Vijana amkeni, nchi imo mikononi mwenu mkipenda!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana amkeni, nchi imo mikononi mwenu mkipenda!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omokora Nyangi, Oct 23, 2012.

 1. O

  Omokora Nyangi Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekuwa natafakari kwa muda mrefu huku nikitathimini mwenendo wa siasa na uchumi wetu wa Tanzania. Tafakari yangu imenizamisha na kunirejesha katika historia mana bila kufahamu historia hatuwezi kujua tuendapo. Mustakabali wa nchi yetu nimebaini unategemea vijana. Nimejaribu kupima uwezo wa watawala wetu wa sasa ambao walibahatika kuwa viongozi kuanzia awamu ya kwanza au ya pili, hawa sasa ni wazee ambao ukiwatathimini utendaji wao wa sasa na uwezo wao wa kufikiri, utabaini kwa kadili mtu anapofikia umri wa miaka 55 na kuendelea, ndipo kiwango chake cha kufikiri, kuamua na kutenda vinapo zidi kudorora. Hebu tizama listi hii:
  1. John Malechela
  2. Pius Msekwa
  3. Benjamin Mkapa
  4. Stephen Wasira
  5. Getrude Mongela Nk, nk......
  6. Samuel Sita
  Hawa ni baadhi tu, ambao naamini katika ujana wao walikuwa makini na watendaji wazuri lakini baadaye walidorora kifikra na kiutendaji kwa sababu ya uzee. Hali hii ndiyo wanafilosofia huamini upo ulazima wa kung'atuka mwenyewe kwanza ktk utendaji na hatmaye katika fani ya kufikiri.

  Ukijaribu kutizama hoja hii kwa upana; Angalia mabingwa wengi wa sayansi, uchumi na masuala ya kijamii utaona wengi wao walifanikiwa au walitoa mchango mkubwa sana katika ujana wao kuliko katika uzee wao.

  Kwa mantiki hii, naamini maisha ya sasa ya watanzania, yawe mazuri au mabayayamefikishwa hapa yalipo na sisi vijana ama kwa kushindwa kutambua ukweli huu mapema au kwa kupuuza na kuendelea kubweteka tukidhani wazee ndio wameshikiria mustakabali wa nchi yetu nzuri ya Tanzania. KARIBUNI KWENYE MADA HII!
   
 2. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Suala si umri japo nao una nafasi yake lakini ukweli ni kwamba wamejisahau na wamebweteka.
   
 3. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani umri wa mtu pamoja na umri wa kutumikia kazi unachangia sana.Na kingine kuwekana wenyewe kwa wenyewe ama kumrithisha mtoto na kuendelea na mfumo uleule wa baba yake au mjomba wake pia unachangia kuto piga hatua.Ni vizuri nguvu na akili mpya ikaingia na kutumia mfumo tofauti kutokana na nyakati tofauti.
   
 4. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nadhani baada ya umri kinachofanya uchumi wetu kuwa mbaya ni ubinafsi ambao unachukua nafasi kubwa zaidi.Na hii inafanya mpaka viongozi kutofuatilia ishu za corruption zinapovuja na hatimae unakuta watu wanakuwa mamilionea kwa wizi na hafanywi chochote ila anahamishiwa kwingine na huko anaendeleza mashambulizi.
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa tufanye nini ikiwa wenyewe wamebana kila kona wanang'ang'ania posts nyeti hata kama wamechoka na wanarithishana na vizazi vyao? Waweza kuwa na nguvu,uwezo na nia ya kufanya uyasemayo lakini system haikupi nafasi.
   
Loading...