Tatizo kiongozi vijana huo ujasiri hawana. Wanafikiria tu vitu vyepesivyepesi. Huwezikuwa unawaza vizuri ukahudhuria usaili wa shortlisted watu 11,000 wakati nafasi zinatakiwa 20. Mtawamaliza mitume na manabii,mtakula sana asali na maji ya upako lakini bado ngoma itaendelea kuwa ngumu. Fanya maamuzi magumu anza na vimiradi vidogovidogo mtatoboa. Hata Mungu alianza kumuumba mtu mmoja la dunia ina mabilioni ya watu.Tunahitaji kujengeana ujasiri kuwa maisha yanaweza endelea kuliko kusindikiza Mwenge kwenye chambers za UDOM!