Vigogo waangushwa uchaguzi CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF,

Nchi iko katika heka heka kubwa kutokana na chama kikuu cha upinzani CHADEMA kuendelea kufanya uchaguzi wake katika ngazi ya Kanda.

Kwa idadi kubwa Watanzania wanafuatilia kwa karibu sana uchaguzi huu pengine kuliko ule uchaguzi wa serikali za mitaa uluosusiwa na upinzani.

Kwa takriban majuma mawili sasa vyombo kadhaa vya habari vikiwemo Television, Radio, magazeti na mitandao ya kijamii habari kuu ni uchaguzi mkuu wa Chadema ngazi ya Kanda.

Katika uchaguzi huo uliohitimishwa jana kwa ngazi ya Kanda Taifa limeshuhudia vigogo kadhaa waliodhaniwa labda hawagusiki wakiangushwa katika uchaguzi huo.

Wachambuzi wa siasa wanaangazia kwamba kuangushwa kwa majina makubwa pengine ni kutokana na demokrasia iliyotamalaki isiyoangalia ukubwa wa jina la mtu.

Baadhi ya vigogo walioangushwa kwenye uchaguzi huo ni Fredrick Sumaye Kanda ya Pwani, John Heche Kanda ya Serengeti, Dr Alphonce Mbassa Kanda ya Kati, Joseph Selasini Kanda ya Kaskazini na Cecil Mwambe Kanda ya Kusini.

Mara baada ya uchaguzi huu wa Kanda kwa sasa gumzo ni uchaguzi mkuu unaoonekana kuwa kivutio si ndani tu bali hata nje ya nchi.

Tayari nafasi ya Mwenyekiti inawaniwa na watu mashuhuri watatu akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Tluway Sumaye,Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe na Mwenyekiti anayemaliza muda wake Freeman Mbowe.Huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikiwaniwa na Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Antipass Lissu na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea.

Lolote laweza kutokea kwenye uchaguzi ingawa wengi wanawapa nafasi Freeman Mbowe na Tundu Lissu kuibuka washindi kutokana na kuungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe.

Kuhusu mabaraza mvutano mkubwa unaonekana Baraza la Vijana BAVICHA ambapo karata inaangukia mafahali wawili ngazi ya vijana Alphonce Lusako na Mdude Nyagali.
 
Mwambieni Mbowe amteuwe John Heche kuwa katibu mkuu, hilo zezeta lake Mashinji amtafututie kazi nyingine.

Pia muhimu zaidi Mbowe akubali kujifunza ni makosa makubwa amefanya kama mpaka leo alikuwa ajaandaa successor wake kwenye uenyekiti.

Ni lazima Mbowe aelewe hii ni awamu ya mwisho anakwenda kuthibishwa lakini aandae mrithi wake sasa, kwa sababu yeye Mbowe pia àliandaliwa iweje yeye hataki kuandaa mrithi wake? Hii ni miaka mitano ya mwisho hatutaki usultani.
 
Back
Top Bottom