Vigogo wastaafu kuingia uwanjani kumwokoa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wastaafu kuingia uwanjani kumwokoa JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Baija Bolobi, Oct 7, 2010.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wana JF

  Sambamba na matokeo ya kuchakachua kutoka REDET, habari zilizoingia kwenye dish langu muda mfupi uliopita, zinasema wastaafu wameombwa na kubembelezwa sana kuingia kwenye kampeini kumwokoa JK ambaye hali yake ni mbaya. Kazi ya kubembeleza imefanywa na Makamu M/Kiti wa CCM (Bara), Mzee Msekwa na amenitonya leo mchana kuwa wazee wanaingia kuanzia wiki ijayo. Waliokubali japo kwa shingo upande ni FTS, BWM, AHM, na of course EL.

  Waliokataa ni JSW na SAS.

  Mzee JSM amekubali kwenda baadhi ya majimbo, siyo kwa kumnadi mgombea urais.

  Inaonekana mkwala wa Redet unalenga kuwapa pa kuanzia katika kampeini zao, na mapolisi wameagizwa wahakikishe wazee hawazomewi.

  Nionavyo mimi: La kuvunda......
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  wacha waingie lakini wasilalamike wakirushiwa makombora Shimbo mwenyewe katulia anajuta kuingia.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Walisema wakizidiwa wataomba wazee wasaidie, sasa watakuwa wamekubali mambo mazito lakini hatudanganyiki. Waliokubali wote wana kashfa wataumbuka na watazomewa, wangekaa kimya kutunza heshima zao.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Tatizo nilionalo hao wote waliorodheshwa wan kashfa nzito ambazo wananchi wangelipenda utawala mpya wa Dr. SLaa uzishughulikie haraka iwezekanavyo bila kuchelea.

  Kwa kujito mhanga watutasaidia katika kuchokonoa vidonda vilivyoanza kupona. Ningewashauri waanze leo kwa jitihada zote zile wawezazo.

  Naelewa JK anakerwa kuona ni familia yake tu ndiyo inachanja mbuga lakini kula si anakula mwenyewe na wapambe wake wachache tu na hivi majuzi alinena uraisi ni suala la kifamilia.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  la kuvunda halina ubani jk habebeki
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kazi wanayo mwaka huu. nasikia mama salma ameshachonga fimbo ili aitumie baada ya uchaguzi.
   
 7. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwanza asante
  Ninajiuliza
  1. Hawa FTS, BWM, AHM wamekuwa sehemu ya familia ya JK? Maana urais wa JK ni wa familia labda EL amekuwa sehemu tayari kwa osmosis
  2. Hao polisi wanaoagizwa kudhibiti wananchi ni wale wanaolala kwenye nyumba za bati na kuishi kwa rushwa ya buku 2 au ni wanajeshi wa Shimbo?

  -Nashukuru hatimaye wametuletea Mkapa aje ajibu tuhuma zinazomkabili.
  -Mwinyi inabidi awe makini maana ile ya kupigwa kofi haikuwa ishara nzuri
  -Sumaye duh nitasubiri atakachosema
  -Lowassa ndo atakuja na tulilia pamoja, sijui tulisimangwa pamoja sana tuchague pamoja...kwi kwi kwiiii
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Jamani na sisi tuongeze nguvu kuwa saidia CHADEMA kwa michango...maana Arusha tunasema wao wana pesa sisi tuna mungu tutashinda...kwa kuwakubusha andika CHADEMA tuma kwenda 15710 mchango wako ni mhimu sana...
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sumaye jukwaani akimna JK duh hii kali naisubi hiyo siku ikifika, na kama Lowasa ataanze kumnadi jamaa yake wajue kura zitazidi kupungua kwa CCM maana hata watu wanao unga mkono tume ya Mwakyembe waliko CCM najua tutawapata wote...
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kinana alisema CCM haitawatumia wazee hadi hapo watakapo zidiwa atueleze kama sasa wameshazidiwa. Ni bora waje ili Slaa aongeze vocabulary kwenye kampeni yake maana alikuwa anaogopa kuwataja atambiwa hana adabu kwa wazee sasa atakuwa na uwezo wa kumuuliza Mkapa kama amekuja na malipo ya wafanyakazi wa Kiwira.
   
 11. m

  mozze Senior Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua Zaidi ya Mwl. Julius K. Nyerere, ndani ya CCM hakuna wa kuweza kuwabadili Watanzia. Watu hawajamchoka Kikwete tu bali hakuna ambacho CCM wanaweza kujivunia, hata hao waliopita. Embu fikiria watakuja na hoja gani? Je ni kivipi kwa mfano wanaweza kumsafisha Kikwete na tuhuma za Ufisadi? Je unafikiri Mkapa anaweza kwenda Kiwira?

  Kwa vile hawana cha kujivunia katika maisha ya mwananchi wa kawaida Haitakuwa na impact. Chadema wawatupie tu makombora ya madudu waliyofanya wakati wa uongozi wao!
   
 12. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  JK alidharau wakunga wakati uzazi ungalipo..... Nakumbuka baada ya ushindi wa kimbunga wa 2005, JK alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzisambaratisha kambi za wapinzani wake, hususan za SAS na FTS!!! Utawala wake ukaendekeza umakundi usio na tija kwa taifa...maana wanasiasa ambao walikuwa na uwezo wa uongozi walinyimwa nafasi za uwaziri kisa eti walikuwa wafuasi wa wapinzani wake... Akaishia kuchagua mawaziri vihiyo(e.g., SS) ambao hatimaye wamemfikisha hapo alipo!!!!!! Mbaya zaidi majuzi tu hapa Makamba na REDET wakamjaza ujinga uliokubuhu(eti JK ni maarufu kuliko chama kilichompa mamlaka)!!!! Hiyo ndio ikampa kiburi cha kudiriki kuteua JK family members wampigie kampeni baba yao......shame ...shame...shame...... Mwisho ndio huu hapa... wakunga waliodharauliwa zamani sasa wanahitajika kuokoa jahazi......

  Hebu tusubiri tuone mwisho!!!
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  jahazi lilishazama . Wataokoa maiti au. Na waje waone moto ulivyo mkali.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yatakuwa makosa makubwa sana kwa JK na CCM kuwatumia wazee hao. Alichotakiwa JK kufanya ni rahisi sana ila kama walivyosema wakongwe JK kiburi sana na ujana bado unamsumbua.

  JK ameshindwa kukubali mapungufu yake kiroho na hakika kama angeweza kuyakabiri mapungufu yake na kuyafanyia kazi mapema sidhani kama kungekuwa na Upinzani mkali kama huu.

  Kikubwa zaidi ni pale alipolazimisha kusimamisha watu wa Lowassa dhidi ya chaguo la wananchi hali akijua fika kwamba wagombea hawa wana scandals kubwa sio tu kitaifa bali hadi ktk majimbo yao wanayogombea..
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Some time intended message haifiki yote kwa walengwa kwa haraka. Mkuu naomba let me decode for others wanaoweza kukkwama kwa amuda kuwatambua
  i guess
  FTS= Fredrick Sumaye
  BWM= Benjamin Wiliam Mkapa
  AHM= Ali Hassan Mwinyi
  JSM= John Samwel Malechela
  SAM = Salim Ahmed Salim

  What about JSW= Joseph Sinde warioba yuko chama gani
   
 16. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Wasiende jimbo la Mbulu.
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,813
  Trophy Points: 280
  Waache hata huko waende! Hujasikia jamaa yao alivyopigiwa mayowe ya MWIIIIZIIIIIIIIIIII PIGA HUYO MWIZIIIIIIIIIIIIIIII!!!!!!!!! WENYEWE TUTAWASIKIA. HEBU WASHAURINI HAO WAZEE WAPUMZIKE WAJILIE PENSION ZAO!!!! YA NINI KUSUMBUKIA JK FAMILY?? NA MTU WAO MWAKA HUU HABEBEKI TUTAWAONA NGOJA WAJE!!!!!
   
Loading...