Vijana 10 wajasiriamali tuungane kwa kuunda kikundi kimoja cha uzalishaji

Digital base

Senior Member
Jul 19, 2020
126
189
Habari ya leo wakuu,

Nna wazo moja ambalo tunaweza kushirikiana vijana 10 WAJASIRIAMALI tunaojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia ni muhimu tusajili kikundi chetu ili kiweze kutambulika na bidhaa zetu tunazozalisha zitambulike.

Lengo la kuungana
1.Kushughulikia vibali vyote vinavyotakiwa tukiwa kama kikundi.
2. A.Kuchangia mtaji sawa kila mmoja ili kufanya uzalishaji wa kutosha na usawa wa mgawanyo wa faida.

B.Kununua malighafi nyingi kwa bei ya jumla kisha kutunza store.
3.Kutengeneza mfumo mzuri wa kumbukumbu na mauzo ya bidhaa zote tutazo zalisha.
4.Kutafuta masoko ya kudumu ya bidhaa zote tutazo zalisha
5.A.Kukodi eneo tutakalo tumia kuzalisha bidhaa zetu.

B.Kununua eneo kwa ajiri ya uzalishaji wa bidhaa zote za kikundi
6.Kuchangia kikundi kila wiki au mwezi kiasi cha fedha ili kuimarisha mtaji wa kikundi.

7.Kuboresha wazo la kila mmoja aliye tayari kukua kiuchumi kupitia kikundi.
8.A.Kutengeneza utaratibu na mfumo wa uongozi utakao wezesha kuendeleza kikundi

B.Kutafuta msimamizi na mtaalamu wa biashara na uendelezaji wa miradi
C.Kutafuta mtaalamu wa masuala ya fedha na kumbukumbu ya mapato na matumizi kwa kufuata dira ya bajeti itakayo wekwa.

D.Kutafuta mwanasheria atakaye simamia mambo yote ya kikundi yahusuyo sheria.

9.Kuendesha mfumo wa mchango kila wiki kwa kiwango tutakacho kubaliana ili kuwezeshana kiuchumi.

Hapo ina maana kila wiki mtu ana chukua pesa huku akijiandaa wiki ijayo kutoa pesa kwa ajiri ya mwenzake.

10.Kutengeneza team za mauzo ya bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na malengo ya kila siku ili kukuza uchumi wa kikundi na mtu mmoja mmoja.

SIFA ZA KUWA MWANA KIKUNDI
1.Uwe unajihusisha na ujasiriamali wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali
2.Uwe na mtaji wa kianzio utakao wezesha kikundi kisajiliwe na kuanza uzalishaji mapema.

3.Usiwe mbinafsi
Kutaka kuendesha mambo yako makubwa pembeni na kwenye kikundi ushiriki wako ni mdogo,hilo hapana tuna ungana ili tufanye kazi kwa pamoja maana umesha fanya mwenyewe umeona matokeo yake hapa unaye kuja tunafanya kwa pamoja.

4.Uwe mchakalikaji usi subiri wenzako wafanye kisha wewe uje uangalie faida iliyo patikana hata kama tuna team za mauzo nawewe ufanye kazi kwa sehemu yako hiyo inaondoa mwili kuzoea uvivu.

5.Usiwe ni mtu wa visingizio kila siku.
Lazima uwe ni mtu uliye badirika kifrika (Entrepreneurship Mindset) usije kwenye kikundi kama mtu anaye fanya part-time (kujaribu) hiyo itasaidia kuondoa lawama.
Kwa uliye tayari na unahisi unaweza kuwa miongoni mwa hao 10 karibu tujumuike.

Na hao watao ungana nami ni kwa wakazi wa Dar na Pwani maana mimi niko Dar ni lazima tuwe karibu ili kuondoa lawama na migongano ya fedha

Ikiwa uko mbali tafuta wenzako 9 hapo ulipo then muendeleze huo mfumo mkiwa karibu mkoa husika.

Mawasiliano yangu ni 0748062691 pia iko WhatsApp.Karibuni sana tuinuane kiuchumi kwa pamoja tuijenge Tanzania.

Nime waza hivi maana uki tafuta business partners wenye mitaji wana fikiria faida tu katika wazo lako bora tukawa wote tulio pitia changamoto hiyo itasaidia hata tukikwama tuna jua solution.
 
Ni wazo zuri sana BUT sioni mantiki ya kuweka boundaries kuwa ni Dsm na Pwani kwa minajili ya hoja uliyotoa.

Tunaishi kwenye ulimwengu wa TEHAMA hebu tuvuke mipaka ili mwenye nia njema mahali popote pale ashiriki kwenye fursa hii bila kujali wa rangi gani au anatoka mkoa gani ilimradi uwekwe mfumo ambao kila mmoja atajisikia ni sehemu ya kikundi.

Hilo mimi sijaona kama ni tatizo bali ni changamoto tu ambayo inaweza kutatuliwa vizuri tu bila shida !
 
Back
Top Bottom