Vijana 5000 waathirika na utumiaji wa dawa za kulevya Tanga

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
unga.jpg

Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin na Cocain katika jiji la Tanga imeongezeka kutoka zaidi ya 3000 hadi kufikia 5000 katika kipindi cha miaka 2 iliyopita kufuatia utafiti uliofanywa na kubaini kuwa kila baada ya nyumba nne hadi tano zimeanzishwa maskani za kuuza dawa za kulevya.

Wakizungumza na ITV mara baada ya maadhimisho ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya nchini ambayo kimkoa yamefanyika katika kituo cha afya cha Ngamiani,mratibu wa afya ya akili katika Halmashauri ya jijii la Tanga George Semsela pamoja na meneja wa kitengo cha kuwatibu watumiaji wa dawa za kulevya Salum Amon wamesema walioathirika zaidi ni vijana wa kuanzia miaka 14 ambao baadhi yao ni wanafunzi hadi 45.

Baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya wenye umri wa kuanzia miaka 14 hadi 15 ambao wanatayarishwa kupelekwa kitengo cha nyumba ya kudhibiti dawa za kulevya baada ya baadhi yao kuathirika na afya ya akili wakiwemo wasichana wadogo wakielezea athari za dawa hizo wameionya jamii kuachana na matumizi hayo kwa sababu ukikosa unakuwa kama mgonjwa.

Kufuatia hatua hiyo,naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga Mohamed Haniu amesema wametoa mwongozo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kutoa taarifa mara wanapohisi mtu anasambaza na kuuza dawa za kulevya ili na wao waweze kufanya mchakato katika vyombo vya sheria.

Source: ITV
 
Ngada ni tatizo Tanzania nzima.tuungane kuyapiga vita madawa ya kulevya.
 
Ngada ni tatizo Tanzania nzima.tuungane kuyapiga vita madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom