Vijana CUF wapata safu mpya ya uongozi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]ALHAMISI, JULAI 19, 2012 05:41 NA ELIZABETH MJATTA, DAR ES SALAAM

BARAZA Kuu la Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), limetangaza kamati mpya ya utendaji ya Jumuiya ya Vijana Taifa (JUVICUF) ambapo watu 17 wameingia katika kamati hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema baada ya kazi kubwa iliyofanywa na jumuiya za chama imeonekana kuwa zinapaswa kuimarishwa zaidi, ikiwamo JUVICUF.

Alisema viongozi walioteuliwa na kuthibitishwa na Baraza Kuu ni pamoja na Katani Katani ambaye amekuwa Mwenyekiti, Yusuph Makame (Makamu Mwenyekiti), Khalifa Ali (Katibu), Thomas Malima (Naibu Katibu).

Wajumbe ni pamoja na Sonia Magongo, Bonifasia Mapunda, Kuruthumu Mchuchuli, Said Maulind, Ashura Mustapha, Hamidu Bobali, Ahmed Mudhihir, Shomvi Issa, Faustin Khalifan, Suleiman Abdallah, Biubwa Mselem, Pavu Abdallah, Gora Hamis, Hafidh Hafidh na Ayoub Khamis.

Alisema viongozi hao watafanya kazi ya kuimarisha chama, hususani kupambana na changamoto mbalimbali zinazohusu vijana katika mustakabali wa Taifa.

Awali, jumuiya hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Mohamed Babu na Naibu Katibu wa Vijana Bara, Abubakar Kitogo, ambao wameachwa katika uteuzi huo.

 
Oh wow afadhali wakristo wame-park kwenye hiyo kamati ya VIJANA...
 

Aisee! Ha ha ha ha ha ha! Asante Lipumba; kweli haki sawa kwa wote. Simpe arithmetic: (19/21) x 100 = 90.5%. Huyu kweli anajua ku-balance.
 
hongera cuf kwa mabadiliko mazuri sana.
Hivi huo ujumbe wa Vijana wa CUF, umri wa kuwa kijana unaishia miaka mingapi? Nimemwona dada yangu mmoja ktk orodha ya wajumbe ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari wa CUF ambaye kwa umri wake alipaswa kuwa ktk Jumuiya ya Wanawake ya CUF.
 

Aisee! Ha ha ha ha ha ha! Asante Lipumba; kweli haki sawa kwa wote. Simpe arithmetic: (19/21) x 100 = 90.5%. Huyu kweli anajua ku-balance.
Sasa ulitaka Prof afanyeje kama hao unaodhani wamepunjwa hawapo? Mwenyekiti achague mawe?
 
Back
Top Bottom