Vigogo watupiana mpira kuhusu vijisenti vya chenge!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo watupiana mpira kuhusu vijisenti vya chenge!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by malkiory, Jul 26, 2011.

 1. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kuona viongozi wetu tuliowaamini na kuwaweka madarakani wanashindwa kutumia madaraka na mamlaka waliyopewa kuongoza, inasikitisha kuona kuwa hawapo tayari kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na hatimae kwa wananchi pale wanapohojiwa juu ya swala fulani.
  Siku hadi siku tunashuhudia viongozi wetu wakiwa na kigugumizi kwa kile wanachoona wao kuwa ni utata, wakati sivyondivyo.
  Inasikitisha kuona kuwa wanajaribu kuutengeneza utata wa swala husika ili ku justify their reluctancy and indisposition in addressing the matter. Tumeona hilo kutoka kwa viongozi wengi akiwamo Waziri Mkuu, sasa tunashuhudia kutoka kwa watendaji wengine wa chini, hii imekuwa ‘culture' katika taasisi zetu, wanataka kutuaminisha kuwa this is the way of doing things.

  Hatukubaliani na hili tunataka wabadilike kwa kuwa wawazi katika maswala ya msingi, maswala yanayofahamika waziwazi. Ni lazima waelewe kuwa hakuna ‘conflicting roles and responsibilities' pale kiongozi anapokuwa wazi juu ya swala fulani hata kama haliihusu Wizara yake mojakwamoja, conflicting roles and responsibility haitokei kwa kuelezea kinachofahamika, au unachokifahamu bali itatokea pale unapohukumu wakati wewe hupaswi kuhukumu, pale unapowajibisha wakati huna mamlaka ya kuwajibisha, pale unapotoa uamuzi wakati huna madaraka hayo n.k (hata hivyo ieleweke hata kama huna mamlaka na madaraka unaweza kupendekeza kwenye chombo husika). Watanzania tuwe wazalendo kuliko kuwa wanafiki katika maswala yanayohusu ustawi wan chi yetu.

  Walichofanya Chikawe, Celina Kombani na Werema hakikubaliki (Angalau Membe kidogo amejibu ingawaje was not good enough, "kwamba wote waliohusika na rada hiyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria huku akisisitiza kwamba, mamlaka husika zitafanya hilo muda ukifika.)
  Viongozi hawa sio kwamba hawafahamu wanachopaswa kufanya bali ni ubabe, ujeuri na kulewa madaraka vimewatawala. Viongozi wetu wanajifanya hawafahamu ni nini wanapaswa kufanya, nini wanapaswa kufahamu, nini maana ya kuingilia madaraka, na ni mambo gani wanapaswa kuyazungumzia hata kama swala husika halipo kwenye Idara/Wizara zao.

  Walichokifanya hawa watatu ni upuuzi na kukwepa kuwajibika. Tumeambiwa na mheshimiwa Membe kuwa jukumu la kuwabaini watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria lipo chini ya ofisi ya Rais Utawala Bora na Sheria na Katiba. Chakushangaza hao wenye dhamana (Chikawe) amejibu kwa dharau kwamba "Sina la kujibu" anawezaje kusema hana la kusema wakati yeye ni muhusika na ni mmoja ya wanaoshughulikia swala hili? Ukwepaji majukumu anaoufanya ni kutowatendea haki wananchi kupitia vyombo vya habari ili kufahamu mustakabali wa mambo ya msingi ya nchi yao.

  Chikawe na wenzake wanapaswa kuelewa wananchi tunahaki ya kuuliza na kupewa taharifa juu ya hili (freedom of information).
  Inasikitisha mheshimiwa Chikawe anayeongoza ofisi inayoshughulikia utawala wa sheria (rule of law) anashindwa kutekeleza matakwa ya sheria. Tunategemea viongozi wetu kuwa custodians wa rule of law, cha kushangaza ni kinyume chake kwani wamekuwa watu wanao violate taratibu, kanuni na sheria., they let conflict unresolved because they afraid to address it.
  Pengine wanashindwa kuwa wazi kwa kuwa hawajiamini kwa nafasi walizopewa, kwani wengi wamepewa kwa upendeleo (nepotism), wanaogopa kutoa tamko au kutoa uamuzi kuhofia bwana mkubwa aliowaweka huenda asipendezwe na walichokisema au walichoamua. Haya ni mapungufu makubwa katika uongozi wa nchi yetu.

  Tunawaagiza viongozi wetu wawe wawazi, wakweli, wawajibikaji na wawajibishaji. Tunawataka wasitoe visingizio kuwa hawawezi kuzungumzia jambo kwa kutoa visingizio kuwa wapo safarini, hata kama wanachotakiwa kuzungumzia sio jambo jipya bali ni jambo la muda mrefu linalofahamika. Tunawataka waache ubabe na dharau kwa kuzima simu, kufanya hivyo ni kupingana na sheria ya uhuru wa kutafuta habarri na kutoa habari, ni kukwepa kuwajibika kwa wananchi waliowaajiri.

  Tanzania tumekuwa wagezaji karibu kwa kila kitu kutoka nchi za Dunia ya 3, kwa nini Viongozi wetu wasijifunze na kuiga jinsi viongozi wenzao wanavyokuwa wazi kwa kutokimbia majukumu yao na kuelezea public kwa kila issue inayotokea. Kwa kufanya haya tutaweza kufikia Tanzania tunayoihitaji.

  Mungu ibariki Tanzania.

  Benedict Kimbache
  Mobile: +447903294496
  land-line: +44(0)2030914226 OR +44(0)2085918077
  Skype name: kimbache1
   
Loading...