Recruitment na Leadership Succession umekaa vizuri sana lakini pia nashukuru wenzangu wamejaribu kuona ukubwa wa tatizo na pengine chanzo cha tatizo lenyewe kulingana na mjadala.Kwa hakika kama hatutakuwa makini na mwenendo huu wa siasa za kutafuta kula na si kutumikia Taifa itapelekea kuwa nchi ya wevi,matapeli na mafisadi kwa kuwa kila mtu anapigania kupata pa kula na hasa hizo political oportunities kwa kuwa hujiona wao ndo wao ktk nchi.

Labda nikumbushe tu kitu kimoja ambacho ndg.Mchambuzi hukukitaja ni tatizo la ajira,hili ndilo linaloleta mizozo,vurumai na sekeseke kwa kuwa sasa watu hawaongozwi na nia thabiti,moyo wa uzalendo na kukuza career zao,sasa watu wanatizama wapi apate akale.Ukweli huu wa ajira ambao pia umewahi uzungumzia sehemu fulani hapa jamvini.Nini vijana wanatazama,wanachotazama ni wapi na kuna nini cha kumtoa alipo na kufikia atakapo,so kwenye siasa ndiyo imeonekana ndiyo sehemu pekee ya kufanikisha mambo yako kwa haraka na hili ni kwasababu wameshaona wenzao waki-ula,wakifanikisha mambo yao faster faster,wakipata heshima hizo wazitakazo so wanaona kunasababu gani wao kuendelea kuwa nje ilihali mwanya upo?

Tatizo jingine linalopelekea vijana na watu wengine kuendelea kukimbilia huko ccm ni sehemu ya uhakika kwa sasa na usalama wao kwa lolote,na kama ulivyosema kuwa tatizo hili pia limeanza kujitokeza chama cha chadema,kwa nini chadema nako ni kwasababu mianya ya kuula imeanza kuonekana so what youths need ni oportunities za kufanikisha maisha hata kama njia hiyo ni haramu.Nimeona wakati fulani vijana wenzangu huku site wakiwa hata kijieleza hawajui,wamesoma fani ambazo hawakuwahi kufikiria kuzisoma maana hata elimu yenyewe ni bora mtu aonekane ana degree but na watu hawaondani na career zao na wapo kama wapo tu.Kwangu hili naona ni tatizo hasa mtu anshindwa kuendeleza career yake kwa kuwa hana uwezo nayo,mtu kusomea kitu ambacho hukuwahi kuwa na interest nacho si rahisi kuendeleza career hiyo so bora kukimbilia kwenye siasa ili kujenga uhakika wa kuishi na kwa kuwa Political oportunities hazina garantee ndiyo maana kila mwenye kupata upenyo lazima aibe ili akikosa kesho naye awe sehemu fulani.

Mchambuzi,nchi ilishaondoka kwenye reli yake siku nyingi na hivyo hakuna ajuaye wapi tuliko na wapi tunahitaji kufika,hii ina maana kwamba hata atakaye chukua nchi miaka ijayo hasa wakiwa wapinzani lazima kwanza turudi kwenye base(msingi) ndipo tuanze safari ya kuelekea huko tukutakako.Tunaongozwa na watu wasio na dira,wamepoteza dira ya nchi na bado wameng'ang'ania usukani.Pale watawala watakapojua kuwa nchi hii ni ya wote nadhani tayari tutakuwa tumechelewa sana na hivyo hata watoto wetu wakiwa matumboni mwa mama zao watakuwa wanafikiria namana ya kuwin via shortcut.

Bado ninaamini,kama vijana tunaojitambua na wenye nia ya dhati kwa taifa hili bado htujachelewa sana japo ili hili nalo liweze kueleweka lazima lirudiwe mara nyingi na wazalendo walio wengi ili kujenga misingi kwa mstakbali wa Taifa letu.Mjadala ni mzuri pamoja ya kwamba wengine hawatokubalina na hoja zetu.
 
Last edited by a moderator:
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
216
Points
170
Age
63
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
216 170
Sawa mkuu, CCM OYEE!
Mchambuzi usinichagulie chama nina haki ya kutoa maoni yangu katika mada yako kama ulivyodai ni straight forward kwa hiyo hoja yangu usiweke kwa mtazamo uliokuwa na sina hata chembe ya U-CCM bali nimesimamia ukweli katika thread yako.Inawezekana umekubaliana nami ndiyo maana umekosa hoja katika komenti yangu.Nashukuru kwa kukubali ukweli.
 
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2011
Messages
216
Points
170
Age
63
W

Wakurogwa

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2011
216 170
Wakurogwa anasema wanaenda kujenga nchi; Angalau angetumia neno 'baadhi' au 'wengi' kama mimi nilivyotumia neno hili kwenye hoja yangu ya msingi; Unajua tabia hii ya baadhi ya wana ccm wenzangu kama wakurogwa ndio watakuwa wanakanyaga wananchi na magari au malori barabarani siku chadema inatupokonya ikulu kwani kwao itakuwa ni kama vile CCM imeporwa uchaguzi; wanaishi maisha ya utopia, na ya CCM baba, CCM mama; Mimi ningeweza kabisa kuwa mpiga debe wa CCM kama yeye, tena nina mizizi mirefu tu kwenye chama hiki, lakini my intellect hainiruhusu nifanye hivyo, na namshukuru mungu kwa hilo; Otherwise I have chosen not to be a jester, ideologue or demagogue kama wakurogwa na wengine;

Tanzania kwanza, CCM baada;
Mkuu!! nilikueleza tangu awali kwamba mada yako umeegemea upande fulani na ulipenda kila anayekomenti thredi yako awe upande wako.Wengine siyo wavivu wa kufikiri.Mi nafahamu kwamba we unaelewa sana kwanini vijana kwa sasa wanapenda sana kuingia kwenye siasa na baadhi ya watu wamekupa maoni mazuri tu ila tatizo lako umekariri majibu.Vijana wote wanaoingia kwenye siasa kwa sasa wengi wao ni kurekebisha maisha yao na siyo vinginevyo nakubaliana na wewe kwamba baadhi yao ni mapaka pori lakini wengine wapo kwa ajili ya kulisukuma taifa hili katika maendeleo na hawa mapaka pori wapo katika vyama vyote na ndiyo maana zipo lawama za hapa na pale tunashuhudia wabunge vijana kwenye majimbo yao kuna changamoto nyingi tu lakini hadi sasa hawajazitatua wote wanafuata ulaji tu ili waboreshe maisha yao.Nitajie kama utaweza walao kijana mmoja ambaye anaishi maisha yanayofanana kabla hajaingia kwenye siasa.Karibu wengi maisha yao yapo tofauti yamebadilika wana nyumba na magari na vitu vingine vingi tu vyenye thamani.Nashukuru umejisema wazi kwenye komenti yako sasa kwanini ulikuwa unafichaficha!!!
 
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
4,888
Points
1,225
Bongolander

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
4,888 1,225
Wakurogwa anasema wanaenda kujenga nchi; Angalau angetumia neno 'baadhi' au 'wengi' kama mimi nilivyotumia neno hili kwenye hoja yangu ya msingi; Unajua tabia hii ya baadhi ya wana ccm wenzangu kama wakurogwa ndio watakuwa wanakanyaga wananchi na magari au malori barabarani siku chadema inatupokonya ikulu kwani kwao itakuwa ni kama vile CCM imeporwa uchaguzi; wanaishi maisha ya utopia, na ya CCM baba, CCM mama; Mimi ningeweza kabisa kuwa mpiga debe wa CCM kama yeye, tena nina mizizi mirefu tu kwenye chama hiki, lakini my intellect hainiruhusu nifanye hivyo, na namshukuru mungu kwa hilo; Otherwise I have chosen not to be a jester, ideologue or demagogue kama wakurogwa na wengine;

Tanzania kwanza, CCM baada;
Mchambuzi this is very interesting comment. Lakini nikija kweli swali lako....naweza kujibu kwa swali. Nikianzia mwanzo kabisa.

Tulipopigiania uhuru, kimsingi tulikuwa tunapigania madaraka na mamlaka, kama nakumbuka vizuri kuna mahali mwlaimu alisema mdaraka kama madaraka tu hayana maana sana, hasa kama anayepewa madaraka hajui anataka kuyatumia kwa manufaa gani.

Tulimuaondoa Sir Edward Twinning ili tuwe na Waziri Mkuu atakayetumia madaraka yake kutusaidia kuondoa umaskini, ujinga, kudharauriwa na kupuuzwa. Nyerere na wenzake walijitahidi sana kufanya kazi hizo. We have a large body of evidence to prove that, despite all short comings and disappointments, madaraka yao yalikuwa kwa ajili ya manufaa ya wanaowatawala.

Walipokea kijiti kwa mwalimu, naona kama kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwandoa wananchi kutoka kwenye lindi tuliloingia kutokana na kuwekewa vikwazo. Yaani reforms and opening up. Na Mkapa aliendelea nayo kiasi na kuleta fiscal discipline na kuimarisha uchumi kiasi. Kutokana na kazi waliyofanya walipokuwa madarakani unaweza kusema waligombea ili wafanye kazi hizo. As a team. sina hakika kaa individually walikuwa na mawazo hayo.

Lakini mpaka sasa sijui ni kwanini JK aliamua kuwa Rais, sijui alipanga kuifanyia nini Tanzania akiwa rais, naweza kusema hilo ni swali pia la kuwaliza baadhi ya wabunge wengi wa sasa. Swali hili naweza kumuuliza hata Halima Mdee, John Komba, Vuai Nahodha.....kwanini waligombea wanataka kufanya nini. Sidhani kama yale ya kusema nguvu mpya, kasi mpya maisha bora kwa kila mtanzania ni lengo la JK, au kauli wanazotoa wabunge kwenye kampeni ndio zenyewe, nadhani matokeo ya kazi zao yanaweza kuonesha ni nini sababu ya wao kugombea.

Kimsingi naweza kusema ukiangalia kwa CCM, vijana wengi wanaogombea wengi ni kutafuta fursa tu za kupata pesa, infact hawana wanalofikiri kuifanyia Tanzania, zaidi ya kuitumia CCM na kuona itawafanyia nini. Siku hizi ukiona mtu anavaa koti la kijani au shati la kijani ujue huyo anatafuta kitu, si kama ana kitu cha kutoa.

Lakini tusiangalie tu kwenye nafasi za kugombea, kuna tabaia za ajabu sana hata kwenye nafasi za kuteuliwa. Labda utakuwa unakumbuka waziri mmoja kijana yeye uwaziri ni kujionesha tu kuwa na madaraka na kutafuta wanawake. Kuna jamaa mmoja namkumbuka aliteuliwa kuwa naibu Mkurugenzi wa kampuni fulani, nakumbuka kabisa alichokuwa anafanya ni zile kazi la kila siku ambazo hata messenger anaweza kufanya. Alichokuwa anasema ni kuwa mabibi wote sasa ntawapata, hiyo ndio ilikuwa fikra yake kubwa.

Kwa hiyo inategemea mara nyingi elimu, utamaduni hata utashi binafsi wa huyo kijana anayegombea nafasi kupitia chama chochote. sio CCM tu.
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Nashukuru umejisema wazi kwenye komenti yako sasa kwanini ulikuwa unafichaficha!!!

Hakuna nilichoficha
, pitia vizuri bandiko namba moja mstari kwa mstari, pengine wewe umeisoma kwa kujificha;
Umeamua tu kutoelewa hoja yangu ya msingi na unabeba rangi zote za kutetea status quo; ungekuwa ni mtu makini na neutral ungeelewa neutrality yangu kwenye bandiko langu namba moja - kwanza najibu hoja ya wildcat, pili najibu zinazotolewa na viongozi wa ccm ambao wanajisifia vijana na wasomi wengi kwenda CCM, lakini muhimu zaidi katika bandiko langu namba moja, nimeelezea wazi kabisa kwamba mjadala huu utakuwa na manufaa kwa vyama vyote, sio ccm tu, na mwishoni nikasema chadema nao wameingiwa na jinamizi hili; ccm ipo kati kwa sababu ndio chama tawala na viongozi wake wengi uenda kutumikia serikali ya walipa kodi; vinginevyo kama umeamua kuelewa unavyotaka, ni haki yako, muhimu ni kwamba wapo walionielewa kabla ya kuwa na hoja mbadala; wewe unakataa ukweli uliopo na kuona ninatunga; hiyo ni haki yako pia;
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Hakika nimeupenda sana uchambuzi wako na ungekuwa na manufaa kwa jamii yote kama usingekuwa umeonyesha USHABIKI wa kisiasa ndanimwe.

Kumbuka katika Miiko ya uandishi wa habari ambao ni muhimili mkuu wa nne (usio rasmi) katika nchi zenye kufuata Rules of Law, utaona Mwandishi kazi zake kuu ni Kuielimisha jamii, Kuipasha jamii habari na kuiburudisha jamii. Na MWIKO MKUBWA SANA KWA MWANDISHI NI USHABIKI ambao ahali yangu umejikita kwayo.

Labda kwa kukusaidia zaidi huko Tanzania. Vijana wengi wanajikita katika siasa sababu kuu ni
1. Wamekosa kazi za kuajiliwa( Kani ilmu ya Tanzania inamwandaa mtoto akimaliza skuli/ Chuo kikuu) kuajiliwa na SIO Kujiajiri.
2. Kazi za Siasa kama Ubunge au hata udiwani ndio kazi inayolipa zaidi bila kutoa jasho (Angalia mishahara yao na marupurupu yao)
3. Zao la Chama kushika hatamu za uongozi wa nchi. Dhana hii imeweka wanasiasa juu kuliko mtu yoyote Serikalini.

Na La mwisho kutokana na ukosefu wa Kazi za Kuajiliwa huko Tanzania. Vijana wengi siku hizi wanajikita SIO tu Katika SIASA lakin pia wanajikita katika Sanaa za Music wa dance na Michezo ya kuigiza ili wapate Rizk.

Nakushauri.

kama utapunguza ama kuacha USHABIKI katika makala zako utakuwa mchambuzi mzuri sana.
Popote unapoona nina ushabiki unatakiwa kupajadili kwa hoja ili nirudi kwenye mstari, kama sisi tunavyosema kila wakati unapokuwa na hoja za kidini na maneno yenye kukashifu badala ya kujenga; Ni kawaida kupitiwa mara nyingine kwani sote nui binadamu na tuna emotions lakini ni muhimu pia kukubali kukosea; vinginevyo umeongea ya msingi sana katika bandiko lako, hasa zile sababu tatu kwanini vijana wengi hujikita katika siasa; hakuna sehemu ulipojadili kwamba kimsingi ni wanaenda kutumikia nchi, na upo sahihi katika hili; vinginevyo kimsingi ni for private gain, suala la public gain ni baadae, ingawa mwenzetu wakurogwa haoni hilo;
 
Forum statistics

Threads 1,296,621
Members 498,672
Posts 31,254,017
Top