Vijana 11 Wakitanzania ‘waliobaka’ Mahakama ya Afrika kusini imewaachia huru

maforce

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
660
615
SA1.jpg

Leo May 30, 2018 Vijana 11 raia wa Tanzania wanaoishi Johannesburg nchini Afrika Kusini, walioshtakiwa kwa kosa la ubakaji wameachiliwa huru na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Johannesburg.

Vijana hao wameachiliwa huru na Jaji Metisie kwa kukosekana kwa ushahidi kutoka upande wa mashtaka.

Wakili wa upande wa Mashtaka wa Jamhuri alimfahamisha Hakimu kuwa Thelma Mondowa aliamua kurejea kwao Zimbabwe na wameshindwa kupata anwani yake.

Vijana hao walishtakiwa mwaka 2015 kwa makosa ya kumteka na kumbaka mwanamke mjamzito, Thelma Mondowa raia wa Zimbabwe.

Inaelezwa kuwa Mwanamke huyo alipokuwa akitoka kazini na mfanyakazi mwenzake wa kiume ghafla walivamiwa na kundi la wanaume wenye silaha na wakamvuta mwanamke huyo kabla ya kumpiga mfanyakazi mwenzake ambae baadaye alifanikiwa kutoroka.
source: millard ayo
 
Back
Top Bottom