Vigogo waficha bilioni 300 Uswisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo waficha bilioni 300 Uswisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 26, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  Rais wa Shirikisho la Polisi Duniani(Interpol) Bw. Khoo Boon Hui

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 25 June 2012 21:43 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwandishi Wetu

  KITENGO cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kinachunguza Sh303.7 bilioni ambazo zinadaiwa kukutwa kwenye akaunti sita za Watanzania, wakiwamo wanasiasa, katika benki mbalimbali nchini Uswisi.

  Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Interpol kilichonukuliwa na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, kimesema baadhi ya wanasiasa nchini na watu wengine ndiyo wanahusika na ufisadi huo kwa kuwa na akaunti zenye fedha nyingi nchini Uswisi.
  Fedha hizo zimeelezwa ziliingizwa katika akaunti hizo na kampuni za uchimbaji mafuta na kampuni za uchimbaji madini, ambazo zinafanya kazi Tanzania.

  Chanzo hicho kiliongeza kwamba fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti, zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa.

  Kiasi hicho cha fedha kilichofichwa Uswisi, kinatosha kuendesha Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa miaka mitano, au kusaidia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kuendesha shughuli zake kwa miaka miwili.

  Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

  "Wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini," kilidokeza chanzo hicho.

  Mabilioni hayo yamebainika kufichwa wakati takwimu zilizotolewa na Umoja wa Taasisi za Kupambana na Rushwa barani Afrika ikiwamo Tanzania, zikionyesha kwamba Sh22 trilioni, zimekuwa zikitoroshwa nchini humo na kufichwa katika nchi za kigeni, ikiwamo Uswisi.

  Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikibainisha nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zake zilizohifadhiwa huko.
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hivi sasa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki.

  Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.
  Jumla ya fedha zilizoko katika benki za Uswisi kutoka nchi hizo nyingine za Afrika ni Faranga 1.53 trilioni za nchi hiyo na ripoti hiyo imeelezwa kuwa kuna msukumo wa kimataifa wa kuitaka nchi hiyo izitake benki zake, kubadilishana taarifa za wateja na serikali za kigeni.

  Ripoti hiyo imekuja wakati pia Uswisi ikiwa na rekodi ya kuhifadhi mabilioni ya dola kutoka nchi za kigeni ikiwamo Afrika, kwani iliwahi pia kuhifadhi dola zaidi ya bilioni 1.5 za aliyekuwa Kiongozi wa Kijeshi wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha na dikteta Mobutu Seseseko wa iliyokuwa Zaire.

  Gavana azungumza
  Akizungumzia ripoti hiyo, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Beno Ndulu (pichani) alisema uamuzi huo wa Uswisi wa kuanza kufungua milango utaiwezesha BoT kuwa na rekodi ya kiasi halali cha fedha zilizopo katika nchi hiyo.

  Profesa Ndulu alifafanua kwamba katika siku za nyuma, Uswisi haikuwa imefungua milango kwa kutaja kiasi cha fedha za wateja wake walioweka fedha katika benki zake, hivyo ilikuwa vigumu kwa mamlaka za ndani kuweza kufanya uchunguzi.

  "Ndiyo kwanza wameanza kufungua milango, sisi siku zote tulikuwa hatuwezi kujua nini kinaendelea. Lakini, angalau sasa tutaweza kujua na kuwa na rekodi baada ya uamuzi huo wa kufichua kiasi cha fedha kilichomo katika benki zake," alifafanua gavana.
  Kiutaratibu, BoT inapaswa kuwa na rekodi ya fedha halali za Watanzania zilizopo nje ya nchi.

  Kauli ya Takukuru
  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alikaririwa na The Citizen hivi karibuni alisema kuwa ofisi yake ina taarifa kuhusu suala hilo na kwamba wanaanza mawasiliano na Serikali ya Uswisi kujua ukweli wake.

  Dk Hoseah alisema taasisi hiyo inataka kujua jinsi gani fedha hizo ziliwekwa kwenye benki za Uswisi, watu waliohusika na namna uhamishaji wa fedha hizo ulivyofanyika.

  "Tutakapogundua fedha hizo zimetoka wapi, tutafuata taratibu zinazohusika kuhakikisha zinarudi nchini," alisema Dk Hoseah na kuongeza: "Tutatumia sheria zilizopo katika nchi hizi."

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa yuko likizo, hivyo aulizwe msemaji wa Jeshi la Polisi.
  Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema hawajapata ripoti hiyo na kwamba atawaomba watu wa uchunguzi kumpatia, ili aweze kutoa taarifa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Takukuru hawana uwezo wa kufuatilia hizo fedha,kauli ya Hosea ni ya kitoto sana,ya humu ndani yamemshinda itakua hiyo ya nje?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana amesema kuwa kuwakamata papa ni issue,na hizo pesa walozijua ni waswizi,sasa tutarajie nini na ikiwa wanasiasa ndo waloziweka???jaman,mafuta hata hatujaanza kuyatumia watu wanakula je tungeanza kuyapata?????
   
 4. d

  dguyana JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ni mapapa wakubwa Takukuru haiwezi kuwafungulia mashtaka labda Yesu arudi. Takukuru ni ya vidagaa tu kama mwenyewe Hosea alivyosema.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  naungana na wewe,,,,mdau
   
 6. e

  evoddy JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni zaidi tuijuavyo,ipo siku Mungu atafungua milango na kuwaacha uchi wezi wetu na hapo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.

  Ee MUNGU TUOKOE NA HILI BALAA LA WEZI WA RASILIMALI ZETU
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sosi:D DAKIKA 45 ITV
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwa sasa nikisikia stor za billions nahis kawaida tu tangu epa
   
 9. IFUNYA

  IFUNYA JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  GIP komboa hizi pesa zetu kama ulivyofanya kwenye pesa za RADA tutakukumbuka sana.
   
 10. IFUNYA

  IFUNYA JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Rekebisha badala ya GIP weka IGP
   
 11. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mbona siku nyingi alishafungua Milango ila WTZ tu ndiyo bado gizani kugundua kwamba Mlango uko wazi.Hivi siku mkuu wa Jamhuri alipowawekea kifua wezi wa EPA siyo kwamba ilikuwa ishara ya Mlango kuwa wazi?.
   
 12. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,648
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ha haaa hii nchi sijui tunaelekea wapi,viongozi wetu wengi ni wezi na wabinafsi wakubwa, sasa mabilioni yote hayo ya nini umeyaficha hata hauyatumii na kuyafaidi, lets stickto the basic mtu moja anahitaji gari moja zuri la maana,nyumba moja nzuri ya maana na kitanda kimoja na ka account ka benki kenye vimilioni kadhaaa, ziadi ya hapo ni uibilisi tu.
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi ni kwa nini watanzania wanaruhusiwa kusoma darasa moja na wazungu(walioendelea)?
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,597
  Likes Received: 4,715
  Trophy Points: 280
  Wengi hatukumwelewa Gamba Chenge aliposema zile bilion mbili zake kule ughaibuni ni vijisenti tu, sasa hapa picha iko wazi bila chenga viongozi wa Tanzania ni mafisadi kupindukia na kusema kweli nawashangaa watanzania wenzangu walala hoi wanaowashabikia hawa mafisadi wanaondelea kushikilia ofisi za umma.Lakini ipo siku haya yatafika mwisho na ole wao.
   
 15. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Said Mwema, Chagonja na huyo rais wa interpol pichani nilidhani ndo wanaongelea pesa za Uswisi!!!
   
 16. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Kinachoniuma sana hapa si watanzania kuwa na kiasi hicho cha pesa kwenye benki za nje. Kinachouma ni jinsi hizi pesa zilivyoingia. Kama na sekta ya mafuta imeanza kimizengwe kama hivi, basi, dawa iliyomroga mtanzania awe maskini ni ya milele.
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Binafsi nilimwelewa. Alimaanisha kwamba, ile bilioni yake moja si kitu mbele ya hizo rushwa za madini. Unadhani kiburi cha akina Ngeleja kugoma kujiuzulu kiklitoka wapi enzi hizo?
   
 18. S

  Semlamba Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote litakalo fanyika zaidi ya kulindana. Yale mapesa ya EPA yako wapi? Na waliohusika wamechukuliwa hatua gani? Ikiwa wale wezi wa EPA majina yao hayajulikani hadi leo hata kwa hili pia hakuna la maana litakalo fanyika zaidi ya kulindana.
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Duuh yaani mafuta yenyewe tunaambiwa hayagunduliwa tayari watu wameshaanza kumega keki ya taifa (yaani kula dividend ya mafuta kwa niaba yetu) kimya kimya. Au mafuta yanachimbwa tayari na sisi hatuna habari?
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Ni kwa sababu college fees za mtanzania mmoja zinatosha kuwasomesha wazungu watatu huko kwao. Kwa hiyo unaruhusiwa ili ukamuliwe vijihela vyako vidogo ulivyonavyo.
   
Loading...