Vigogo wafurika Arobaini ya Bilionea Mathias Manga, ajengewa mnara wa kihistoria

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Baadhi ya wafanyabiashara wa madini, wanasiasa akiwemo mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha juzi walishiriki hafla ya kuadhimisha siku 40 ya kifo cha aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini na mwekezaji wa hoteli za Goldcrest Arusha na Mwanza marehemu Bilionea Mathias Manga.

Marehemu Mathias Manga alifariki mwezi Agosti mwaka huu nchini Afrika ya Kusini baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo na kisha kuzikwa nyumbani kwao eneo la Manyire mkoani hapa.

Akizungumza katika hafla hiyo mbunge wa jimbo la Monduli, Fred Lowasa ambaye alimwakilisha baba yake alisema kwamba marehemu Manga alikuwa mchangiaji wa shughuli mbalimbali kwenye jamii na alijitoa kwa nafasi yake hivyo wao watayaenzi mema yote aliyofanya.

“Ni pengo gumu sana kuzibika katika mazingira ya kawaida kutokana na mchango wake ndani ya jamii sisi tutayaenzi mema yote aliyofanya “alisema Lowasa

Naye Paroko msaidizi wa Parokia ya roho Mtakatifu katika kanisa la Katoliki Ngarenaro, Padri Karduni Olelesirkon alisema kwamba kanisa limepoteza muumini ambaye alipenda kujitoa katika kusaidia shughuli mbalimbali za kanisa.

Padri Olelesirkon alisema kuwa pamoja na kanisa kumpoteza muumini wake mahiri lakini aliwataka wanafamilia kuendeleza tabia ya kujitolea kusaidia shughuli za kanisa kama njia ya kumuenzi marehemu.

“Marehemu mpaka anafariki alikuwa Mwenyekiti wa ujenzi wa kanisa hakika kanisa limepoteza muumini wake ambaye alipenda sana kujitolea “alisema Padri Olelesirkon

Brayan Manga ambaye ni mtoto wa marehemu alisema kwamba wao kama familia wamepoteza mtu muhimu sana kwenye familia yao lakini watahakikisha wanayaenzi mema yote aliyoyaacha ikiwa ni pamoja na Mali sanjari na miradi mbalimbali alizokuwa akizimiliki.

"Miradi yote iko kwenye mikono salama sisi kama familia tutahakikisha tunasimamia kwa uhadilifu kama njia mojawapo ya kumuenzi baba yetu" alisema Brayan

Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilayani Arumeru, Neema Mollel alisema kwamba chama kimempoteza kada wake muhimu sana ambaye alikipambania kwenye mazingira magumu.

"Chama kimepoteza kada wake muhimu sana ambaye mbali na kuwa mlezi lakini alikisaidia katika mazingira magumu kwenye kampeni mbalimbali" alisema Mollel

Naye mmoja wa familia ya marehemu, Jerome Kilave maarufu kama "jombii" alisema kwamba wao kama familia wameamua kutengeneza mnara wa kumbukumbu kwenye kaburi la marehemu kama njia mojawapo ya kumuenzi marehemu.


Mwisho.


IMG_20211003_144639_841.jpg
IMG_20211003_150701_969.jpg
IMG_20211003_153551_854.jpg
IMG_20211003_150308_983.jpg
 
Ni pengo gumu sana kuzibika katika mazingira ya kawaida kutokana na mchango wake ndani ya jamii sisi tutayaenzi mema yote aliyofanya “alisema Lowasa
Pengo huku kuna kreti nyeusi na chupa za brown😆😆
 
Wewe kilaza hao ndo vigogo? Mnapenda sana kujisifu utajiri! Huyo Manga mwenyewe alikuwa mpangaji tu kwenye majengo ya mashiriki ila mnavyopenda sifa za kijinga bilionea ndo nini?
Wewe humfahamu Marehemu, alikuwa bilionea wa kweli, wa fedha na roho
 
Maneno ya Padri ndio ya muhimu, tuwahimize wanafamilia waliobaki wasiache kutoa fungu alilokuwa analitoa marehemu kanisani.
 
Kwanza ningeshangaa nisingewaona sisiyemu kusifia wamepoteza mwanachama, ila kwa hamza hawakwenda kusifia.

Ila kanisa letu mtu akiwa na hela ndio anakua mwenyekiti wa ujenzi. Ata kaka hasali nyumbani kwake paroko na mapadri hawakatiki
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom