Vigogo wachunguzwa ufisadi wa Sh86 bilioni IPTL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wachunguzwa ufisadi wa Sh86 bilioni IPTL

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Feb 7, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  SERIKALI inawachunguza baadhi ya maofisa wake waandamizi kwa tuhuma za wizi wa dola50 milioni za Marekani sawa na Sh86 bilioni, zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa mafuta mazito ya kuzalishia umeme kwa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), katika kipindi hiki nchi inapokabiliana na tatizo la uhaba wa nishati hiyo.

  IPTL inayozalisha megawati 100 za umeme iliingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco), lakini utendaji wake umekuwa na mkanganyiko.Chanzo kutoka serikalini kililiambia gazeti dada la The East African la Februari 12, kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwamba baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Hazina na Tanesco, wanahusika katika mpango huo wa wizi.

  Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alipoulizwa alijibu, “Ndiyo naweza kuthibitisha upo uchunguzi unaoendelea, lakini ndiyo kwanza upo katika hatua za awali.” Tayari taarifa za awali za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), zinaonyesha kumekuwa na maelezo yaliyokiuka utaratibu wa fedha zilizolipwa na Serikali kwa ajili ya usambazaji wa mafuta mazito kutoka kampuni za ndani.

  Ukosefu wa nishati ya umeme unaoikabili nchi kwa sasa unaifanya Tanesco kulipa IPTL dola12 milioni za Marekani sawa na Sh19.2 bilioni kila mwezi, kwa uzalishaji wa megawati 60 badala ya megawati 100.

  Mwaka 1995, Tanesco iliingia mkataba na IPTL, mkataba ambao uliihusisha kampuni ya nchini Malaysia , Mechmar Corporation na wawekezaji wa ndani, na VIP Engineering and Marketing Company kwa ajili ya kuzalisha megawati 100 kwa kutumia mitambo inayotumia dizeli kwa miaka 20.Katika mkataba huo, VIP ina hisa ya asilimia 30 na ile ya Mechmar ya Malaysia ikiwa na hisa ya asilimia 70.Serikali ilikubali kulipa kwa ajili ya uzalishaji huo kwa kuwa haikuwa na njia nyingine.

  Mpango wa kuifilisi IPTLTayari hivi karibuni Mahakama iliamua IPTL ifiilisiwe na jukumu hilo lilikabidhiwa kwa Wakala wa Ufilisi, Vizazi na Vifo (Rita).Hata hivyo, baadhi ya benki zinazoidai IPTL ziliweka zuio mahakamani zikitaka kwanza kulipwa fedha zao ambazo kampuni hiyo ilikopa.IPTL inakadiriwa kuwa na Sh200 bilioni zilizopo Benki Kuu (BoT) ambazo kama ikifilisiwa zingeangukia mikononi mwa Serikali. Kampuni hiyo imekuwa ikiitafuna Tanesco mabilioni ya shilingi tangu kuingia mkataba huo ambao umekuwa ukitajwa kama wa kifisadi, kuliko hata wa Richmond. Ends

  Hivi huu ufisadi utaisha lini nchi hii jamani??na hao wanatuibia wanaishi wapi??mbona hatujawahi wakamata??mimi nadhani kuna haja ya kuhoji huu uvumilivu wetu mana nahisi tumerogwa, nini tufanye kukabiliana na UFISADI??
   
 2. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  huyu jamaa aitwaye tanzania ameliwa sana hadi amebakia mifupa tuuu,na hata mifupa nayo inatafutwa kwa mbinde..... duh!Mungu atunusuru watz na hao mafisadi mafisi
   
 3. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mtu akishtakiwa maana yake IMEBIDI ashtakiwe. Serikali yeyote worth it's salt inatakiwa kuwa makini na kuchukua hatua zinazostahili kuhakikisha watuhumiwa wa uhalifu wa aina yeyote wanafikishwa mbele ya sheria.
  Naelewa upo kazini kwa hivyo ni wajibu wako kuleta "sread" kama hii. lakini hebu tufafanulie: kama serikali hii iko makini kama unavyojitahidi kutuaminisha iweje wahusika wa tuhuma zenye ushahidi hawapelekwi mahakamani? Hapa naongelea kwa uchache Kagoda, Meremeta na ununuzi wa rada (achilia mbali IPTL ambayo huyo uliemsifia alishiriki kwa kiwango kikubwa kufanikisha mkataba wake akiwa waziri wa nishati na madini).
   
 4. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni kama gari bovu lilowekwa juu ya mawe! Karibu itashindikana hata kulifufua. Sijui litatupwa wapi!
   
 5. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hebu tutajie waliofungwa.
  Pia unajua hii nchi imeshafilisika?https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/220818-government-in-cash-crisis-says-kikwete.html
  Kukumbuka neti wakati mbu wameshakutafuna na asubuhi imefika ni ujanja?
   
 6. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waziri mwenyedhamana,wizara na serikali iliyo madarakani ni mzigo kwa watanzania, mpaka nathubutu kusema ccm na serikali yake ni janga la kitaifa. Nchi imekuwa shamba la bibi, watu wanachuma, no one to sentenced. Days are numbered. God bless revolutionalists.
   
 7. mshana org

  mshana org JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 2,102
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kw tarifa yako pia naomba kukumbusha kua waheshimiwa.zitto,j makamba, mnyika waliwahi kuiyomba wizara husika kufanya uchunguzi iptl na tuliletewa hapa.mleta mada hiyo alikua na lengo lakupotosha kua kwakua umeme unapatikana hapakua na haja yakuhoji matumizi yake.leo tumemeona matokeo yaliyopatikana.naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza waheshimiwa hao pamoja na mleta mada hii
   
 8. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hivi huyu FF ameolewa ? Nina mashaka sana kama kuna mwanamme anaweza kuona na kuishi na huyu mwanadamu. Lazima atakuwa ameolewa na Magamba, maana lazima apinge any comment ambayo inaonekana constructive ambayo inakosoa serikali au Magamba. Kuwa +ve sometime sio lazima upinge kila hoja. Sio lazima uchafue hali ya hewa hata kwenye hoja za msingi.
   
 9. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Lol! Ufisadi kila sehemu duh!
   
 10. H

  HlicesArerich Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Days are numbered. God bless revolutionalists.
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 11. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  FF,

  Inaelekea kuwa wewe ni Binti dogo sana ila huo ushungi na sura ya kumaa inawafanya watu wafikiri kaumri kamepanda kidogo. Kwa taarifa zako awamu zilizopita tumeshuhudia watu wakijiuzulu, kupelekwa mahakamani na kufungwa.

  Sasa hii ya kuja kutoa pongezi kwa baba mkwe wakati hatujaona kigogo yeyote akipelekwa Ukonga zaidi ya kutufanyia mazingaombwe pale Kisutu, tunashindwa kukuelewa. Hao dagaa waliopelekwa Ukonga tumesikia wakiwasiliana na Rais kwa simu za mkononi tokea huko huko gerezani. Sasa kweli unataka tuamini kuna kazi inaendelea hapo??
   
 12. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  I was making reference on YOUR OWN RESPONSE, japo kama kawaida yenu umeamua kujifanya hujui ninachokisema. IPTL ni mradi ulioanzishwa wakati kiwete, oops sorry kikwete akiwa waziri wa madini na nishati. Nakubaliana na wewe kuwa Mkapa alifanya madudu mengi tu lakini kati ya hayo la kumteua kikwete kuwa waziri wa madini na nishati hakulifanya.
   
 13. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  IPTL Alli hassan mwinyi, jakaya kikwete, and co.
  Hao wala watu walituletea janga lililo kazini kwa karibu miaka ishirini sasa, na hata baada ya mkataba huo kuisha madhara yake yataendelea kwa miaka na miaka... Walaaniwe wezi wote.
   
Loading...