Vigogo wanane wa manispaa ya K'ndoni kortini kwa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wanane wa manispaa ya K'ndoni kortini kwa ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Jun 29, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Vigogo wanane kortini kwa ufisadi


  Vigogo wanane kortini kwa ufisadi

  Waandishi Wetu

  VIGOGO wanane wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka 45 tofauti.

  Mashtaka ya watendaji hao wa Manispaa ya Kinondoni yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ikiwemo kutumia madaraka vibaya pamoja na kutoa taarifa za uongo kwa mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

  Washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Ardhi Manispaa ya Kinondoni, Hamidu Mgaya, Ofisa Mtendaji Kilongawima Mbezi, Wanura Maranda, Mwenyekiti wa mtaa Kilongawima Mbezi, Francis Woiso na Diwani wa kata ya Kunduchi, Patrick Makoyola.

  Watuhumiwa hao kwa pamoja walisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Leonard Swai, ambaye aliieleza mahakama kuwa watuhumiwa hao wamevunja kifungu namba 31 cha kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutumia madaraka yao vibaya pamoja na kutoa taarifa za uongo kwa waajiri wao.

  Swai alidai mbele ya Hakimu Yohana Yongolo wa mahakama hiyo kuwa, mnamo mwezi Juni na Julai mwaka 2008, watendaji wa hao walitoa taarifa za uongo kwa mkurugenzi wao zikionyesha kuwa eneo ambalo lililopo katika michoro ya mipango miji namba TR.DRG. 1/12/8001 kuwa linamilikiwa na Athumani Mahimbo ambapo walimsajili kwa namba ya eneo 2466 Block L Mbezi.

  Swai alidai kuwa watuhumiwa hao walifanya jambo hilo huku wakijua kuwa ni kosa na kwamba mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni asingelikubali hilo endapo angepewa maelezo sahihi.

  Wengine waliofikishwa mahakamani hapo na Takukuru ni Anna Macha ambaye ni Ofisa Mipango Miji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mapambano Baseka (Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni), Said Waligwah (Ofisa Mtafiti wa ardhi Manispaa ya Kinondoni) na Hamidu Mgaya (Ofisa ardhi manispaa ya Kinondoni).

  Swai alidai kuwa watuhumiwa hao walitumia madaraka yao vibaya na kuvunja kifungu cha sheria namba 12(1) cha mwaka 1999 namba nne katika sheria ya michoro ya mipango miji kwa kummilikisha Kheri Mabira eneo walilolisajili kwa namba 2473 lililoko Block L Mbezi.
  Swai alidai eneo hilo ni la wazi ambalo lilitengwa na serikali kwa matumizi ya umma.

  Watuhumiwa wote walikana na mashtaka hayo na walipata dhamana baada ya wadhamini kukubaliana na masharti waliosomewa na hakimu.

  Hata hivyo, watuhumiwa saba kati ya nane ndiyo walifika mahakamani hapo huku Patrick Makoyola akikosekana, ambapo mahakama iliamuru atafutwe na polisi na kufikishwa mahakamani hapo.

  Hata hivyo, Hakimu Yongolo alisema kesi hiyo itasomwa tena Julai 26 mwaka huu.

  Chanzo: Mwananchi  My Take:

  Vipi hawa PCCB kazi yao kubwa ni kufungua mashitaka dhidi ya kutoa taarifa za uongo. Kwa nini huwa hakuna mashitaka ya kupokea rushwa au wizi,i nk?
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,054
  Likes Received: 6,495
  Trophy Points: 280
  Hizo ni bla bla tu, bongo hakuna kesi, ni nchi ya kitu kidogo
   
 3. m

  mob JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  mbona kinondoni iko ivi.jana machozi yamenitoka baada ya kuona wamachinga walioko ndani ya stendi ya mwenge anakaguliwa na baunsa atoe risiti kwa ajili ya kuuza mahindi ya kuchoma ndani ya stendi.hii ni bila risiti ukikataa inakuwa shida kwako.jamani viongozi wenye dhamana na nchii hii hili jambo linakatisha tamaa jamani
   
 4. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hakuna kitu TAKURUKU wanajisafisha kama kweli vidume wamtoe chenge uraiani BAE na JK richmond
   
 5. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Wameshtakiwa kwa kosa la Matumizi mabaya ya madaraka,kusema uwongo na kujipatia manufaa kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa No.11,2007. Yote hayo ni makosa ya Jinai mzee
   
 6. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huyo mwandishi anaandika taarifa bila kufanya utafiti wa kina, waandishi bana. hamidu mgaya sio mkuu wa kitengo cha ardhi na wala sio afisa ardhi. Mgaya alikua mkuu wa kitengo cha upimaji na ramani na yeye ni mpima wa ardhi, pia mapambano baseka ni afisa mipango miji na wala sio afisa ardhi. Waandishi msiwe wavivu kufanya utafiti wa habari kwani mnaupotosha umma
   
 7. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,964
  Trophy Points: 280
  hao nao ni vigogo? vigogo wapo wanaendelea kuitafuna nchi huku wako kwenye viyoyozi hizo ni kafara ili takukuru ionekana inafanya kazi.
   
Loading...