Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Ni ukweli usiopingika kuwa kundi la vijana katika nchi yoyote ile linabaki kuwa kundi muhimu katika kusukuma ajenda mbalimbali. Mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu vijana tulikuwa mstari wa mbele katika nyanja zote kwa maana ya Michakato ya kuwapata wagombea, Kampeni za Vyama vya Siasa, Uchaguzi wenyewe na hata baada ya kutangazwa washindi wa uchaguzi vijana tuliingia barabarani kuwapongeza washindi kwa maandamano, kucheza na shangwe za kila aina.
Nimeandika uzi huu kwa lengo moja tu kwamba kama tulivyofanya 2015 kwa kutambua wajibu wetu kama vijana tufanye kweli 2020 kwenye uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha tunawachagua viongozi wenye sifa. Pia sisi vijana ambao ni kundi kubwa kuelekea uchaguzi ujao tuwe walinzi wa amani yetu kwa kushiriki kikamilifu katika hatua zote kama tulivyofanya 2015.
Vijana tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa, tuingie kwenye hizo nafasi kwa kuwa uwezo wa kuongoza tunao, sababu za kuongoza tunazo na nia tunayo! Zaidi ya yote vijana tunao wajibu wa kujitokeza kupiga kura mwaka 2020 zaidi ya vile tulivyofanya mwaka 2015, tuhakikishe tunashiriki moja kwa moja katika kuwaweka madarakani viongozi tunaowataka.
Mwisho kuelekea uchaguzi ujao, kwa mujibu wa majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutakua na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi hasa waliofikisha umri wa miaka 18 waweze kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu ujao, chonde chonde vijana tuitumie vizuri fursa hii, naamini tutajitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zetu na wale wasiokuwa na Kadi za kupigia kura ambao watakuwa wametimiza umri watawezeshwa kuwa na kadi hizo ili wapige Kura.
Vijana ndio sisi, Kama kawaida 2020 ni mafuriko ya kwenda kupiga Kura, Hakuna kulala!