Vijana CCM Misenyi wamuumbua vibaya Nape Nnauye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana CCM Misenyi wamuumbua vibaya Nape Nnauye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 28, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, kimekutana na wakati mgumu kwa kuumbuka mbele ya Katibu wa Taifa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa baraza la vijana la wilaya hiyo lililofanyika Ijumaa.
  CCM imeumbuka baada ya vijana wake wilayani hapa kuonesha msimamo wao ndani ya chama hicho, kwa kususia baraza la vijana lililokuwa limeandaliwa, ambalo katika hali isiyo ya kawaida liliudhuriwa na wazee ambao ni pamoja na kina mama, kina baba na watoto.
  Baraza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa vilivyoko eneo la Bunazi yalipo makao makuu ya Wilaya Misenyi, vijana wengi wa CCM walisusia baraza hilo kwa madai ya kutokuwa na imani na serikali iliyoko chini ya CCM.
  Wakati baraza la vijana likiendelea, vijana wengi, hasa ambao ni wakereketwa wa CCM, walionekana wakizurura ovyo, wakipita maeneo ambayo baraza lilikuwa likifanyika huku wengine wakiendelea na shughuli zao za kujipatia kipato.
  Vijana waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao, waliokutwa maeneo ya Bunazi karibu kabisa na eneo lilikokuwa linafanyika baraza, walisema CCM haina mwelekeo, wamechoka nayo kwa kuwa kila siku inaendelea kuwatelekeza.
  Kwa nyakati tofauti, walisema chama hicho kimeshindwa kabisa kulinda maslahi ya vijana badala yake kimekuwa kikiwatumia kila siku kufanikisha maslahi yake.
  “Mimi ni mkereketwa wa CCM, mbunge wa sasa nimeshiriki kumpigia kampeni hadi akapita, wengi walioko ndani ya chama wapo kwa ajili ya kulinda maslahi yao wala si maslahi ya walio nyuma yao,” alisema mmoja wa vijana.
  Kauli za vijana kususia baraza hilo, zilithibitika pale Katibu wa Umoja wa Vijana CCM wa Wilaya ya Misenyi, Philbert Ngemella aliposema mbele ya Nnauye kwamba vijana wamesusia baraza hilo kwa madai kwamba serikali iliyoko chini ya CCM haiwajali na imeshindwa kutafuta namna ya kuwawezesha kiuchumi.
  Aidha, wakati wa baraza hilo, mzee Abdul Mwanandege alimtahadharisha Nape awe makini sana ili CCM isifie kwenye mikono yake.
  Alisema CCM ni ya wanachama wote hivyo maamuzi ndani ya chama ni lazima yaende kulingana na matakwa ya wanachama.
  Mwanandege alisema mpasuko ulioko ndani ya CCM kwa sasa unatokana na maamuzi yanayotolewa, ambayo hayaafikiwi na baadhi ya wanachama, na kuongeza kuwa, ili chama kiendelee kuwa imara kinahitaji umakini zaidi.
  Naye Nape akihutubua baraza hilo la vijana alikiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM, akisema ndani ya chama kuna mamluki, ambao ndio chanzo cha mpasuko.
  “Watu hao tunao ndani ya chama na ndio wanatuvuruga ila tutaendelea kukabiliana nao hata kama chama kitabaki na mtu mmoja, tunataka watu safi wenye mapenzi ya dhati na chama,” alisema.
  Nnauye alisema CCM inaendelea na mkakati wake wa kuwaadabisha wale inaowabaini kuchangia mpasuko, na kwamba haitamfumbia macho mtu yeyote atakayeisaliti.
  Aliendelea kusema kuwa, CCM haimbembelezi mwanachama yoyote abaki ndani ya chama.
  “Nasema anayetaka kuhama ahame, hata kama nitabaki peke yangu chama kitaendelea kuwepo, CCM si mali ya matajiri, ni mali ya maskini,” alisema Nape kwa kejeli.
  Kauli hiyo ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na wanaCCM wachache walioudhuria baraza hilo, baadhi bila kutaja majina yao, wakisema kwamba Nape anakimaliza chama kwa kauli zake.

  Source:Tanzania Daima
   
 2. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vuvuzela alionekana kwenye TV wakati akiongea, misuli ya usoni ilikuwa imekakamaa, na mishipa ya damu kuonekana. Bila shaka haliu ilikuwa ngumu sana kwa Nyinyiem.
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hahahaha! Ngoja tu CCM ipumzike. Ila nahisi watabadili jina hivi karibuni ili ionekane imezaliwa upya.
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Nape Nnauye ni mteule wa Kikwete, namaanisha yule Kikwete aliyewadanganya wananchi kwamba atafanya maisha bora kwa kila Mtanzania lakini baadaye akastukiwa kuwa ni muongo wa kutupwa na uchaguzi uliofuata Watanzania walio wengi hawakumchagua lakini Tume ya Taifa ya uchaguzi iliamua kumtangaza kama Mshindi kwasababu katiba iliyopo hairuhusu kuhoji urais mahakamani. Hivyo tutegemee vituko zaidi kutoka kwa Nape
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nape ajue sasa mwisho wa CCM uko mlangoni
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  NAPE, kuwaita wenzako ni mamluki ni kosa hata wao wanakuona wewe ni mamluki toka CDM na CCK na hizo jitihada zako za kukifanya chama ni wewe na bila wewe hakuna chama utakiua chama chako kuwa makini

  sipendi chama kife bali kiwe cha upinzani wa kweli 2015
   
 7. d

  dmvuno Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni kisiwa cha amani, umoja na usawa, sasa hao ambao wanalalama ni sawa pia sautizao zisikike na zifanyiwe kazi. CCM ndio maana kuna demokrasia ya kweliio vyama vingine tayari wangewafukuza hao, lakini CCM ni chama cha wote. CCM oyeee!!, Nape kazi dume!!!!!!
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli na ww GT ? habari nusu nusu halafu tukikwambia hapakufai humu JF unaliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 10. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Maajabu;
  {Naye Nape akihutubua baraza hilo la vijana alikiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM, akisema ndani ya chama kuna mamluki, ambao ndio chanzo cha mpasuko.
  “Watu hao tunao ndani ya chama na ndio wanatuvuruga ila tutaendelea kukabiliana nao hata kama chama kitabaki na mtu mmoja, tunataka watu safi wenye mapenzi ya dhati na chama,” alisema.}
  -Nashindwa kuelewa hawa mamuluki wamepandikizwa na nani?
  -Je huyu msemaji ana mapenzi ya kweli na CCM?

  Kituko;
  {“Nasema anayetaka kuhama ahame, hata kama nitabaki peke yangu chama kitaendelea kuwepo, CCM si mali ya matajiri, ni mali ya maskini,” alisema Nape kwa kejeli.}
  -Alidhani anaiongelea CCJ nini?

  Wana masikio lakini hawasikii!, wanamacho likini hawaonina wana akili lakini hawatambui!.
  Ole wao siku ikifika.
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  na bado...
   
 12. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,833
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Hizi habari ambazo hazina nyama huwa zinanibore kweli kweli
   
 13. Ishina

  Ishina Senior Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari nusu nusu kivp?! Jamaa kakuambia ugonge hapo utapata habari yote.
   
 14. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] UVCCM wamtosa Nape Missenyi

  na Audax Mutiganzi, Misenyi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, kimekutana na wakati mgumu kwa kuumbuka mbele ya Katibu wa Taifa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa baraza la vijana la wilaya hiyo lililofanyika Ijumaa.
  CCM imeumbuka baada ya vijana wake wilayani hapa kuonesha msimamo wao ndani ya chama hicho, kwa kususia baraza la vijana lililokuwa limeandaliwa, ambalo katika hali isiyo ya kawaida liliudhuriwa na wazee ambao ni pamoja na kina mama, kina baba na watoto.
  Baraza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa vilivyoko eneo la Bunazi yalipo makao makuu ya Wilaya Misenyi, vijana wengi wa CCM walisusia baraza hilo kwa madai ya kutokuwa na imani na serikali iliyoko chini ya CCM.
  Wakati baraza la vijana likiendelea, vijana wengi, hasa ambao ni wakereketwa wa CCM, walionekana wakizurura ovyo, wakipita maeneo ambayo baraza lilikuwa likifanyika huku wengine wakiendelea na shughuli zao za kujipatia kipato.
  Vijana waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao, waliokutwa maeneo ya Bunazi karibu kabisa na eneo lilikokuwa linafanyika baraza, walisema CCM haina mwelekeo, wamechoka nayo kwa kuwa kila siku inaendelea kuwatelekeza.
  Kwa nyakati tofauti, walisema chama hicho kimeshindwa kabisa kulinda maslahi ya vijana badala yake kimekuwa kikiwatumia kila siku kufanikisha maslahi yake.
  "Mimi ni mkereketwa wa CCM, mbunge wa sasa nimeshiriki kumpigia kampeni hadi akapita, wengi walioko ndani ya chama wapo kwa ajili ya kulinda maslahi yao wala si maslahi ya walio nyuma yao," alisema mmoja wa vijana.
  Kauli za vijana kususia baraza hilo, zilithibitika pale Katibu wa Umoja wa Vijana CCM wa Wilaya ya Misenyi, Philbert Ngemella aliposema mbele ya Nnauye kwamba vijana wamesusia baraza hilo kwa madai kwamba serikali iliyoko chini ya CCM haiwajali na imeshindwa kutafuta namna ya kuwawezesha kiuchumi.
  Aidha, wakati wa baraza hilo, mzee Abdul Mwanandege alimtahadharisha Nape awe makini sana ili CCM isifie kwenye mikono yake.

  Alisema CCM ni ya wanachama wote hivyo maamuzi ndani ya chama ni lazima yaende kulingana na matakwa ya wanachama.
  Mwanandege alisema mpasuko ulioko ndani ya CCM kwa sasa unatokana na maamuzi yanayotolewa, ambayo hayaafikiwi na baadhi ya wanachama, na kuongeza kuwa, ili chama kiendelee kuwa imara kinahitaji umakini zaidi.
  Naye Nape akihutubua baraza hilo la vijana alikiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM, akisema ndani ya chama kuna mamluki, ambao ndio chanzo cha mpasuko.
  "Watu hao tunao ndani ya chama na ndio wanatuvuruga ila tutaendelea kukabiliana nao hata kama chama kitabaki na mtu mmoja, tunataka watu safi wenye mapenzi ya dhati na chama," alisema.
  Nnauye alisema CCM inaendelea na mkakati wake wa kuwaadabisha wale inaowabaini kuchangia mpasuko, na kwamba haitamfumbia macho mtu yeyote atakayeisaliti.
  Aliendelea kusema kuwa, CCM haimbembelezi mwanachama yoyote abaki ndani ya chama.
  "Nasema anayetaka kuhama ahame, hata kama nitabaki peke yangu chama kitaendelea kuwepo, CCM si mali ya matajiri, ni mali ya maskini," alisema Nape kwa kejeli.

  Kauli hiyo ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na wanaCCM wachache walioudhuria baraza hilo, baadhi bila kutaja majina yao, wakisema kwamba Nape anakimaliza chama kwa kauli zake.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  sikio la kufa halisikii dawa
   
 16. Ishina

  Ishina Senior Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, kimekutana na wakatimgumu kwa kuumbuka mbele ya Katibu wa Taifa Itikadi na Uenezi wa chama hicho,Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa baraza la vijana la wilayahiyo lililofanyika Ijumaa. CCM imeumbuka baada ya vijana wake wilayani hapakuonesha msimamo wao ndani ya chama hicho, kwa kususia baraza la vijanalililokuwa limeandaliwa, ambalo katika hali isiyo ya kawaida liliudhuriwana wazee ambao ni pamoja na kina mama, kina baba na watoto.

  Baraza hilo lililofanyika kwenyeviwanja vya Mashujaa vilivyoko eneo la Bunazi yalipo makao makuu ya WilayaMisenyi, vijana wengi wa CCM walisusia baraza hilo kwa madai ya kutokuwa naimani na serikali iliyoko chini ya CCM. Wakati baraza la vijana likiendelea,vijana wengi, hasa ambao ni wakereketwa wa CCM, walionekana wakizurura ovyo,wakipita maeneo ambayo baraza lilikuwa likifanyika huku wengine wakiendelea nashughuli zao za kujipatia kipato.

  Vijana waliozungumza na gazetihili bila kutaja majina yao, waliokutwa maeneo ya Bunazi karibu kabisa na eneolilikokuwa linafanyika baraza, walisema CCM haina mwelekeo, wamechoka nayo kwakuwa kila siku inaendelea kuwatelekeza. Kwa nyakati tofauti, walisema chamahicho kimeshindwa kabisa kulinda maslahi ya vijana badala yake kimekuwakikiwatumia kila siku kufanikisha maslahi yake.“Mimi ni mkereketwa wa CCM,mbunge wa sasa nimeshiriki kumpigia kampeni hadi akapita, wengi walioko ndaniya chama wapo kwa ajili ya kulinda maslahi yao wala si maslahi ya walio nyumayao,” alisema mmoja wa vijana.

  Kauli za vijana kususia barazahilo, zilithibitika pale Katibu wa Umoja wa Vijana CCM wa Wilaya ya Misenyi,Philbert Ngemella aliposema mbele ya Nnauye kwamba vijana wamesusia baraza hilokwa madai kwamba serikali iliyoko chini ya CCM haiwajali na imeshindwa kutafutanamna ya kuwawezesha kiuchumi.

  Aidha, wakati wa baraza hilo, mzee AbdulMwanandege alimtahadharisha Nape awe makini sana ili CCM isifie kwenye mikonoyake. Alisema CCM ni ya wanachama wote hivyo maamuzi ndani ya chama ni lazimayaende kulingana na matakwa ya wanachama. Mwanandege alisema mpasuko uliokondani ya CCM kwa sasa unatokana na maamuzi yanayotolewa,ambayo hayaafikiwi na baadhi ya wanachama, na kuongeza kuwa, ili chamakiendelee kuwa imara kinahitaji umakini zaidi.

  Naye Nape akihutubua baraza hilola vijana alikiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM, akisema ndani ya chama kunamamluki, ambao ndio chanzo cha mpasuko. “Watu hao tunao ndani ya chama na ndiowanatuvuruga ila tutaendelea kukabiliana nao hata kama chama kitabaki na mtummoja, tunataka watu safi wenye mapenzi ya dhati na chama,” alisema. Nnauye alisema CCM inaendelea namkakati wake wa kuwaadabisha wale inaowabaini kuchangia mpasuko, na kwambahaitamfumbia macho mtu yeyote atakayeisaliti.

  Aliendelea kusema kuwa, CCMhaimbembelezi mwanachama yoyote abaki ndani ya chama. “Nasema anayetaka kuhama ahame,hata kama nitabaki peke yangu chama kitaendelea kuwepo, CCM si mali yamatajiri, ni mali ya maskini,” alisema Nape kwa kejeli. Kauli hiyo ya Napeilipokelewa kwa hisia tofauti na wanaCCM wachache walioudhuria baraza hilo,baadhi bila kutaja majina yao, wakisema kwamba Nape anakimaliza chama kwa kaulizake.

  Quoted from 'Tanzania Daima'
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Hahaaaaaaaaaa! Mkuu nimegundua mchina wako hana uwezo wa kugonga.
  Wacha tu nikutafunie kila kitu!

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa, kimekutana na wakati mgumu kwa kuumbuka mbele ya Katibu wa Taifa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa baraza la vijana la wilaya hiyo lililofanyika Ijumaa.
  CCM imeumbuka baada ya vijana wake wilayani hapa kuonesha msimamo wao ndani ya chama hicho, kwa kususia baraza la vijana lililokuwa limeandaliwa, ambalo katika hali isiyo ya kawaida liliudhuriwa na wazee ambao ni pamoja na kina mama, kina baba na watoto.
  Baraza hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa vilivyoko eneo la Bunazi yalipo makao makuu ya Wilaya Misenyi, vijana wengi wa CCM walisusia baraza hilo kwa madai ya kutokuwa na imani na serikali iliyoko chini ya CCM.
  Wakati baraza la vijana likiendelea, vijana wengi, hasa ambao ni wakereketwa wa CCM, walionekana wakizurura ovyo, wakipita maeneo ambayo baraza lilikuwa likifanyika huku wengine wakiendelea na shughuli zao za kujipatia kipato.
  Vijana waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao, waliokutwa maeneo ya Bunazi karibu kabisa na eneo lilikokuwa linafanyika baraza, walisema CCM haina mwelekeo, wamechoka nayo kwa kuwa kila siku inaendelea kuwatelekeza.
  Kwa nyakati tofauti, walisema chama hicho kimeshindwa kabisa kulinda maslahi ya vijana badala yake kimekuwa kikiwatumia kila siku kufanikisha maslahi yake.
  "Mimi ni mkereketwa wa CCM, mbunge wa sasa nimeshiriki kumpigia kampeni hadi akapita, wengi walioko ndani ya chama wapo kwa ajili ya kulinda maslahi yao wala si maslahi ya walio nyuma yao," alisema mmoja wa vijana.
  Kauli za vijana kususia baraza hilo, zilithibitika pale Katibu wa Umoja wa Vijana CCM wa Wilaya ya Misenyi, Philbert Ngemella aliposema mbele ya Nnauye kwamba vijana wamesusia baraza hilo kwa madai kwamba serikali iliyoko chini ya CCM haiwajali na imeshindwa kutafuta namna ya kuwawezesha kiuchumi.
  Aidha, wakati wa baraza hilo, mzee Abdul Mwanandege alimtahadharisha Nape awe makini sana ili CCM isifie kwenye mikono yake.
  Alisema CCM ni ya wanachama wote hivyo maamuzi ndani ya chama ni lazima yaende kulingana na matakwa ya wanachama.
  Mwanandege alisema mpasuko ulioko ndani ya CCM kwa sasa unatokana na maamuzi yanayotolewa, ambayo hayaafikiwi na baadhi ya wanachama, na kuongeza kuwa, ili chama kiendelee kuwa imara kinahitaji umakini zaidi.
  Naye Nape akihutubua baraza hilo la vijana alikiri mpasuko mkubwa ndani ya CCM, akisema ndani ya chama kuna mamluki, ambao ndio chanzo cha mpasuko.
  "Watu hao tunao ndani ya chama na ndio wanatuvuruga ila tutaendelea kukabiliana nao hata kama chama kitabaki na mtu mmoja, tunataka watu safi wenye mapenzi ya dhati na chama," alisema.
  Nnauye alisema CCM inaendelea na mkakati wake wa kuwaadabisha wale inaowabaini kuchangia mpasuko, na kwamba haitamfumbia macho mtu yeyote atakayeisaliti.
  Aliendelea kusema kuwa, CCM haimbembelezi mwanachama yoyote abaki ndani ya chama.
  "Nasema anayetaka kuhama ahame, hata kama nitabaki peke yangu chama kitaendelea kuwepo, CCM si mali ya matajiri, ni mali ya maskini," alisema Nape kwa kejeli.
  Kauli hiyo ya Nape ilipokelewa kwa hisia tofauti na wanaCCM wachache walioudhuria baraza hilo, baadhi bila kutaja majina yao, wakisema kwamba Nape anakimaliza chama kwa kauli zake.
   
 18. E

  ESAM JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mbona jamaa kaweka link ya habari nzima hapo, mimi nimeisoma yote. Na siku ile ITV waliripoti upande mmoja wa kuonesha mambo shwari kumbuka haikuwa kihivyo, lol....
   
 19. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]
   
Loading...