Vigogo wenye uraia wa nchi mbili ni hawa wafuatao

uraia nchi mbili ulisharuhusiwa wewe!
uwe unafanya utafiti kabla ya kukurupuka kuandika, katiba yetu pamoja na ubovu wake lakini bado inatambua uraia wa nchi moja tu, hivo hao walio na urai wa nchi mbili wanatakiwa wapelekwe mahakani haraka kama kuna ushahidi wa kutosha.
 
Asili haipotei, haya mambo ya Uraia sijui nini ni katika kuendeleza tu mikakati ya "devide and rule". Hao Waheshimiwa wenyewe unasikia hapo wana Uraia wa nje.
Hata JK? au hawa waliotajwa tu............na wewe.
:nerd:
 
Kha...hizi habari mtu anaamka na kuandika ndoto zake. Weka basi passport number hapa, nk. Sio unaandika tu kama kichaa
 
Kama ni kweli wana uraia wa hizo nchi nyingine,basi ni lazima waukane uraia wa Tanzania kwasababu bado hatutambui uraia wa nchi mbili.(unless sheria iwe imepitishwa)

Hao wa USA inawezekana wana green card,na hivyo wanachotakiwa tu ni kufanya safari ya marekani at least once in a year and thew will be fine, wenye green card hawaruhusiwi kuishi nje ya marekani kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kurudi kwanza marekani...na ndiyo maana ansema inabidi wafanye safari ya marekani at least mara moja kwa mwaka..However, hilo haliwezi kuwaondolea uraia wa Tanzania.

Watanzania wenzangu wengi tunaendekeza majungu badala ya ukweli na hali halisi. habari hii haina miguu wala macho ya kuangalia iendako. Angetuletea hapa ushahidi wa uraia wa nchi mbili kwa aliowataja ningekuwa mmojawapo wa kuchangia mengi zaidi, lakini hii inaonyesha ni yale yale ya vijiweni.

Wengi wetu wanashindwa kutofautisha kati ya permanent resident na naturalized citizenship. Permanent resident sheria zake zinatofautiana kati ya nchi na nchi. Mfano kama JMushi1 alivyotolea mfano wa Marekani, permanent resident status imezoeleka kwa jina la green card kutokana na historia ya gamba walilokuwa wanapata hapo awali lilikuwa la rangi ya kijani lakini siku hizi gamba hilo limekuwa electroniced. Na mwenye status ya green card anatakiwa asikae nje ya Marekani zaidi ya miezi sita bila sababu muhimu ambayo ruhusa inatakiwa itolewe na homeland security au ubalozi wa marekani nchini aliko mwenye status, vinginevyo hataruhusiwa kuingia tena.

Tunachohitaji ni uthibitisho, lakini hii la kujadili vijiweni na kulileta hapa tunapunguza hadhi ya mtandao wetu wa Jamii Forums.
 
Laurance Masha nae ana urai wa USA na TZ. Baada ya kushindwa Ubunge wa Nyamagana last year muda wake mwingi yupo USA. Yeye TZ anaipenda tu ikimpa Ubunge na Uwaziri.
 
Wana Jf
katika kufatilia baadhi ya mambo nimepata kufahamu yafuatayo
(1)Mh sugu Ana uraia wa Tz na USA
(2)Mh Membe Ana urai wa Tz na Canada
(3)Mh Letecia Nyerere Ana uraia wa Tz na USA
(4)Mh Nyalandu Ana uarai wa Tz na USA

wana Jf Uchunguzi unaendelea Kama mnataatifa zaidi mnaweza kutoa Kama mnawafahamu wengine ongezea list
Nchi yenyewe aieleweki kama watu wana ID zaidi ya moja unashangaa watu kuwa na uraia wa nchi mbili!!hata wewe mwenyew una account ngapi??yahoo,gmail.hotmail,facebook,jf vyote vya nini??account moja haikutoshi??au haramia wa mitandao??ukijibu maswali haya kwa hoja mimi nitashangaa kwa nini watu wanakuwa na uraia zaidi!!
 
My take: Uraia wa nchi mbili upitishwe kisheria,na pia ISIWE lazima kwa mwanamke pekee awe na uwezo kisheria wa kumfuata mumewe aliyehamishiwa mkoa mwingine kikazi,BALI hata mume aruhusiwe kumfuata mkewe! Yaani vice versa iwe true!
 
Haki ya kwanza kabisa inayomtambulisha mtu kuwa raia ni uwezo wa kupiga kura. Bila kuwa na huo uwezo wa kupiga kura wewe sio raia kamili wa nchi husika hata kama una makaratasi. Sasa hapa kwetu nchini Tanzania kuna watu wengi sana ambao ni raia wa nchi jirani lakini wanapiga kura kwenye chaguzi zetu. Tume yetu ya Uchaguzi kwa kushindwa kufanya kazi sawasawa imewawezesha hawa jamaa kupiga kura kwetu kwa kuwapa vitambulisho vya kupiga kura. Na wakienda Immigration watapata passport za Tanzania. Hawa watu ni malaki kwa malaki. Wanaweza wasiwe vigogo lakini hili tatizo kubwa sana Tanzania kuliko hata hii issue ya vigogo. Endapo kutakuwa na uchaguzi wa rais na atakayeshinda kwa kura chache, tuseme elfu kadhaa, tunaweza kabisa kusema Tanzania tumechaguliwa kiongozi wetu na warundi au wamalawi au wasomali. Kazi ya kuwapa watu uraia wa nchi mbili imekuwa ikifanywa kwa muda mrefu hapa Tanzania na TUme ya Uchaguzi!
 
Wana Jf
katika kufatilia baadhi ya mambo nimepata kufahamu yafuatayo
(1)Mh sugu Ana uraia wa Tz na USA
(2)Mh Membe Ana urai wa Tz na Canada
(3)Mh Letecia Nyerere Ana uraia wa Tz na USA
(4)Mh Nyalandu Ana uarai wa Tz na USA

wana Jf Uchunguzi unaendelea Kama mnataatifa zaidi mnaweza kutoa Kama mnawafahamu wengine ongezea list

asa si wapiganie kuwe na uraia wa nchi mbili tu ama?
 
Niuwachie tena, hivi tu niko bongo lakini inabidi ubalozi wanipigie simu kila mwezi kuniuliza kama nnashida yoyote. Niyaachie ma privilege kibao kisa nini? Kwani mie nilienda kucheza kule? Nilienda kutafuta maisha bora ambayo Nyerere alishindwa kunipa, na kweli nimefaidika, nashkuru AlhamduliLlah.

Wengi tu hapa wana uraia wa nchi za nje na si wa Tanzania tu
. Sio kuwa hatuipendi nchi yetu, la hasha, ni maslahi. Hapa kwetu nani atakulipia nyumba, matibabu, mshahara, transport, kama huna kazi? Lakini leo si haba.

Ndio maana akina nanihii hukimbiza wake zao wakajifungulie USA? Halafu wanataka urais?? Tunawasubiri watakapojitokeza tuwaulize maswali magumu. Huku nataka na kule nataka.Chagueni moja.
On a serious note - Kama vigogo waliotajwa hapa wana "uraia" wa nchi mbili, achilia mbali green card, halafu wakaja kupewa ubunge na uwaziri basi Tanzania ina matatizo makubwa zaidi.Watunga sheria (wabunge) wanaposhiriki uvunjaji sheria tumekwisha.
 
Wana Jf
katika kufatilia baadhi ya mambo nimepata kufahamu yafuatayo
(1)Mh sugu Ana uraia wa Tz na USA
(2)Mh Membe Ana urai wa Tz na Canada
(3)Mh Letecia Nyerere Ana uraia wa Tz na USA
(4)Mh Nyalandu Ana uarai wa Tz na USA

wana Jf Uchunguzi unaendelea Kama mnataatifa zaidi mnaweza kutoa Kama mnawafahamu wengine ongezea list

Source?
 
Swali la Msingi? Je mjiulize ni kwa nini USA na Canada wanaruhusu uraia wa nchi mbili??. Je ni kwanini waruhusu uraia wa watu waliotoka kwenye nchi masikini kama Tanzania wakati USA tayari kuna watu million 300?. Sisi Tanzania na fikra za kimasikini na kishamba tunataka kufukuza wazawa wa Kitanzania kwa kuchukua uraia!!!! . Tanzania tunajiuliza kila siku je ni kwanini USA na Canada ni matajiri na majibu yako machoni kwetu! ni fikra za kimaskini na sheria za kikoloni!

Ghana, Nigeria, Togo n.k wana uraia wa nchi mbili wameona mbali
Nani kakwambia USA inaruhusu uraia wa nchi mbili? Ukiupata wa USA inabidi uukane ule wa awali. Chanzo cha umasikini wetu labda ni kukosa umakini kama huo wa kwako.
 
Back
Top Bottom