Vigogo walioficha fedha nje wabanwa; TAKUKURU yasema imeanza kuwachunguza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo walioficha fedha nje wabanwa; TAKUKURU yasema imeanza kuwachunguza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 17, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
  na Hellen Ngoromera | Tanzania Daima

  SIKU moja baada ya Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto, kutishia kuwataja vigogo wa serikali walioficha mabilioni ya fedha kwenye akaunti za nje ya nchi, ikiwa serikali haitawataja, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeibuka na kudai kuwa inazifanyia kazi tuhuma hizo.

  Zitto alisema kuwa wamepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu nchini na baadhi ya mawaziri wa serikali za awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizo zipatazo sh bilioni 314.5.

  Alisema sehemu kubwa ya fedha hizo zililipwa na kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi katika pwani ya Mkoa wa Mtwara, zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006, hivyo akaitaka serikali iwataje wahusika na kuwachukulia hatua, vinginevyo atawataja kwa majina.

  Hata hivyo, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah, jana alijitokeza katika Kipindi cha Baragumu kinachorushwa na kituo cha runinga cha Channel Ten na kusema kuwa tayari wameanza kazi ya kuchunguza tuhuma hizo.

  "Jambo lolote likituhumiwa lazima lifuate taratibu, TAKUKURU imeshawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu ndiyo mamlaka ya kuwasiliana na Uswisi, tufahamu ni kiasi gani benki za Uswisi zinacho na ni kina nani wamehusika, tumfuatilie nani amehusika na ufisadi huo na kupeleka hizo fedha huko," alisema.

  Alisema kwa sasa Uswisi wanayafanyia kazi madai hayo na wakikamilisha kazi hiyo watapeleka majibu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kisha TAKUKURU watajua maeneo gani ya kuyafanyia kazi.

  "Kumekuwapo na dhana kwamba hatuwafikishi mahakamani na kwamba kuna watu wametuhonga ili tusifanye hivyo; kama kuna ushahidi tutaachaje kumfikisha mtu mahakamani? Ni aibu kumfikisha mtu mahakamani halafu ionekane huna ushahidi, lakini tukubaliane kwamba kazi inafanyika," alisema Dk. Hoseah.

  Tuhuma kwa wabunge
  Kuhusu tuhuma za baadhi ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kudaiwa kujihusisha na rushwa, Dk. Hoseah alisema wanasubiri Bunge limalize kazi yake ndipo nao wafanye kazi yao.

  "Itakumbukwa kwamba Mheshimiwa Spika aliunda kamati ya kushughulikia yaliyojitokeza kwa baadhi ya wabunge, tutakachofanya ni kusubiri Bunge lifanye kazi yake," alisema.

  Alisema hatua zitachukuliwa lakini lazima wapishe kamati ya Bunge ifanye kazi yake kwanza.

  Alisisitiza kuwa wanasubiri ripoti ya kamati hiyo ambayo ilipewa wiki mbili imalize kazi yake ili iwasaidie kuona maeneo gani ya kuyafanyia kazi.

  "Sisi tunajikita zaidi kuona sheria ya kupambana na rushwa inavyokwenda, ikiwamo kuona kama kuna mtu alihongwa," alisema Dk. Hoseah.

  Alisema si kila tuhuma TAKUKURU inaweza kuibaini, lakini kuna zile ambazo wamekuwa wakizifanyia kazi ambapo tayari wameshaanza kuwahoji baadhi ya wabunge.

  Alisema taasisi yake haiwezi kutangaza kwa umma kila kitu, kwani sheria inawabana, kwamba wanapokuwa wanamchunguza mtu yeyote au taasisi hawaruhusiwi kwenda kutangaza.

  Gharama za uchaguzi
  Alisema taasisi hiyo inafanya kazi na hadi sasa kuna kesi 24 mahakamani zinazowahusu wanasiasa mbalimbali kudaiwa kuhusika na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.

  Alisema sheria hiyo ilianza kutumika mwaka 2010, dhana yake kubwa ni kuzuia vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi kwa kumzuia mgombea kutowarubuni wananchi kwa fedha ili washawishike kumchagua.

  "Mwanasiasa yeyote anapotaka kuingia kwenye ulingo wowote wa siasa lazima awe na fedha ili aweze kufanya hivyo, vitu vyote vinakubalika, lakini asichoruhusiwa kufanya ni kuwarubuni wananchi kwa zawadi, usafiri, chakula na mengine ili wamchague," alisema Dk. Hoseah.

  Pamoja na mambo mengine, alisema kuna haja ya kuangalia mfumo mzima kwa vyama vya siasa ili kumudu gharama za uchaguzi wakati wa uchaguzi.

  Aliweka wazi kwamba ni vigumu kushughulikia vitendo vya rushwa, kwa sababu ofisi za TAKUKURU hazijafika kwenye maeneo ya kata, bali wako kwenye wilaya.

  Alisema ili kuvidhibiti ni jukumu la wanasiasa wenyewe kuheshimu suala hilo kwa kuepuka kutoa rushwa.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi huu unachukua muda gani? Si uchunguzi unaohitaji wiki mbili tu? au ndio wamepata nafasi ya kupata imprest kusafiri mara kwa mara kwenda Switzerland kukusanya ushahidi halafu tutaambiwa uchunguzi uligharimu bilioni 10 au zaidi!!! Habari hii ilitoka tangu June 23rd, 2012 naamini kabisa ilikuwa imeshafahamika Serikalini mapema zaidi sasa kipi kinachochelewesha majina hayo kuanikwa hadharani?

  Home
   
 3. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Hii tasisi ni mzigo kwa walipa kodi! Mara nyingi hujishughulisha tu pale ccm inapotaka kuwaengua baadhi ya wagombe wakati wa chaguzi hapa nchini.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,814
  Likes Received: 83,212
  Trophy Points: 280
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wanachunguza nini????kwahiyo wanawafahamu hao watu au wanachunguza ili wawafahamu.

  Hosea na propaganda za mezani bana.!!!!!
   
 6. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  takukuru wanaendeleza rushwa siyo wanapambana rushwa hata wajinga wanalijua hilo kama kuna mtu ana rekodi ya kesi takukuru walizopeleka mahakamani wakashinda naomba atuwekee hapa
   
 7. t

  tenende JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tuna safari ndefu sana kuondokana na umaskini kwa mfumo huu!.
   
 8. S

  SIPIYU30 JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 686
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
  TAKUKURU and CCM have totally failed, wamebaki kuimba Chorus ya CHADEMA. Chadema wakiibua jambo wao wanadakia, haya, hizo story za Dr. Hosea ni alfa ulele,
   
 9. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wasipotaka kufanya kwa hiari yao, tutawalazimisha kufanya.
   
 10. M

  MKALIMOTTO Senior Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hosea angalia takukuru yako wilayani rorya, ni walevi na wala rushwa hakuna mfano. tafuta ushahidi shirati utaambiwa ni bei gani walihongwa kuiuza ccm katika uchaguzi mdogo wa madiwani, just a million!
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ni kama askari katika sinema za Kihindi, uhalifu unatendeka na kuisha wao ndo wanakuja baadaye!
   
 12. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kama unao si umpelekee?
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Dr. Hosea na taasisi yake ni mzigo mkubwa kwa walipa kodi. Hawana jipya la kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa letu zaidi ya kulinda wanaolitafuna. Ipo siku kila mtu atakuwa accountable kwa matendo yake. Nahisi yeye ndiye anayewalinda wala RUSHWA wakubwa.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu,
  Wala rushwa hawana tofauti na wale Magaidi waliolipua WTC na Pentagon ambayo ina ulinzi wa kufa mtu! Wanajua mbinu zote za kukwepa kugundulika na wamejiandaa vilivyo legally pale wanapogundulika!

  Kwahiyo, nionavyo mimi mfumo uliopo sasa kwa ujumla wake hauwezi ku-contain hii vita dhidi ya rushwa! Hata ikiletwa CIA au Mosad ndani ya mfumo uliopo itashindwa kufanya kazi!

  Pia kuna taasisi mbalimbali za Serikali ambazo ni mzigo:
  1. TRA - kushindwa kudhibiti ukwepaji kodi/rushwa,
  2. Polisi - kuua raia/rushwa/kushirikiana na wahalifu,
  3. Wanyamapori - Wanyama wetu kuroroshwa nje ya nchi,
  4. Ofisi ya AG - Mikataba yote mibovu imepitiwa na ofisi hii na kuonekana iko "ok!"
  5....

  Kwa hiyo hapa tatizo si kuiona Taasisi moja tu ndio "mzigo" kwa walipa kodi bila kufanya consideration of the whole Gvt setting!
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Buchanan umemaliza tatizo ni mfumo mzima wa serikali ya ccm..2015 tuwang'oe tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...