kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), kupitia vyombo vya habari nchini, limekaririwa likisema litazuia Mkutano Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu mjini Dodoma.
Mkutano huo maalumu wa Julai 23, mwaka huu una dhamira moja tu, kukabidhi uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa Rais John Magufuli kutoka kwa Mwenyekiti wa sasa, Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.
Lakini wakati CCM wakijipanga kwa shughuli hiyo ya ndani ya chama, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi alisema Bavicha imeamua kuzuia mkutano huo kutokana na tamko la Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yote ya kisiasa.
Ingawa Patrick hakufafanua, alisema watatumia njia halali kuhakikisha mkutano huo hautafanyika kama ambavyo mikutano ya vyama vingine imezuiwa na Jeshi la Polisi nchini. Wameongeza kuwa, vijana wa Chadema kutoka mikoa yote nchini wanaandaliwa kwenda Dodoma kuzuia mkutano huo maalumu wa CCM.
Wamezungumza, tumewasikia lakini baada ya kutafakari, tunajiuliza, vijana hawa wa Chadema wanajua wanachokizungumza? Na watafanya haya kwa maslahi ya nani? Maswali ni mengi, hasa kutokana na ukweli kwamba, kilichozuiwa na Jeshi la Polisi ni mikutano ya hadhara, tena ile inayoonekana kuwa na vimelea vya uvunjifu wa amani.
Na wanachokwenda kukifanya CCM mkoani Dodoma si mkutano wa hadhara, bali mkutano wa ndani wa chama hicho. Kama ndivyo, una athari gani kwa amani ya nchi? Tuonavyo sisi, vijana hawa wa Chadema hawakujipa muda wa kutafakari juu ya tamko lao.
Aidha, wanapaswa kufahamu ya kwamba, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa mikutano ya ndani ya vyama haiingiliwi hata na polisi na ndio maana hata mikutano ya viongozi wa juu wa vyama vya upinzani maarufu kama Ukawa, licha ya kukutana mara kwa mara haijawahi kuingiliwa na chombo chochote.
Tunaamini kwamba, kama kungekuwa na zuio la mikutano ya ndani katika nchi hii ni dhahiri wabunge wa Ukawa wasingebaki salama, hasa baada ya kususia vikao vya Bunge mjini Dodoma.
Mara zote, baada ya kutoka ndani ya Bunge, walikutana katika mikutano yao ya kimkakati na hakuna aliyeguswa. Huo ndio ukweli kwamba, mikutano ya hadhara, tena yenye mwelekeo wa kutaka kuchonganisha wananchi dhidi ya serikali au watawala ndiyo inayoangaliwa kwa jicho la karibu na hata kukemewa.
Na hata Rais Magufuli anayepakaziwa kupiga marufuku siasa nchini, mara kadhaa ufafanuzi umetolewa kuwa, kinachokataliwa ni siasa zisizo na tija, bali wanasiasa wajikite katika mambo ya msingi kwa lengo la kuijenga nchi, vinginevyo wasubiri kupiga porojo wakati wa kampeni katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.
Lakini kwa wakati huu, ni vyema nguvu za vijana hawa zingetumika vizuri kusaidia kujenga uchumi wa nchi. Ni wakati ambao vijana wangeutumia katika kusaidia utengenezaji wa madawati, kusaidia ujenzi wa miradi ya maji, kwenda kukaa na kuwafundisha ujasiriamali vijana wasio na elimu na kadhalika.
Tunajiuliza, kwa kupoteza muda na rasilimali kwenda Dodoma kuvuruga mkutano wa CCM, vijana hawa watapata faida gani zaidi ya kuonekana wakorofi, wenye dhamira ya kuibua chokochoko na ambao huenda wakitawanywa kwa mabomu wataishia kulia kuwa wanaonewa?
Je, kinachowapeleka Dodoma ni kwenda kutafuta haki au huruma za kisiasa? Tuonavyo sisi, vijana wa Chadema wanapaswa kutakafari upya juu ya dhamira yao hiyo, na badala yake wajipange kuja na siasa zenye mashiko, zitakazomsaidia kila Mtanzania kusonga mbele, badala ya kuturudisha katika vurugu za kisiasa.