Vigogo wahaha kumwokoa Masha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wahaha kumwokoa Masha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,058
  Trophy Points: 280
  Wafanya vikao hadi usiku

  Baba yake atinga bungeni
  Na Saed Kubenea
  Mwanahalisi~Maslahi ya Taifa mbele​

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, ambaye katika misingi ya utawala bora angekuwa ameshajiuzulu au amefukuzwa kazi, sasa ameanza kukingiwa kifua, MwanaHALISI limeelezwa.

  Masha anakabiliwa na tuhuma nzito za kuingilia mchakato wa kutafuta mzabuni wa kutengeneza vitambulisho vya taifa katika mradi utakaogharimu zaidi ya Sh. 200 bilioni ulioko chini ya wizara yake.

  Waziri anadaiwa kubeba malalamiko ya kampuni ya nje iitwayo Sagem Securite na kuyatumia kujenga hoja ya kurejewa hatua za mchakato ili naye awemo.

  Katika wiki moja tangu kufumuka kwa taarifa za waziri huyo kuingilia mchakato, Masha ameripotiwa kuwa katika wakati mgumu kwa kuwa suala lake ndilo limekuwa "gumzo la Dodoma."

  Hakuna taarifa zozote juu ya alichokisema Rais Jakaya Kikwete alipokutana na Baraza la Mawaziri mjini Dodoma, lakini taarifa zisizo rasmi zinasema alidokeza juu ya "mwenendo wa baadhi ya viongozi na misingi ya maadili ya uongozi."

  Aidha, kuna taarifa kuwa waziri Masha amekwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kukutana naye. Haijafahamika ilikuwa matembezi ya kawaida, kikazi au safari mahsusi ya "kutafuta kinga" kutoka kwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

  Bila ya kutaja majina, mbunge wa kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru, alikiambia kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kuwa "waweke mbele maslahi ya chama."

  Ngombale-Mwiru amenukuliwa akisema kuna wanaosema "maslahi ya taifa kwanza." Alisema sharti waweke maslahi ya chama mbele na kwanza.


  Hoja yake ilionekana kama majibu ya hoja nyingine kuwa kashfa inayomkabili Masha, inaweza kuwa mtaji mkubwa kwa vyama vya upinzani; na kwamba wabunge wa CCM wasiposimama pamoja, basi chama kitabomoka.

  Wachunguzi wa siasa za CCM wanasema kauli ya Ngombale-Mwiru ni sehemu ya vitisho kwa wabunge na hata karipio kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa kitabu alichozindua (ambamo kuna sura aliyoandika) kiitwacho Bunge lenye meno ambacho kinasisitiza utaifa kwanza.

  Hadi tunakwenda mitamboni, Kamati ya bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambayo ilipewa jukumu la kushughulikia hoja ya Masha kuingilia Bodi ya Zabuni ilikuwa haijatoa taarifa zozote kwa spika.

  Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi ilitakiwa kusikiliza hoja binafsi ya mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa juu ya tuhuma dhidi ya Masha na hatimaye kuwasilisha matokeo kwa spika.

  Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya kamati zinasema wajumbe wake wamegawanyika kuwili. Upande mmoja unataka suala hilo lipelekwe bungeni na wengine wanataka liishie kwenye kamati.

  Kinachofanya baadhi waogope hoja hiyo kwenda bungeni ni hofu ya kuundwa kwa Kamati Maalum ya kuchunguza tuhuma na hatimaye kuja na hitimisho kama lililomkumba aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.

  Naye baba yake Masha ambaye ni mbunge wa Baraza la kutunga Sheria la Afrika Mashariki, Dk. Fortunatus Masha, ameripotiwa kuwapo mjini Dodoma akikutana na baadhi ya wabunge na viongozi mbalimbali.

  Taarifa zimeenea mjini Dodoma kuwa Dk. Masha amekuwa akiwaomba wabunge na viongozi wengine kumnusuru mwanae.


  Waziri Masha anataka kukwepa, pamoja na mambo mengine, tuhuma za:

  Kujipatia taarifa za maandishi juu ya mchakato wa zabuni wakati yeye siyo mjumbe wa Bodi ya Zabuni.

  Kulalamikia hatua za Bodi ya Zabuni wakati yeye hayumo katika mlolongo wa wahusika.

  Kutumika kama mlalamikaji wa mmoja wa wazabuni kutoka nchi ya nje kiasi cha kufikisha kilio kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Kushinikiza Katibu Mkuu wa wizara yake kutafuta ushauri wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi serikalini (PPRA) wakati suala hilo halihitaji kufikishwa huko katika hatua ya sasa.

  Kutawanya taarifa za Bodi, ambazo haziko mikononi mwake kihalali, kwa waziri mkuu, katibu mkuu wa wizara yake, katibu mkuu kiongozi na PPRA.

  Kujadili mambo yaliyomo katika Bodi ya Zabuni ambayo bado hayajatangazwa na hivyo kuingilia uhuru wa Bodi.

  Kushindwa kufuata sheria ya ununuzi kwa kupokea taarifa za malalamiko, kama anavyodai katika barua kwa waziri mkuu, na kukaa na taarifa hizo bila kuziwasilisha kwa Bodi ya Zabuni.

  Kushindwa kufuata misingi ya utawala bora ya kutofanya au hata kuonyesha upendeleo.


  Taarifa zilizopatikana Jumapili jijini Dar es Salaam zinaendelea kumshindilia Masha kwenye tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

  Inadaiwa kuwa Oktoba mwaka jana, alikwenda Geneva, Uswisi kuhudhuria mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi ambako baada ya mkutano, alipata wasaa wa kukutana na wenye kampuni ya Sagem Securite.

  Imefahamika kuwa Masha aliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya kampuni ya Swissair. Mjini Geneva alikutana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Jean Lin Fournereaux hapo 5 Oktoba 2008 kwa muda wa saa mbili kuanzia saa 12 jioni.

  Taarifa zimeeleza kuwa Masha alifikia chumba Na. 0306 katika hoteli ya Mandarin Oriental na kutembelea ofisi za Sagem siku iliyofuata, katika eneo la Max Schmidheiny, Mtaa 202 CH 9435 Heerbrugg, mjini Geneva.


  Naye Dk. Slaa, mwenye hoja binafsi juu ya waziri Masha kuingilia mchakato wa zabuni, aliiambia MwanaHALISI juzi Jumatatu kuwa kwa kuwasilisha hoja hiyo kwa spika, ametimiza wajibu wake na kwamba anasubiri jibu.

  Kanuni za Bunge Na. 47 na 48 zinasema spika akiridhika, hoja binafsi yaweza kuwasilishwa bungeni. "Mpaka sasa hajanijibu," amesema Dk. Slaa.

  Mfumuko wa pilikapilika za kumtetea Masha ulianza pale Dk. Slaa alipoweka wazi kwamba ataomba maelezo bungeni kuhusu waziri kuingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho.

  Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila aliiambia MwanaHALISI juzi kuwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilitarajiwa kuendelea na kikao chake jana na kupeleka ripoti yake kwa spika.

  Alikataa kusema hatua gani imefikiwa hadi juzi na kuongeza kuwa shughuli za kamati hiyo ni za siri. Mkutano wa 14 wa Bunge unamalizika leo.

  Wakati tuhuma dhidi ya Masha kuhusu kuingilia mchakato wa zabuni zingali mbichi, kampuni binafsi nchini imetishia "kumlazimisha kufuata sheria."

  Kampuni ya Power Roads (T) Limited inamtuhumu Waziri Masha kufuta amri ya Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji ya kumwondolea uhalali wa kuishi nchini Mwingereza aitwaye Douglas Hume Claxton.

  Mkurugenzi wa Uhamiaji alifuta kibali cha Claxton, Daraja A Na. 018076 cha 30 Oktoba 2007, kwa barua Kumb. Na. 272673/31 ya tarehe 15 Septemba 2008, ambayo MwanaHALISI imeona.

  Mkurugenzi amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa Claxton alipata kibali cha kuishi nchini kwa kutumia hati batili na iligundulika kuwa baada ya kupatiwa kibali, alikuwa akifanya kazi zisizolingana na kibali chake.

  Lakini katika hali inayotia shaka, Waziri Masha alifuta amri hiyo ya Mkurugenzi wa Uhamiaji na badala yake akaruhusu Mwingereza huyo abaki nchini hadi sasa.

  Katika barua yake Kumb. Na. DN 272673/32 ya tarehe 15 Oktoba 2008, Mkurugenzi wa Uhamiaji anamweleza Claxton juu ya uamuzi wa waziri.


  Anasema, "…waziri ameelekeza kwamba uendelee kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia hati hiyohiyo na kwamba mahakama ndizo zilizomo katika nafasi nzuri ya kushughulikia matatizo na migogoro inayokabili Power Roads (T) Limited."

  Barua ya mkurugenzi imesainiwa na M.P. J. Ulungi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uhamiaji.

  Hoja ya Power Roads kwa waziri, kupitia barua Kumb. Na. proads/08/16 ya 21 Oktoba 2008, ya kupinga hatua yake na kusema watahakikisha wanamlazimisha kufuata sheria, haikujibiwa hadi jana.

  Baada ya kuona hawapati majibu, kampuni imemwandikia Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani na kumwomba afikishe nakala ya barua yao ya awali kwa waziri.

  Katika barua hiyo, Kumb. Na. roads/09/01 ya 22 Januari 2009, kampuni inamwomba Katibu Mkuu kuwasilisha nakala ya barua yao kwa waziri kwa kuwa yeye, katibu mkuu, "ni mtekelezaji wa utawala bora, mu-wazi na muwajibikaji."

  Barua hiyo imesainiwa na Abba P. Mwakitwange, mkurugenzi na mwenye hisa 51 katika kampuni hiyo.
   
  Last edited: Feb 13, 2009
 2. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mungu Ibariki Tanzania na watu wake. Walaani wale wote wanaoshabikia, kujenga na kuubariki ufisadi.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa kuna dili tu ,aidha mtandao wa Slaa umezidiwa kete ndio mambo yakaja juu ,pengine mtandao wa Slaa ambao upo serikalini umeona donge la fedha lililoahidiwa ikiwa zabuni itapata kampuni wanayoijua wao watalikosa kama Masha akifanikiwa kuinyakuwa zabuni na kuipeleka kwa sagem na kushinda ,natumai kuna ile bahashishi au kiasi fulani cha takirima kinachotunikiwa watu fulani wanaosaidia kushinda zabuni ambacho kitu hiki kiligusiwa katika ununuzi wa rada ila donge la rada lilipita mipaka na kuonekana si takirima tena bali ni rushwa ,nwakilisha kuwa hapa kuna mapambano ya kuwania takirima ,upande wa Slaa ukishinda basi nae Slaa atakatiwa chake ,wasijidai kuwa wanafuata sheria na kuwa wawajibikaji ,ilatakirima ndio inawafanya watu waonyeshane ubabe kwa kila mmoja kwa upande wake.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mhhhhhhhhh Huyu kijana wanamuacha uchi sasa !
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo wewe hutakia sheria ifuatwe.
  Sheria ifuatwa no matter nani anafaidiaka acha speculation
   
 6. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo unataka kutuambia nini hasa katika hili?
   
 7. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Natafakari mara nyingi nashindwa kupata majibu sahihi.Ni nini hasa kimelikumba taifa letu,mbona zile akili za kibinadamu nilizozizoea sizo zinazofanya kazi sasa.Kilichokuwa straight forward wakati ule mbona sio straight forwad sasa?Lakini nini hasa kinaendelea?Kwa akili za kawaida kabisa Masha hafai tena kuwa kiongozi.Tuhuma zake ni nyingi mno.He completelely lacks the confidence of even the very normal citizen.Lakini anacho ng'ang'ania hasa ni nini ,kuendelea kutuibia,it's ridiculous.
   
 8. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tikerra ndugu yangu, ni kweli kuwa common sense inaelekea kutokuwa na maana kabisa katika jamii yetu siku hizi. Inaweza kuwa hivyo kwa bahati mbaya ama kwa makusudi. Sijui lipi kati ya hayo mawili ni sahihi (time will tell).

  Mimi kinachonisikitisha zaidi ni kauli za kushangaza ambazo naona zinaanza kujitokeza kutoka kwa viongozi wa kutegemewa kabisa katika Taifa letu. Kauli za kuweka mbele maslahi ya chama badala ya Taifa, kauli za kuvunja sheria/Katiba bila kujali. Kauli ambazo dhahiri zinaonyesha kutojali mkataba kati ya chama kinachotawala na wananchi, viapo mbalimbali viongozi wetu walivyoapa mbele ya Taifa baada ya kupewa ridhaa ya kuliongoza Taifa na kadhalika.

  Ngugu zangu, mimi nashangaa sana na mara nyingi hujiuliza kama kweli CCM ina nia ya kuendelea kuliongoza Taifa hili zaidi ya mwaka 2010. Maana kama nia bado ipo, dalili hizi ni kinyume cha nia hizo. Tanzania ni ya wote, labda kweli umefika wakati wa kujaribu kwingine, maana sidhani kama huko nako watavunja sheria/Katiba na kudharau viapo vyao kwa kiasi hiki.

  Mimi ni mwana CCM, ila ninasikitikshwa sana na mwenendo huu wa kutojali. Kama alivyosema/kumaanisha Hayati Mwl. Nyerere (Baba wa Taifa), CCM si mama yangu, na ninaweza kuiacha kama itaendelea kufanya yasiyofaa. Kauli kama hii ilitolewa si kwa maslahi ya Chama bali kwa maslahi ya Taifa na sisi wote ni vyema tukatenganisha haya mawili. Chama pia ni lazima kiwe kwa maslahi ya Taifa na si vinginevyo. Vinginevyo kitakuwa kinyume cha Katiba na hakitafaa kuwepo tena.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani maslahi ya chama ni muhimu kuliko maslahi ya taifa? Huyu ndiye Kingunge Ngombale Mwiru anayejifanya gwiji la political science? Mungu atunusuru na myopicism ya CCM.
   
 10. M

  Maps Member

  #10
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii nchi inaelekea kubaya sasa. Tumesikia mengi sana kuhusu Masha, Magazeti yanamwandika sana. Ukweli hakuna anaeujua kwa kuwa Masha hajasimama kujubu tuhuma yoyote dhidi yake, nadhani kama hoja ya Slaa ingewkenda Bungeni tungejua ninani mkweli kwa sababu kinachoonekana hapa ni kama akina Mengi na Kubenea wanataka kutuaminisha kwa nguvu kuwa Masha kasosea na anahaha kujiokoa. Masha kwenda kwa Waziri Mkuu ni ajabu? Kama ameitwa hata kwa issue nyingine mlitaka asiende? Baba yake ni kosa kwenda Dodoma katika mazingira yanayomhusu Mwanae? Hata ungekuwa wewe ungeenda kujua ukweli ni upi? Nadhani tupime tunachosoma, si kila tunachoandikiwa tukisome na kuamini kama kilivyo. Naamini Katika Mawaziri Matajiri wasio na njaa ni pamoja na Masha ambaye leo hii hata akiacha Uwaziri staili yake ya maisha haitabadilika tofauti na Mawaziri wengine ambao tangu wamekuwa Mawaziri hawajawahi kutumia magari yao binafsi. Ipo siku tutajua ukweli badala ya kuendelea kulishwa kasa na akina Kubenea, Mengi na Rostam
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tajiri ndie anaependa pesa kuliko masikini. Kadiri mtu anavyozidi kuwa tajiri, ndivyo maisha yake yanavyokuwa yakihitaji pesa nyingi zaidi na ndivyo anavyozidi kuwa mlafi. Matajiri kote duniani ndio chanzo cha rushwa kubwa na wanajua jinsi ya kutumia pesa zao kujifunika.

  Masikini akipata chochote huridhika. Wakati tajiri anataka apate anachopenda yeye. Hapo ndipo matatizo makubwa yanapoanzia. Tajiri haridhiki hata mara moja.
   
 12. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hapa jamani maslahi ya Taifa mbele;unajua kuna watu wengine waajabu sana,unapewa madaraka kwaajili ya kuwatumikia wananchi badala yake unafanya vitu kama unavyotaka wewe!Kila kazi inatakiwa ifanywe kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sheria inavyoelekeza.
  Nashangaa watu wanaacha kazi zao kwa maslahi ya Taifa halafu wanaenda kumtetea mpinzani wa Taifa;watu wa aina hii wanahitaji check-up kama akili zao ziko sawasawa.Unajua unaweza kudhania mtu yuko timamu kumbe mwenzio fuse, mshipa wa aibu vimekwisha achia siku nyingi.Matokeo yake,anaanza kufanya mambo ya ajabu!

  Hawa wapinzani wa maendeleo ya Taifa hili wanahitaji adhabu kali sana ili iwe fundisho kwa wafuasi wao, hatua ya kwanza: kuwafilisi, na mwisho kitanzi hadi kifo/snipers watumike katika hatua hii nafikiri ndiyo watu akili zitawakaa sawasawa na kuweza kutoa maamuzi sahihi;vinginevyo longolongo mtindo mmoja.
   
 13. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  BUT why is Kingunge still thr? the fact is: he is useless old fella and selfish period!!
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Maslahi ya chama yanatakiwa kurandana na maslahi ya taifa, vinginevyo chama ni cha mabazazi.

  Kingunge anakubali wazi kabisa kwamba CCM haijali maslahi ya taifa, inataka kuendelea kutawala tu.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hili lathibitisha kitu kimoja tunachokisema kila mara - adui mkubwa wa taifa letu ni CCM. Halafu kuna anayethubutu kusema CCM ni safi ila bla bla bla.

  Kwa kuzima hoja za kupambana na MAFISADI, wabunge wote wa CCM kwa umoja wao na wakiongozwa na Waziri Mkuu, wakilindwa na Spika wa Bunge na wakishauriwa na kada/gwiji/mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wameamua kulinda na kutetea UFISADI.

  Swali la kujiuliza ni hili - Mbona mpaka sasa hatujasikia hao walio wasafi ndani ya CCM wakilalamikia huo uamuzi ?
   
 16. Chibidu

  Chibidu JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 387
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa wabunge wanapoapishwa huwa wanaapa kulinda maslahi ya Chama ama taifa?. Kuna maana gani basi mtu kutoa kiapo ambacho una hiari ya kukitekeleza ama kutokitekeleza?. Naona muda umefika wananchi wenye hasira na nchi yao waanze kumkemea Ngombale-mwiru ili akae pembeni aache watu wenye uchungu na nchi wafanye kazi zao na yeye aendelee kuimarisha chama akisubiri Mwenyezi Mungu atakapomwita kwake kwa mahojiano
   
  Last edited: Feb 13, 2009
 17. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kawa kamanda wenu CDM

   
 18. A

  Ally maganga JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2017
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 669
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 80
  hatareeee
   
 19. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2017
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,885
  Likes Received: 266
  Trophy Points: 180
  Finally Kingunge Ngombale Mwiru amekaa pembeni.
   
 20. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180

  2015 aligeuka kamanda
   
Loading...