Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Vigogo wanaotuhumiwa kumiliki Tangold wahojiwa TAKUKURU
2008-05-14 10:28:08
Na Simon Mhina
Makatibu wakuu wa wizara tatu wanaodaiwa kumiliki kampuni ya Tangold iliyokuwa inachimba dhahabu katika mgodi wa Buhemba mkoani Mara, wamehojiwa mara kadhaa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Bw. Patrick Rutabanzibwa, aliyedaiwa kuwa mmoja wa Makatibu Wakuu wanaomiliki kampuni hiyo, alithibitisha kuhojiwa na taasisi hiyo.
Bw. Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kuundwa Tangold na kuanza uchimbaji dhahabu Buhemba, alisema hayo jana alipohojiwa na Nipashe kwa njia ya simu.
Alisema makatibu hao waliohojiwa ni waliokuwa wajumbe wa kamati ya Rais Benjamin Mkapa, iliyoundwa kusimamia na kumaliza matatizo ya kampuni ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya MEREMETA iliyokuwa inachimba dhahabu Buhemba.
Wajumbe wa kamati maalum iliyoundwa 2003 ni Dk. Daudi Balali, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Wengine ni Makatibu Wakuu, Bw. Gray Mgonja wa Wizara ya Fedha, Bw. Rutabanzibwa, Bw. Vincent Mrisho aliyekuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, sasa yuko Ofisi ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu, Bw. Andrew Chenge.
Bw. Rutabanzibwa alisema wapo `roho juu`, kufuatia kuhojiwa mara kadhaa bila kupata ripoti juu ya tuhuma hizo.
``Tumehojiwa, mwenyewe nimehojiwa mara tatu kuhusiana na madai hayo. Niko roho juu maana sijui nini kinafanyika,`` alisema.
Hata hivyo, alisema anaamini kuwa, taarifa ya TAKUKURU itakapotolewa itamsafisha kwa vile yeye ni mtu safi.
Alipoulizwa inadaiwa kuwa, wajumbe wa kamati maalum ndiyo baadaye waliochukua mgodi wa Buhemba kupitia Tangold, alikanusha na kusisitiza kwamba, mgodi huo ni mali ya serikali.
``Kila hatua kamati iliyofikiwa ilikuwa inamwarifu Rais Mkapa ambaye naye alikuwa akitoa maelekezo kadhaa,`` alisema na kuongeza ``hatujawahi kuwa wamiliki na hata sasa Buhemba ni mali ya umma.``
Bw. Rutabanzibwa ambaye alitajwa na kambi ya upinzani kwenye orodha inayodaiwa kuwa ni ya mafisadi, alisema kamati maalum ilikuwa ni Wakurugenzi wa Tangold kwa niaba ya serikali.
Alifafanua kuwa, moja ya majukumu waliyokuwa nayo ni kurithi mali na madeni ya MEREMETA.
Alisma Rais mstaafu aliunda kamati hiyo kwa busara kwa vile aliona kuwa madeni ya kampuni hiyo ya JWTZ iliyoingia ubia na Triennex Properietary Limited ya Afrika Kusini ingekuwa na athari kwa taifa.
Kuhusu madai kuwa mgodi ulipata faida na fedha hazijulikani zilipo, alikanusha na kuongeza kwamba, hakuna fedha zilizopotea.
Aliongeza kuwa, zingetoweka ingegundulika kwa vile walikuwa wanaripoti na serikali ilikuwa inafuatilia uzalishaji.
Wakati Bw. Rutabanzibwa akitoa maelezo hayo, Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, Tangold walitaka kuhamisha kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) cha Kiabakari ili kuwezesha kuchimba dhahabu iliyokuwa eneo hilo.
Mkakati huo wa kutaka kuhamisha kambi ya Kiabakari, ulipendekezwa na manejimenti ya mgodi wa dhahabu wa Buhemba kampuni ya Tangold na kubarikiwa na kamati hiyo ya Makatibu Wakuu, BoT na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
Kiabakari ilianzishwa na serikali baada ya Uhuru ili kulinda madini hayo hadi Tanzania itakapokuwa na uwezo wa kuyachimba na pia ilikuwa karibu na kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Buhemba ambayo nayo ilikuwa na nia ya kulinda raslimali hizo.
Menejimenti hiyo ilitoa wazo hilo ilikuwa chini ya Meneja Mkuu wa Mgodi, Bw. Jan Duvenage, na kwamba iliona kuwa kuhamishwa Kiabakari ni suala la kipaumbele ili kufikia dhahabu iliyokuwa kwenye ardhi ya kambi hiyo.
Watendaji wengine waliokuwa wanatoka nje ya nchi Meneja wa Mitambo, Roy Dias na Mtaalam wa Uangalizi wa Mitambo, Bw. Marius Hayes.
Wengine ni Meneja wa Fedha, Bw. Prudence Kami, Meneja Uajiri, Bw. Augustine Athumani, wakati Meneja wa Masuala ya Miamba, Jiolojia na Mazingira alikuwa Bw. Emmanuel William na kwa upande wa Vifaa na Mipango alikuwa Bw. Agnus.
Manejimenti ya BGM ilitoa wazo kwamba ipewe kibali cha kuingia katika kambi ya Kiabakari na kuchimba madini katika maeneo hayo ambayo yamegundulika kuwa yana dhahabu.
``Kwa kuelewa kuwa, maamuzi ya kuhamisha kambi ya Kiabakari kwenye eneo jingine ili kuanzisha uchimbaji kutahitaji maamuzi ya ngazi za juu kitaifa, menejimenti ya BGM imeiomba Wizara ya Nishati na Madini kufanikisha mpango huo,`` kilisema chanzo hicho kilichokuwa kikikariri miniti za mikutano ya menejimenti.
Watanzania walikuwa 173 wakati wataalamu wa kigeni ni watano. Kwa mujibu wa ripoti zilizoandaliwa na manejimenti, watawala hao waliitaka serikali kuamua kwa haraka hatma ya mgodi wa Buhemba na uhamishaji wa kambi ya Kiabakari ili kuokoa mashine na mitambo inayoharibika katika eneo hilo bila kutumika.
Manejimenti hiyo haiko tena.
SOURCE: Nipashe