Vijana CUF sasa watishia Serikali

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Dar es Salaam. Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), imetishia kuandamana nchi nzima ikiwa haki haitatendeka kwa mwenyekiti wao, Katani Ahmed Katani aliyekamatwa na na polisi kwa tuhuma za uchochezi mkoani Mtwara.

Mwenyekiti huyo, alikamatwa Alhamisi Dar es Salaam na kusafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Mtwara, ambako vurugu zilizotokea kupinga ujenzi wa bomba la kusafirishwa gesi kwenda jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa JUVICUF, Yusufu Kaiza aliwaambia akisema “Tunataka atakapofikishwa mahakamani apewe dhamana na kama tukiona haki haitendeki juu yake, sisi tutaitisha maandamano nchi nzima kuhakikisha haki inatendeka’’.

Kaiza alisema Serikali inatakiwa kukutana na wananchi wa Mtwara na kuzungumza nao kwa undani juu ya manufaa watakayoyapata kutokana na mradi wa gesi asilia na siyo kuanza kukamata watu ovyo.

Alisema Katani alikamatwa Alhamisi baada ya kupigiwa simu na maofisa wa polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na alipofika aliwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa kwa saa kadhaa.

“Katani anakubalika sana mkoani humo kutokana na kujulikana sana kisiasa kwani mwaka 2010 aligombea Ubunge Jimbo la Tandahimba na kushindwa kwa mizengwe’’, alisema Kaiza.
 
Dar es Salaam. Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), imetishia kuandamana nchi nzima ikiwa haki haitatendeka kwa mwenyekiti wao, Katani Ahmed Katani aliyekamatwa na na polisi kwa tuhuma za uchochezi mkoani Mtwara.

Mwenyekiti huyo, alikamatwa Alhamisi Dar es Salaam na kusafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Mtwara, ambako vurugu zilizotokea kupinga ujenzi wa bomba la kusafirishwa gesi kwenda jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa JUVICUF, Yusufu Kaiza aliwaambia akisema "Tunataka atakapofikishwa mahakamani apewe dhamana na kama tukiona haki haitendeki juu yake, sisi tutaitisha maandamano nchi nzima kuhakikisha haki inatendeka''.

Kaiza alisema Serikali inatakiwa kukutana na wananchi wa Mtwara na kuzungumza nao kwa undani juu ya manufaa watakayoyapata kutokana na mradi wa gesi asilia na siyo kuanza kukamata watu ovyo.

Alisema Katani alikamatwa Alhamisi baada ya kupigiwa simu na maofisa wa polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na alipofika aliwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa kwa saa kadhaa.

"Katani anakubalika sana mkoani humo kutokana na kujulikana sana kisiasa kwani mwaka 2010 aligombea Ubunge Jimbo la Tandahimba na kushindwa kwa mizengwe'', alisema Kaiza.
Mkuu hayo mandamano ya nchi nzima yatapita njia gani au anadhani hii nchi ni kuchezea kama maalimu anavyowachezea wao cuf.
 
Aisee, kaandamane Jikoni kwa mkeo akichelewa kukupikia usipoacha kumpatia fedha ya chakula kutokana na kukesha humu kupost thread za kjinga
 
huyu ni zaidi ya lema, hawa tufuatilie historia zao, anachofanya huyu bwana ni zaidi siasa.....hana adabu.
 
Maajabu saba ya dunia haya. Sisimizi anatishia tembo. Dooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Aisee nilikuwa sijui kama na CUF nao wanao Jumuiya ya vijana.

By the way labda mkafanye maandamano nchini Zanzibar huku Tanganyika hamna lenu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ole wao wasimwachie tutakuja kumchukua wenyewe

Nyie Maliberali na waume zenu si ndio kila siku mnawalaani Chadema kwamba ni Chama cha Maandamano! Kumbe ni Chuki binafsi tu! Mkiwa wapinzani hamuwezi kuhepuka maandamano kwa ukandamizaji WA demokrasia unaoendelea kwenye nchi hii! Waombeni radhi Chadema kwa talalila zenu mnazopiga mkiwa na Mume wenu Mr. Gamba.
 
Back
Top Bottom