Vigogo wanaotuhumiwa kumiliki Tangold wahojiwa TAKUKURU

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,584
6,635
Vigogo wanaotuhumiwa kumiliki Tangold wahojiwa TAKUKURU

2008-05-14 10:28:08
Na Simon Mhina

Makatibu wakuu wa wizara tatu wanaodaiwa kumiliki kampuni ya Tangold iliyokuwa inachimba dhahabu katika mgodi wa Buhemba mkoani Mara, wamehojiwa mara kadhaa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Bw. Patrick Rutabanzibwa, aliyedaiwa kuwa mmoja wa Makatibu Wakuu wanaomiliki kampuni hiyo, alithibitisha kuhojiwa na taasisi hiyo.

Bw. Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, wakati wa kuundwa Tangold na kuanza uchimbaji dhahabu Buhemba, alisema hayo jana alipohojiwa na Nipashe kwa njia ya simu.

Alisema makatibu hao waliohojiwa ni waliokuwa wajumbe wa kamati ya Rais Benjamin Mkapa, iliyoundwa kusimamia na kumaliza matatizo ya kampuni ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ya MEREMETA iliyokuwa inachimba dhahabu Buhemba.

Wajumbe wa kamati maalum iliyoundwa 2003 ni Dk. Daudi Balali, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Wengine ni Makatibu Wakuu, Bw. Gray Mgonja wa Wizara ya Fedha, Bw. Rutabanzibwa, Bw. Vincent Mrisho aliyekuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, sasa yuko Ofisi ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu, Bw. Andrew Chenge.

Bw. Rutabanzibwa alisema wapo `roho juu`, kufuatia kuhojiwa mara kadhaa bila kupata ripoti juu ya tuhuma hizo.

``Tumehojiwa, mwenyewe nimehojiwa mara tatu kuhusiana na madai hayo. Niko roho juu maana sijui nini kinafanyika,`` alisema.

Hata hivyo, alisema anaamini kuwa, taarifa ya TAKUKURU itakapotolewa itamsafisha kwa vile yeye ni mtu safi.

Alipoulizwa inadaiwa kuwa, wajumbe wa kamati maalum ndiyo baadaye waliochukua mgodi wa Buhemba kupitia Tangold, alikanusha na kusisitiza kwamba, mgodi huo ni mali ya serikali.

``Kila hatua kamati iliyofikiwa ilikuwa inamwarifu Rais Mkapa ambaye naye alikuwa akitoa maelekezo kadhaa,`` alisema na kuongeza ``hatujawahi kuwa wamiliki na hata sasa Buhemba ni mali ya umma.``

Bw. Rutabanzibwa ambaye alitajwa na kambi ya upinzani kwenye orodha inayodaiwa kuwa ni ya mafisadi, alisema kamati maalum ilikuwa ni Wakurugenzi wa Tangold kwa niaba ya serikali.

Alifafanua kuwa, moja ya majukumu waliyokuwa nayo ni kurithi mali na madeni ya MEREMETA.

Alisma Rais mstaafu aliunda kamati hiyo kwa busara kwa vile aliona kuwa madeni ya kampuni hiyo ya JWTZ iliyoingia ubia na Triennex Properietary Limited ya Afrika Kusini ingekuwa na athari kwa taifa.

Kuhusu madai kuwa mgodi ulipata faida na fedha hazijulikani zilipo, alikanusha na kuongeza kwamba, hakuna fedha zilizopotea.

Aliongeza kuwa, zingetoweka ingegundulika kwa vile walikuwa wanaripoti na serikali ilikuwa inafuatilia uzalishaji.

Wakati Bw. Rutabanzibwa akitoa maelezo hayo, Mwandishi Wetu anaripoti kuwa, Tangold walitaka kuhamisha kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) cha Kiabakari ili kuwezesha kuchimba dhahabu iliyokuwa eneo hilo.

Mkakati huo wa kutaka kuhamisha kambi ya Kiabakari, ulipendekezwa na manejimenti ya mgodi wa dhahabu wa Buhemba kampuni ya Tangold na kubarikiwa na kamati hiyo ya Makatibu Wakuu, BoT na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Kiabakari ilianzishwa na serikali baada ya Uhuru ili kulinda madini hayo hadi Tanzania itakapokuwa na uwezo wa kuyachimba na pia ilikuwa karibu na kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Buhemba ambayo nayo ilikuwa na nia ya kulinda raslimali hizo.

Menejimenti hiyo ilitoa wazo hilo ilikuwa chini ya Meneja Mkuu wa Mgodi, Bw. Jan Duvenage, na kwamba iliona kuwa kuhamishwa Kiabakari ni suala la kipaumbele ili kufikia dhahabu iliyokuwa kwenye ardhi ya kambi hiyo.

Watendaji wengine waliokuwa wanatoka nje ya nchi Meneja wa Mitambo, Roy Dias na Mtaalam wa Uangalizi wa Mitambo, Bw. Marius Hayes.

Wengine ni Meneja wa Fedha, Bw. Prudence Kami, Meneja Uajiri, Bw. Augustine Athumani, wakati Meneja wa Masuala ya Miamba, Jiolojia na Mazingira alikuwa Bw. Emmanuel William na kwa upande wa Vifaa na Mipango alikuwa Bw. Agnus.

Manejimenti ya BGM ilitoa wazo kwamba ipewe kibali cha kuingia katika kambi ya Kiabakari na kuchimba madini katika maeneo hayo ambayo yamegundulika kuwa yana dhahabu.

``Kwa kuelewa kuwa, maamuzi ya kuhamisha kambi ya Kiabakari kwenye eneo jingine ili kuanzisha uchimbaji kutahitaji maamuzi ya ngazi za juu kitaifa, menejimenti ya BGM imeiomba Wizara ya Nishati na Madini kufanikisha mpango huo,`` kilisema chanzo hicho kilichokuwa kikikariri miniti za mikutano ya menejimenti.

Watanzania walikuwa 173 wakati wataalamu wa kigeni ni watano. Kwa mujibu wa ripoti zilizoandaliwa na manejimenti, watawala hao waliitaka serikali kuamua kwa haraka hatma ya mgodi wa Buhemba na uhamishaji wa kambi ya Kiabakari ili kuokoa mashine na mitambo inayoharibika katika eneo hilo bila kutumika.
Manejimenti hiyo haiko tena.

SOURCE: Nipashe
 
I smell kumpandisha JK chart hapa .JK alitamka kule Dodoma kwamba hakuna wa kukamatwa na iweje leo watu wahojiwe ? Wana hojiwa kwa sababu ipi na mahojiano haya yana faida gani ?
 
I smell kumpandisha JK chart hapa .JK alitamka kule Dodoma kwamba hakuna wa kukamatwa na iweje leo watu wahojiwe ? Wana hojiwa kwa sababu ipi na mahojiano haya yana faida gani ?

Mkuu

Kikubwa sana ni kwamba hawa watu walisha kubali kwamba TANGOLD wao ni wakurugenzi mimi nafikiri haitakuwa haki kuhojiwa wakati bado wako OFISINI. Tayari wakati Dr. Slaa amekata issue hizi hawa wenyewe walikuja juu na kusema kuwa wangeenda mahakamani. Mkuu Jk alishasema kelele za Wapinzania haziwezi kumnyima usingizi.

Tutashukuru sana kama kweli sasa kuna kitu kinafanyika. Lakini pia nafikiri kuojiwa hakuko makini sana. Utamuojije Waziri, Katibu Mkuu nk. Nafikiri imefika wakati kama tuhuma zinakwendea moja kwa moja huna budi kuhakikisha unaachia ngazi hili uchunguzi uwe wa huru nahaki.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tangold ni Daudi Balali je bado Serikali haimhitaji? CHANGA LA MACHO.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Tangold ni Daudi Balali je bado Serikali haimhitaji? CHANGA LA MACHO.

Au wame-mmhoji saa ngapi ili hali wanasema hawa muhitaji? Next press -conference inabidi wamuulize Salva , lakini najua Salva atalikwepa hili
 
yote ni maisha,ila serikali yetu inatumaliza kila kitu...... mwisho wa ccm umefika bora tuwe kama kenya au zimbabwe....
 
Tanzania... Tanzania... tanzania inateketea, mimi sioni mantiki ya kuunda kamati ambayo ni wakurugenzi wa kampuni moja tena inayojihusisha na madini. Kwanini kampuni iwe kamati kuwakilisha serikali? hebu ona huo uamuzi wa kuyalinda ulivyokuwa wa busara, sasa tunataka kila kona tupa expose kwa wawekezaji mafisadi...oooohhhh..
 
Nazidi kuuliza wana hojiwa ili iwe nini ?Maana Mkuu JK hana mpango wa kuwakamata na alitamka bayana pale Butiama mimi nilikuwepo leo unasema wame hojiwa ili nini kitokee jamani ?
 
Changa la Macho hilooooooooo!!!! Tanzania nchi ya amani, nchi yenye utulivu, nchi yenye watu wanaofuata utawala bora, utawala wa sheria. Watu wasiopokea rushwa. Tuendelee kuwa wapole tuu

Hakuna kitu hapa.. maneno tuu.. Tulianza na Balali kafukuzwa kazi kimla ila bado anaendelea na nyadhifa nyingine za ukurugenzi kwenye baadhi ya taasisi.. Tukaja kwa EL akaenda kuchinja ng'ombe kule kwao watu wakala wameshasahau.. Karamagi kimyaaaa... Amekuja mzee wa vijisenti nayo ni historia tuu imebaki... Richmond, EPA, TANGOLD, Meremeta, Radar, Ndege ya Rais ambayo ipo tuu kama scraper na kuna mjinga mmoja alisema tutakula nyasi ila ndege lazima inunuliwe naye yupo tuu...

Nasema hakuna kitu.. naomba ambaye anaweza kuniambia kuwa kuna kitu kitafanyika athibitishe hapa... I said Nothing ni kelele amabzo hazimnyimi mkuu wa kaya kulala usingizi tena mnono. Hakuna kazi rahisi kam akuongoza watu waoga.. na wasiojua mambo... Tunapiga kelele tuu hapa JF nani anayejua haya kule Maneromango? kule Iramba, au kule Kyela? Hakuna nasema ni kelele za chura tuu...

We need action. Sisemi tufanye action za kuoigana kama Kenya la Hasha.. nasema tuviweke hivi tunavyoviandika huku kwa matendo.. twende kule kijijni wanakogawa ng'ombe tuwaambie wazee wetu wakatae kula hizo ng'ombe. Vyama vya siasa viache malumbano waende vijijni mapema kabisa kuwaambia wananchi wanavyoibiwa damu yao.. waende huko vijijini kwenye wapiga kura wengi.. Hawa wanaoandika hapa wala hawapigi kura....

Waandishi wa habari waache njaaa zao za kuhongwa vihela kidogo tuu wanaandika mambo yasiyokuwa na maana.. kuandika magazeti ya udaku tuu.. sijui nani kafumaniwa.. nani alikuwa uchi.. yote hayo hayana maana... waandike yanayotokea tz kwa sasa na wapeleke vijijjini...,
 
siwezi kuthamini mchango wa tukururu kwenye hili.
tukururu yenyewe imejaa ufisadi, na hilo lipo wazi.
sasa leo fisadi huyo huyo unataka afichuwe fisadi wenziwe, kweli kutapatikana ukweli wowote hapo?

hivi watanzania tutaendelea kuongozwa kwa tamaa mpaka lini? kwa nini tumekuwa na mioyo ya kuwaamini sana hawa watawala wetu?

watu wanafanya ufisadi kila kukicha, na watu hao hao wakituambia wanachunguza ufisadi, tunawaamini! amazing!
 
Wajumbe wa kamati maalum iliyoundwa 2003 ni Dk. Daudi Balali, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) aliyefukuzwa kazi kwa tuhuma za ufisadi uliofanyika kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Wengine ni Makatibu Wakuu, Bw. Gray Mgonja wa Wizara ya Fedha, Bw. Rutabanzibwa, Bw. Vincent Mrisho aliyekuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, sasa yuko Ofisi ya Waziri Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu, Bw. Andrew Chenge.


Huitaji kuwa na akili kubwa kiuua ni kiasi hapa watu hawa wamewekwa hapa kwajili ya kula na kulindana, kuna sababu gani ya Kiwete kuwa kimya mpaka muda huu.... kutoachia vyombo vya sheria kuwa huru na kufanya kazi yao....

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hata hivyo, alisema anaamini kuwa, taarifa ya TAKUKURU itakapotolewa itamsafisha kwa vile yeye ni mtu safi

Anajua kuwa TAKUKURU io kwa ajili ya kuwalinda wao ndio maana anajua kuwa itamsafisha.... hivi Pinda ameshahojiwa na kuzungumzia malalamiko ya wananchi juu ya kutotakiwa na kutoaminiwa kwa HOSEA NA MWANYIKA???
 
5. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA

Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma

http://www.chadema.net/habari/2007/orodha1/ukurasa5.php
 
Nakumbuka Mwaka 2004...ilyokuwa Pcb,waliwahi Kumuhoji El Na Rita Mlaki....hadi Leo Umeshawahi Kusikia Matokeo Ya Uchunguzi Ule?maana El Alitokwa Na Jasho Kama Anaumwa Vile Wakati Anahojiwa......sioni Ajabu Hata Hao Kuhojiwa..hakuna Lolote Litakalotokea...hizo Pesa Wametafuna Wote
 
Hii ni hatari hakika taifa limekosa wazalendo na wanaojiita wazalendo ndiyo wezi na mafisadi wa wakubwa.

Mhe. Kafulila amepasua jipu kwa kueleza kuwa Mhe. sana Joseph Sinde Warioba anachunguzwa kwa ufisadi wa kampuni ya uchimbaji madini ya TAN Gold kwa ufisadi wa billion sita. Anachunguzwa na TAKUKURU na faili la ripoti ya TAKUKURU ipo kwa Mhe. Rais.

Chanzo: EATV (Hot Mix)
 
Back
Top Bottom