Vigogo waliomuua Amina Chifupa

kkiwango

Senior Member
Aug 27, 2007
173
14
Mzee Chifupa: Bado tunachunguza vigogo waliomwua Amina

na Prisca Nsemwa

DUNIA imetakiwa kusimama imara na kwa nguvu ili kupinga dawa za kulevya kwa kuwa zina athari kubwa kwa jamii, hasa vijana.

Katibu wa Mfuko wa Amina Chifupa ambaye pia ni baba wa Amina, Luteni Hamis Chifupa alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), ambapo alikifananisha kifo cha mtoto wake na cha Yesu Kristo au Nabii Issa.

Alisema amemfananisha marehemu Amina na manabii hao kwa kuwa alikuwa na maajabu, hivyo kutokana na maajabu hayo pamoja na mambo mazito aliyoyafanya enzi ya uhai wake, familia imejenga kaburi lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 ambalo linafanana na uzito huo.

“Amina amekufa kama Nabii Issa aliyekufa na alivyozaliwa, ndiyo maana familia imejenga kaburi linalofanana na uzito wake ingawa Issa bin Mariamu hana kaburi duniani,” alisema Chifupa.

Pia alisema Amina alikufa akiwa vitani akipagania vijana wanaoharibika kwa kutumia dawa za kulevya na wale wanaosambaza dawa hizo.

Akizungumzia ugonjwa uliosababisha kifo cha Amina, alisema kuwa ni kisukari na ushirikina, na kuongeza kuwa kifo chake kimeharakishwa na watu ambao hivi sasa familia inaendelea na uchunguzi na mara baada ya kumalizika watatoa matokeo.

“Wakati Amina anaumwa alikuwa akitaja majina ya watu wazito ambao wengine ni viongozi na wafanyabiashara, hivyo tunafanya uchunguzi wetu wa kimya kimya kwa kuwa hatujui aliyataja majina yale kwa mazuri au mabaya, na tukimaliza tutayataja hapa hapa kutimiza maandiko yake,” alisema.

Luteni Chifupa alisema kuwa kaburi la Amina ni la kihistoria nchini kwa kuwa limejengwa kwa mfano wa kaburi la Shariff Musa ambaye ana makaburi saba duniani.

Amina ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifariki Juni mwaka jana.
 
Hivi huyu mzee si alisema ni mapenzi ya Mungu wala watu wasiseme ni ushirikina, hawajamkolimba Amina, na sasa anasema bado wanachunguza huo ushirikina. Sasa tuelewe lipi? mgao alioahidiwa hajakatiwa au ni vipi?
 
kkiwango, truth always prevail.... tusimlaumu sana. yawezekana amepata mwangaza zaidi maana binadamu huwa tunajifunza mapya kila siku. as long as ata acknowledge kuwepo kwa statement zake za awali na atazifuta, basi hatuwezi kumpinga kwa hili jipya aliloliona na kuamua aliseme.
 
Hivi huyu mzee si alisema ni mapenzi ya Mungu wala watu wasiseme ni ushirikina, hawajamkolimba Amina, na sasa anasema bado wanachunguza huo ushirikina. Sasa tuelewe lipi? mgao alioahidiwa hajakatiwa au ni vipi?

Nakumbuka siku hiyo ya kifo Amina alitaja kuna ushirikaina ulosababisha kifo cha mwanawe, kwenye mahojiano na TV...sikumbuki ni ipi.....halafu baadae katika mahojiano mengine hakutaja ushirikina
 
Mzee Chifupa:
ambapo alikifananisha kifo cha mtoto wake na cha Yesu Kristo au Nabii Issa.

Alisema amemfananisha marehemu Amina na manabii hao kwa kuwa alikuwa na maajabu, hivyo kutokana na maajabu hayo pamoja na mambo mazito aliyoyafanya enzi ya uhai wake, familia imejenga kaburi lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 ambalo linafanana na uzito huo.
“Amina amekufa kama Nabii Issa aliyekufa na alivyozaliwa, ndiyo maana familia imejenga kaburi linalofanana na uzito wake ingawa Issa bin Mariamu hana kaburi duniani,” alisema Chifupa.

Pia alisema Amina alikufa akiwa vitani akipagania vijana wanaoharibika kwa kutumia dawa za kulevya na wale wanaosambaza dawa hizo.

Akizungumzia ugonjwa uliosababisha kifo cha Amina, alisema kuwa ni kisukari na ushirikina, na kuongeza kuwa kifo chake kimeharakishwa na watu ambao hivi sasa familia inaendelea na uchunguzi na mara baada ya kumalizika watatoa matokeo.

Huyu Mzee aache kujikanyaga sasa. Yaani ameamua kuanza kutafuta umaarufu kwa nguvu kupitia kifo cha mtoto wake???!!!!

Eti amekufa kama Nabii Isa......KUFURU hii. Amina si ndo huyo tunasikia alikuwa anarukaruka kama kindege tu .... anafananishwa vipi na manabii???!!!

Alikuwa na maajabu.... Maajabu ya kutangaza redio au ya kufanyaje??? Huyo mtoto hata shule alishindwa kusoma ...halafu leo alikuwa wa ajabu.

Huyo mzee anatakiwa kushauriwa. Kila mtu angependa kumuona mtoto wake wa ajabu. Lakini kama wewe unamuona wa ajabu uwe unashangaa uajabu wake ndani kwako. Unaita waandishi wa habari kutoa pumba

Eti kaburi la milion tatu linafanana na Amina.... ama kweli alikuwa mtoto wa ajabu !!! Kama alikuwa anafanana na kaburi ni ajabu na kweli. Mzee anatakiwa kushauriwa nini anaongea kwenye vyombo vya habari sio kukurupuka tu.
 
Mzee Chifupa: Bado tunachunguza vigogo waliomwua Amina

na Prisca Nsemwa

DUNIA imetakiwa kusimama imara na kwa nguvu ili kupinga dawa za kulevya kwa kuwa zina athari kubwa kwa jamii, hasa vijana.

Katibu wa Mfuko wa Amina Chifupa ambaye pia ni baba wa Amina, Luteni Hamis Chifupa alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), ambapo alikifananisha kifo cha mtoto wake na cha Yesu Kristo au Nabii Issa.

Alisema amemfananisha marehemu Amina na manabii hao kwa kuwa alikuwa na maajabu, hivyo kutokana na maajabu hayo pamoja na mambo mazito aliyoyafanya enzi ya uhai wake, familia imejenga kaburi lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 3 ambalo linafanana na uzito huo.

“Amina amekufa kama Nabii Issa
Nabii Issa alikufaje? Wenye data watuwekee tujadili.
aliyekufa na alivyozaliwa

Alizaliwaje huyo Nabii Issa? ndiyo maana familia imejenga kaburi linalofanana na uzito wake ingawa Issa bin Mariamu hana kaburi duniani,” alisema Chifupa.

Pia alisema Amina alikufa akiwa vitani akipagania vijana wanaoharibika kwa kutumia dawa za kulevya na wale wanaosambaza dawa hizo.

Akizungumzia ugonjwa uliosababisha kifo cha Amina, alisema kuwa ni kisukari na ushirikina, na kuongeza kuwa kifo chake kimeharakishwa na watu ambao hivi sasa familia inaendelea na uchunguzi na mara baada ya kumalizika watatoa matokeo.

“Wakati Amina anaumwa alikuwa akitaja majina ya watu wazito ambao wengine ni viongozi na wafanyabiashara, hivyo tunafanya uchunguzi wetu wa kimya kimya kwa kuwa hatujui aliyataja majina yale kwa mazuri au mabaya, na tukimaliza tutayataja hapa hapa kutimiza maandiko yake,” alisema.

Luteni Chifupa alisema kuwa kaburi la Amina ni la kihistoria nchini kwa kuwa limejengwa kwa mfano wa kaburi la Shariff Musa ambaye ana makaburi saba duniani.
Amina ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifariki Juni mwaka jana.

?????????? Nilidhani weekend. Mapambo yakizidi nao huwa ni UCHAFU
 
Last edited:
tuwe macho na hizi fikra za ushrikina, zinalipeleka taifa mahali pabaya! fikra za ushirikina ndo chanzo cha mauaji ya wazee wetu vikonngwe huko shinyanga

kuhusisha kifo cha amina ambaye mnasema alikuwa kiruka njia(mimi sina uhakika) ni mwendelezo wa yale yale ya kutoamini kuwa mwenyezi MUngu, Bwana wa Majeshi, ndo mwamuzi wa uhai kutokuendelea.

Ripoti ya Kifo cha amina inaweze kupatikana wazi pale hospitalini alikokuwa amelazwa. ukiniambia ni nani aliharakisha kifo hiki ninaweza kusema kuwa ni huyu mzee, kwa kutompa nafasi mwanawe atoe mafundo yaliyokuwa moyoni

haya ya kujenga makaburi ya 3m nakadhalika ni kuchanganyikiwa,

hivy mumewe amina yule mtaka masifa sana, yuko wapi siku hizi? angekuja hapa ajibu.
 
Aache Kuropoka,akae Atulie,na Sasa Abadilike Aendane Na Umri Wake
 
ukweli ni kuwa vita dhidi ya madawa ya kulevya na vijana haijapata mpiganaji,
hayo mengine ni ubinadamu, tumsamehe mzee, ni mzazi na ana uchungu na mwanae kama mzazi mwingine yeyote.
VITA YA MADAWA JE?
 
Inaonyesha fungu aliloa ahidiwa na mafisadi kama rambi rambi hajapata ndo maana ameamua kukurupuka toka usingizini kama mnavyo ona...inabidi wamlipe jamani wamemuulia mwanae alafu wanamwacha mikono mitupu hii sio fair kabisa.
 
Mwogope Mungu, hujafa hujaumbika.
 
I have very low opinion of this old man. He is an opportunist and attention seeker. I think senile dementia is also setting in as well.
 
Aache Kuropoka,akae Atulie,na Sasa Abadilike Aendane Na Umri Wake

Angeanza kumchunguza huyo mkwe wake kwanza apunguze porojo.Anataka kuwa Mohammed al Fayed sasa ambaye alikuwa hataki kutulia kuhusu kifo cha Diana and Dodi mpaka the recent inquest ilipo mfunga mdomo?Akae chini amuombe Mola amweke peponi.
 
Akimfananisha Amina Chifupa na Yesu katika kuzaliwa anakosea, ila Kafananisha na Issa. Akimfananisha na Yesu katika kufa pia anakosea kwani Yesu alikufa baada ya kupigwa na kutundikwa Msalabani, huyu Amina alilazwa Lugalo Hospitali ya JWTZ. Asimfananishe Amina Chifupa na Yesu atakuwa anakufuru kwani huyu Dada aliishi maisha ya anasa sana. HATA HIVYO LALA PEMA AMINA CHIFUPA "Gonage uka-lambalala Amina Chifupa.:(
 
Amina hajazaliwa Lugalo, na zaidi ya hayo hakuzaliwa Dar es Salaam. Alizaliwa kijiji cha Lupembe au jina kama hilo huko Iringa. Na mimba yake kweli ilikuwa na mizengwe mizengwe.
 
".....????????..Mizengwe!!!????, Mama naomba unigee news hiyo vipi tena?
 
Yaani Mama Amina anasema alipokuwa na mimba ya Amina alikuwa akiumwa sana na kutapika damu. Madaktari walimshauri aitoe hiyo mimba, lakini kwa uwezo wa Mungu wakati wanafikiria kuitoa, mambo yakabadilika ghafla, mama mjamzito akapata nafuu. Na pia walijua atapata complications wakati wa kujifungua, lakini hakupata shida yeyote akajifungua salama na hata madaktari wakashangaa. Hivyo marehemu Amina alikuwa exceptional blessing kwa Mama yake, ingawa hii kila mzazi anaona mtoto ni blessing.
 
Back
Top Bottom