Vijana, hawana ajira, Wazee ajira za mikataba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana, hawana ajira, Wazee ajira za mikataba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MchunguZI, Mar 22, 2012.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Eti nimesikia kuna mjadala wa Kitaifa juu ya ukosefu wa ajira TZ. Ni jambo la kushangaza ktk nchi hii.

  Ni kweli kabisa kwamba Vijana hawana ajira. Elimu ya juu inamwaga kila mwaka, wanaoajiliwa ni chini ya robo yao. Wakti hayo yakitokea, wazee hawaondoki madarakani na kuna wazee wengi wanaomba jira za mikataba. Vijana kweli mutapata ajira?

  Vyuo vikuu sasa hivi vinaendeshwa na wastaafu. Kila profesa anayestaaafu anapewa mkataba.
  Makatibu wakuu wa Wizara pia wanaendesha Wizara kwa ajira za mikataba.
  Wakurugenzi ni mtindo huo huo wa ajira za mikataba.
  Mabalozi wetu nje ya nchi ni hivyo hivyo!

  Wapi tunakokwenda?
   
 2. b

  baba koku JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mimi sishabikii mtindo wa kuwapa mikataba wastaafu, lakini siamini kuwa hao ndio kielelezo au kisababishi cha vijana kukosa ajira. Hivi kwa mfano, zile ajira za mikataba za wastaafu zikisitishwa au kufutwa kabisa, ndio tutakuwa tumeondoa tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana?
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,493
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
  Hao wastaafu wanazuia fresh ideas kuja kurekebisha mambo!! They think ujamaa at this time of a century badala ya kuthink grobalization!! Hukusikia walitaka kurudisha JKT!!!
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo unataka ma-prof wote wafutwe kazi???????/. unachekesha kweli.
   
 5. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ukweli utaratibu wa kuwapa mikataba wanaotakiwa kustaafu c mzurio na hauawa na mafanikio,mtu kashalipwa mafao yake then anaanza kufanya kazi kwa mkataba hata responsibility inapungua mbali ya kufinya fursa za ajira/madaraka kwa vjana. Huwa sishangai hata Kamnda wa Polisi Nzowa wa kikosi cha kuzuia madawa kutajwa kushiriki mpango wa kumwekea madawa mtoto wa Mengi kwa malipo makubwa. Enzi zake mzee yule alikuwa kaksi,lkn leo anafanya kwa mkataba si ajabu alikubali kweli rotten deal kama ile
   
 6. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  sasa nyie vijana mnataka mmepewa mikataba ya hao Maprofesa? Kazi siyo kuajiriwa tu ofisini. tumieni Elimu yenu Kujiajiri.
   
 7. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  and it does'nt mean that all Professors are above age as they contunue wiz their employment.
   
 8. m

  moshingi JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikamanda mingi ya Polisi ipo kwa mikataba, wengi wao walishastaafu zaidi ya miaka mitatu iliyopita, wao ndiyo
  chanzo cha unyanyasaji wa Raia...mtu akistaafu asiongezewe hata siku moja...kama hamkuandaa vijana wa kushika
  madaraka kwa muda wote wa miaka 30 ya utumishi wao shauri yenu...Wanapoongezewa mikataba huvurunda sana
   
 9. Mkale

  Mkale JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 700
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 80
  Nafasi za ajira zina toka kila siku, tatizo kujuana kwingi.
   
 10. K

  Kyoombe JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 649
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Ili vijana wapate ajira inabidi umri wa kustaafu kwa hiari urejeshwe kuwa 50 yrs na kwa lazima 55 yrs. Hali ingebadilika kidogo.
   
 11. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,721
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi la leo, nikaona historia, takwimu na mikakati mingi isiyotambulika juu ya kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira, waziri Kabaka alikuwa anamjibu Lowasa n.k, kwani Lowasa amekuwa 'akiionya' serikali juu ya ukosefu wa ajira nchini.
  KUHUSU AJIRA, TUPIGE MAGOTI TUSALI!
   
 12. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Tunaweza tukapunguza umri lakini ni vigumu maana watu wanaendelea kuwa na maisha marefu. Tatzizo ni huu mtindo wa kupeana mikataba hata kama huyo anayepewa mkataba hana tija.

  Nimesikia VC wa Dodoma Prof. Kikula anatakiwa kuondoka kwa umri. VC wa UDSM pia kisha staafu lakini naye anaachwa tu utadhani wamefanya la maana. Hayo yote yanafanyika kwa urafiki badala na ubora wa uongozi wao.
   
 13. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nasikitika kule Costech, wizara ya elimu na wizara ya mifugo wastaafu wamejazana:siyo kila mstaafu ana taaluma 'rare' wengi wao wanazo Msc. sawa kabisa na vijana na wengine wana PhD zaidi ya wastaafu wanaopewa mikataba. Hili pia ni tatizo hata kama si pekee chanzo cha kukosa ajira vijana
   
Loading...