Vijana CUF wataka mitihani Z’bar irudiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana CUF wataka mitihani Z’bar irudiwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 10, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Talib Ussi, Zanzibar
  JUMUIYA ya Vijana ya CUF (JUVICUF), imeelezea kusikitishwa kwake kuhusu kufutwa kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ya skuli kadhaa za Zanzibar.

  Jumuiya hiyo imesema kitendo hicho kinaonyesha kuwa Serikali haina nia njema na maisha ya wanafunzi hao.

  Hayo yamo katika taarifa ya chombo hicho kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Khalifa Abdallah Ali.

  “Unapowafutia matokeo watoto hao unawasababishia athari kubwa za kisaikolojia na hata kushindwa la kufanya,” ilisema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo ilisema walimu ndiyo wanaopaswa kubeba lawama kuhusu kuvuja kwa mitihani na kwamba inasikitisha kuona kuwa hawahukumiwi.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo jumuiya hiyo haiamini kama msingi wa tatizo hilo ni wanafunzi pekee yao.

  “CUF ilishasema kuwa inapotokea kesi kama hiyo, Baraza la Mitihani linapaswa kuwachukulia hatua wale waliosababisha kuvuja kwa mitihani na mitihani hiyo ichapishwe upya,” ilisisitiza taarifa.

  “Tunaiomba wizara ihakikishe kuwa mitihani hii inarejewa ili wanafunzi walioathirika watendewe haki yao,” ilisema.

  Taarifa hiyo ilisema kurejewa kwa mithani si jambo geni hasa ikizingatiwa kuwa ilishawahi kurejewa katika baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam .:A S 465:
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hapo Point ni kwamba saikolojia ya mtoto inavurugika sana
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naunga hoja mkono.
   
Loading...