Vijana 7 Wachadema wanaofanya vizuri nje ya Bunge.... hawa hapa

unapenda ugomvi mkuu.yani unamaanisha wanauwezo mkubwa wa kupika majungu?

Nadhani umetumia fasihi kufikisha ujumbe kwa wapika majungu walioumbuka ziara ya Dr Slaa Kigoma ambao ni sixgate,taswira na nyakarungu! aibu kwao na yale magazeti ya kufungia vitumbua DIRA,UHURU,MZALENDO,RAI kwa vijipropaganda vyao vya kitoto! walisahau kuwa ngoma ya watoto huwa haikeshi? Chezea CDM weye! teh... teh teh teh teh...
 
Umemwacha dada anaitwa Jesca Kishoa, huyu dada kiboko ya Mwigulu.
 
duuuh yaani hiyo ndio top ten bora? kwsha habari yenu woooote hao pumba tupu labda huyo Golugwa na Bashe wengine woote pumba pumba
 
Ongeza Ben xa 8; Pia nashauri namba 1 na 2 wahold position moja moja ili kuonesha dhana ya mgawanyo wa mamlaka..! Hatutaki injinia Manyanya staili.
 
huyo mtu hapo juu (jina no. 2) kwenye red kazi zake hizi hapa
[h=1]AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUNGUA VIBAYA MJINI IGUNGA[/h]by JOHN BUKUKU on SEPTEMBER 10, 2011 in SIASA with NO COMMENTS
MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCMKumekuwepo na kushutumiana kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kutokana na matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea, hasa katika kipindi hiki cha Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa Mbunge wa jimbo la Igunga, kufuatia kujiuzulu kwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo Bw. Rostam Azizi
Vyombo vya usalama na ulinzi vinatakiwa kuwa katika hali ya tahadhari na umakini mkubwa kwa muda wote wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo, ili kudhibiti vitendo kama hivyo vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani na utulivu katika kipindi hiki cha kampeni jimboni humo.

MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika , ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kupandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCM
Anayemtazama ni Daktari wa hospitali hiyo, Selemani Masinga. (Na Mpigapicha Wetu)

naapa, duniani tunafanya siasa ila kiama ndiyo mtagundua hii ni kazi ya shetani savimbi wa hapoo singida. Kazi ya shetani ni kuua na kuharibu. Savimbi
 
Naona kwa maoni ya wengi vijana wangu wanakubalika, nitaendelea kuwaletea wabunge waliyofanya vizuri 2013... Najua huko ndipo kwenye kasheshe...
 
john heche amezungukwa vibaya sana na CCM na jopo lake ndani ya wilaya yake ya tarime kwa misimamo yake mara aitwe kibaraka wa wachaga
CHADEMA MUWE MACHO
 
Ni haki yao Wapo akina malisa godlisen, John mnyika, godbles Lema, lisu, na mm piank hao ni wachache
 
Hawa ndiyo vijana wa chadema wanaofanya vizuri nje ya Bunge na wakati mwingine wamekuwa msaada mkubwa kuliko baadhi ya wabunge wa CDM.

1. Amani Golugwa
Kamanda huyu kwasasa ndiyo katibu wa kanda ya kaskazini ni mtu mpole sana na mwenye ushawishi wa aina yake pale anapopewa nafasi ya kuongea jambo Fulani, anakisaidia chama sana kwenye kanda hii ya kaskazini.

Ameiamsha kanda kwa kiwango kikubwa sana, vile vile ni katibu wa mkoa wa Arusha na ameweza kuingiza wabunge wengi bungeni pamoja na madiwani wa kutosha na sasa tunaona eneo la Arusha lilivyomsaada kwa ukombozi wa nchi yetu.

2. Henry Kilewo
Huyu ni kamanda wa chadema kanda maalum ya Dar es salaam akiwa anatokea mkoa wa kinondoni kichama( Katibu wa chadema mkoa wa kinondoni na kanda maalum ya Dar es salaa) vile vile aliwahi kuwa Mratibu wa Muda wa Kanda ya pwani.

Ni kijana jasiri sana tofauti na muonekano wake, ni mtu anayejishusha sana na mwenye kuangalia maslahi ya chama chake kwanza na kulinda sifa ya chama mahala popote pale, kwasasa amejipambanua kuwa Mgombea Ubunge Mwanga 2015 kama chama chake kitampitisha.

3. Ally Bananga
Ni kijana aliyeibuka kutokea upande wa pili wa kisiasa yaani chama cha mapinduzi, kiukweli ameonyesha kipaji chake ambacho nadhani ccm ilikuwa inakimaliza taratibu bila yeye kujua na alipokuja kujua akaona njia pekee ya kuendelea kuwepo kwenye siasa ni chadema na sip engine, Ameonyesha dhamira yake hiyo ya dhati na kwasasa ukimsikia Bananga ni Bananga kweli kweli.

3. Ibra Bashe
Ana nafasi ya kufanya vizuri kwenye siasa za chadema kama ataamua kuwa muwazi na kuingi front kupambana, uwezo wake siyo wa kutiliwa mashaka hata kidogo ni mtu anayejua anatakiwa kufanya kitu gani kwa wakati gani na ni kijana mtaratibu sana na mwenye kuhoji.

4. John Heche
Huyu ni M/kiti wa Taifa wa vijana chadema (Bavicha) Ni mtu asiyeogopa awapo jukwaani ni mtu mwenye msimamo ni mtu asiyeburuzwa ni mtu mwenye maamuzi na kwasasa ndiye mgombea pekee anaye aminiwa kurudisha jimbo la Tarime mi kononi mwa Chadema 2015.

5. Mohamed Mtoi
Ni kijana asiyetambulika sana kwenye majukwaa ya kisiasa ila ni kijana ambaye yupo makini sana kwenye shughuli za chama kwasasa yupo idara ya Kanda ndani ya Makao makuu ya Chama, Siku akipewa fursa ya kuongea na watanzania huenda tukalithibitisha hili bila wasi wasi wowote.

6. James Millya
Nadhani huyu alikuwa kada wa ccm na sasa amekuwa msaada mkubwa sana wa chadema upande wa umasaini na hata kutishia kutokurudi kwa mbunge wa sasa Bungeni 2015, Ni kijana aliyejipambanua na kuwa muwazi katika siasa zake siku za hivi karibuni akiwa upinzani.

7. Mawazo
Kamanda huyu alikuwa Diwani wa kata ya sombetini kwa tiketi ya ccm akaamua kuvua gamba na kuvaa gwanda, bila kusita kamanda mawazo ameweza kuinyanyua kanda ya ziwa na kwasasa ndiyo ICON ya wasukuma, Kamanda anapiga mzigo sijawahi kuona ni noma huyu jamaa.
Hawa ndiyo makamanda wangu ninao waona wapo mstari wa mbele kila kukicha wakishirikiana na makamanda wengine kulikomboa Taifa letu nje ya bunge.
Ombi langu kwa viongozi.
Tunajua tunamakamanda wengi makamanda hawa kwasasa inapaswa makae nao chini muendelee kuwasuka kwani chadema ni chuo cha mafunzo, wapeni nafasi waonyeshe vipaji vyao.
Naamini chaka kama kitaweza kuitumia hiyo list hapo juu vizuri na kuongeza wengine wengi ambao wapo ninauhakika ccm inaweza kupotea hata kabla ya 2015.

Kwa yoyote yule anaweza kuongeza wengine anaowafahamu ...

Good analysis nimekosa pa ku like
 
Back
Top Bottom