Vigogo watupiana mpira kuhusu ‘vijisenti’ vya Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo watupiana mpira kuhusu ‘vijisenti’ vya Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 26, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Vigogo watupiana mpira kuhusu ‘vijisenti' vya Chenge
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 25 July 2011 21:07
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwandishi Wetu
  JALADA la tuhuma za kumiliki dola 1 milioni za Marekani (sawa na Sh 1.5 bilioni za sasa) zenye utata zinazomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, limezidi kugonganisha vigogo serikalini wakiwamo mawaziri, ambao kila mmoja ametua zigo kwa mwenzake.

  Chenge alikutwa na kiasi hicho cha fedha mwaka 2008 katika Kisiwa cha Jersey, baada ya uchunguzi wa kashfa ya rada kati ya Serikali na Kampuni ya BAE Systems, uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO).

  Hata hivyo, hadi sasa kumekuwa na kutupiana mpira miongoni mwa vigogo wa Serikali wakiwamo mawaziri ambao Bernard Membe wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alisema jukumu hilo liko chini ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na Sheria na Katiba.

  Wakati mawaziri hao wakirushiana mpira, tayari Mkurugenzi Mkuu, Dk Edward Hoseah aliuambia umma kwamba amekamilisha uchunguzi wa vijisenti hivyo na kukabidhi jalada kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliazer Feleshi kwa taratibu zaidi za kisheria, lakini mkuu huyo wa mashtaka alikana kupokea jalada bila hata kuangalia masjala.

  Msimamo wa Membe
  Akizungumzia hilo, Membe alisema kazi kubwa ya wizara yake ilikuwa ni kuhakikisha fedha za BAE Systems zinarejeshwa nchini na kuwekwa katika akaunti maalumu ndani ya Benki Kuu (BoT).

  Membe alifafanua kwamba, jukumu la kuwabaini watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria lilikuwa chini ya Ofisi ya Rais (Utawala bora) na ile ya sheria na katiba, lakini akiweka bayana kwamba, "watuhumiwa wa rada wapo."

  "Ingawa siwezi kuwataja kwakuwa siyo mamlaka yangu, lakini watuhumiwa wa rada wapo na naamini mbele ya safari mamlaka husika zitawashughulikia tu. Kwa hiyo jukumu la kuwataja siyo langu," alisema Membe wakati alipotakiwa kutaja watuhimiwa bungeni.

  Membe alifafanua kwamba, wote waliohusika na rada hiyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria huku akisisitiza kwamba, mamlaka husika zitafanya hilo muda ukifika.

  Kauli ya Chikawe
  Waziri Mathiasi Chikawe mwenye dhamana ya utawala bora, alipoulizwa kuhusu msimamo wa Serikali baada ya DPP kukana hadharani kutokuwa na jalada la Chenge kutoka Takukuru kama ilivyoelewa na Dk Hoseah, alikwepa zigo na kujibu, "sina cha kusema."

  Chikawe hata alipoulizwa haoni kwamba kuna tatizo katika utendaji kazi wa ofisi ya DPP kutokana na tuhuma za kukalia majalada mengi ya ufisadi kama ambavyo imekuwa ikilalamikiwa na Takukuru, alijibu kwa msisitizo, "sina cha kusema," kisha akaakata simu.

  Kauli ya Kombani
  Alipoulizwa waziri mwenye dhamana ya Sheria na Katiba, Celina Kombani, alijitetea kwamba kwa wiki nzima hakuwa nchini, bali alikuwa Afrika Kusini hivyo, hajui lolote.

  Kombani alijitetea zaidi akisema licha ya kwamba hayupo, wizara yake ina wanasheria akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akashauri aulizwe yeye huenda akawa anajua.

  Lakini, alipoulizwa maoni yake akiwa Waziri wa Sheria na Katiba kwa mtumishi wa umma anaposikika amehifadhi Sh1.2bilioni katika akaunti moja tena nje ya nchi, alijibu, "mimi sijui nimekwambia nilikuwa safarini, " kisha naye akakata simu.

  Kauli ya AG Werema
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, alipoulizwa kuhusu hatma ya jalada hilo, alijibu, "mimi ndiyo nimetoka safari, hivyo ngoja nifike ofisini kwanza."

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  .....Ama kweli Serikali imeshika "utamu"
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Wanafanana na moto,
  Wacha kucheza na moto x 2,
  Moto ni moto, huunguza.

  By Hemed Maneti, pamoja na Vijana Jazz Band (Wanapambamoto, awamu ya pili)
   
 4. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  vidumu vyombo huru vya habari...!
   
 5. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ishu ya chenge sio ya leo wala jana..mimi nashindwa kuelewa waziri anapouliuzwa halafu anasema hajui chochote akisingizia alikuwa safarini...ofisi yake pia inaenda safarini? Sasa kama mwanasheria wa serikali anashindwa kujua je mimi raia itakuaje?
   
 6. W

  We know next JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serilikali, kwa kweli mnatutia kinyaaa, tena kinyaa cha kutaka kutapika. Hivi inakuaje Mawaziri wazima mnashindwa kujibu maswali rahisi kama hayo? Je mnajua wajibu wenu nyie kama mawaziri? Kwani taratibu za mtumishi wa umma zimefungiwa magogoni kwa Mzee Luhanjo, kiasi ambacho nyie hamzijui? Haiwezekani mkatoa sababu eti tulikuwa safari, kwani ukiwa safari ndio hujui taratibu na sheria? Jamani, msifanye kazi kwa mazoea tu, kama hamuwezi si mwambieni anayewateua kuwa hamuwezi kazi zenu? Kwa kweli mnatia aibu na kutudhalilisha Watanzania. Kama kila kitu hamjui sasa mnafanya nini humo maofisini????? tumechoka na kuwakinai kabisa. Shame upon you!
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hii serikali watu wote wako safarini kila siku ? Ndiyo maana Nchi inakuwa gizani wao wako nje wanapata mwanga.Wote hao ni Chikawe pekee alikuwa Tanganyika ila wengine wote walikuwa safari duh .
   
 8. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nimetoka safari, subiri nifike kijiweni ndio nitaongelea hii mada,
  kwa sasa nashauri Chenge aendelee kuishi kwa kodi za walalahoi na ulinzi wa serikari asishitakiwe, yeye yuko juu ya sheria na ana hela nyingi.
   
 9. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  baba = mwana
  hakuna viongozi hapo
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ndio nipo njiani natoka safari, sijui chochote. Subirini nikifika ntachangia
   
 11. M

  MRULI Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unataka kujua kuwa hapa hatuna viongozi makini muulize ****** naye atakwambia kuwa alikuwa safarini south a.si unaona hata ishu ya yule katibu wa ngeleja mpaka leo inasubiri atoke safari!!!? Tafadhalini tunaomba mtupishe kama mnaitakia mema nchi yetu ninyi muendelee kutumbua vijisenti vyenu mlivyoficha huko mnakokimbilia kila siku mkituacha gizani......
   
 12. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hivi wananchi hawawezi kutafuta dawa ya hawa wanaojiona miungu watu! Nakumbuka mtaani1 ulikuwa ukisikia: niagieni x 3; niagieni marafiki zangu ...; ujue kuna kibaka kafungwa tairi na kamiminiwa mafuta ya taa na moto unawaka. Vipi hawa wa vijisenti
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Yaani! We acha tu! wanajifanya hawajui lolote utafikiri hii issue ya fisadi Chenge imetokea juzi hivyo hawana details zozote zile kumbe ndio usanii wa Serikali hii wakimuiga yule Boss wao Mawingu ambaye hajui lolote linaloendelea ndani ya nchi.
   
 14. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nasema na nitasema tanzania hatuna viongozi kabisa.watatupiana sana huo mpira mpaka tutasahau
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tehe tehe teh,,,,,,,,,,,,,,,bongo hata waziri anatembea na ofisi kwenye briefcase.......ngoja aifungue atakujibu
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  BOSS mwenyewe hajawahi kumwajibisha yeyote yule hata wale waliovurunda kwa kiwango cha juu kabisa tangu aingie madarakani miaka sita iliyopita. Saa zote anacheka cheka tu badala ya kuwawajibisha watendaji wake, halafu utasikia watu wanasema Kikwete anaangushwa na watendaji wake!!! UPUUZI MTUPU!!
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kila mara wapinzani wanapata agenda zao za kisiasa toka serikali ya magamba halafu wanaishia kulaumiana, kwanini wanawaundia agenda wapinzani ambazo mwisho wa siku ni mwiba kwao? Ok kwangu ni faida acha waendelee na tabia hiyo ambayo inasaidia kufumbua macho wadanganyika, hata watetezi wao (fa, ms nk) humu jamvini kwenye mada kama hii huwasiki wanaingia mitini!
   
Loading...