mwanaone
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 637
- 760
Mauaji ya South Beach yazua utata
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 20 April 2011
MAZINGIRA yanatengenezwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam , Lillah Hussein (25) kuachiwa huru, MwanaHALISI limeelezwa.
Lillah alifariki dunia Jumamosi usiku akiwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), baada ya kupata majeraha ya moto baada ya kumwagiwa petroli huku akiwa amevikwa tairi shingoni.
Tukio hilo lilitokea kwenye hoteli ya South Beach, Kigamboni, Dar es Salaam ambako mhanga huyo alifika kwa ajili ya kupata burudani ya muziki. Inadaiwa alitaka kuingia ukumbini bila ya kulipa kiingilio.
MwanaHALISI limeelezwa kuwa mara baada ya tukio hilo la kuchomwa moto, watendaji wawili waliohusishwa na tukio hilo , walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Mjimwema, Kigamboni.
Taarifa zinasema walifikishwa mahakamani juzi Jumatatu, kwa mashitaka mawili tofauti yasiyokuwa ya mauaji kama alivyoahidi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, ACP David Misime.
Pia, meneja wa hoteli hiyo, Salum Nassoro na mtuhumiwa mwingine katika kesi hiyo, nao wamekamatwa tayari na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.
Kwa mujibu wa hati ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, watuhumiwa hao wawili; John Ambumbulwisye na Salum Nathoo Chipata, walifunguliwa kesi kwa mashitaka tofauti ya kushambulia na kujeruhi.
Haiwezekani watu wamwagie mtu mafuta ya petroli na kumfunga tairi halafu useme walitaka kujeruhi. Hawa walitaka kuua na mashitaka yao ilibidi yaseme kutaka kuua na si kujeruhi, alisema Laetitia Petro, mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
LHRC imechunguza tukio hilo tangu lilipotokea 10 Aprili 2011 na kubaini kasoro nyingi katika namna lilivyoshughulikiwa na vyombo vya dola.
Kwa mfano, Laetitia alieleza juzi Jumatatu kuwa watuhumiwa hao wa mauaji walipewa dhamana na mahakama hiyo kwa kutumia hati isiyokuwa na nguvu yoyote kwenye misingi ya kisheria.
Nakala ya hati hiyo haina jina la mahakama iliyoitoa, namba ya kesi husika wala mwaka. Pia haina muhuri wa mahakama, mambo ambayo LHRC inaona yanalenga kupoteza mwelekeo wa kesi.
Katika tukio hilo, Lillah ambaye wakazi wa Kigamboni wanadai hakuwa mwizi, alikamatwa na kuchomwa moto kabla ya kuokolewa baada ya mwenyewe kwenda kujitupa baharini kuokoa maisha yake.
Lillah aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa nguo za kuogelea na vitu vya kitamaduni kwenye fukwe za bahari eneo la Kigamboni, aliharibiwa katika sehemu za siri, mwilini na kichwani.
Alikumbwa na mkasa huo baada ya kukutwa ukumbini bila ya tiketi maalum inayovaliwa mkononi na wale wanaoingia ndani kupata burudani.
Baada ya kukamatwa, alipigwa kabla ya kupelekwa kwa Chipata anayetajwa kuamuru Lillah achomwe.
LHRC inaamini kuwa kuna ushahidi unaoonesha kuwa baadhi ya walinzi wa hoteli hiyo walikuwa wakimfahamu Lillah na hawakutaka achomwe moto na ndiyo waliotoa taarifa kwa wananchi kuwa anachomwa.
Tukio la kuchomwa moto kwa Lillah lilichafua amani maeneo ya Kigamboni, kiasi kwamba wananchi walifikia hatua ya kutaka kuichoma moto hoteli hiyo yenye utata mkubwa.
Kuna madai kuwa wakazi wengi hawafurahishwi na kuwepo kwa hoteli hiyo iliyojengwa baada ya kubomolewa makaburi ya wenyeji bila ya kulipwa fidia.
Inadaiwa kuwa hoteli hiyo imekuwa ikipiga muziki mfululizo nyakati za usiku; ikiwamo mara baada ya tukio la kuchomwa moto kwa Lillah, jambo lililopandisha hasira za wananchi wa Kigamboni ambao wameumizwa na ukatili uliofanyika kwa mwenzao huyo.
Wakati tukienda mitamboni, MwanaHALISI liliarifiwa kuwa baadhi ya viongozi waandamizi serikalini walikuwa wanajitahidi kutaka kuhakikisha wahusika hawashitakiwi kwa kosa zito kwa kuwa ni wawekezaji na huenda kushitakiwa kwao kukachafua shughuli za uwekezaji.
Mmoja wa maofisa wa jeshi la polisi ambao wanalifahamu sakata hilo kwa undani amelithibitishia gazeti hili kuwa kuna baadhi ya vigogo ndani ya serikali na polisi wanajaribu kuzuia haki kutendeka.
Kwa sasa, kesi hiyo iko katika Mahakama ya Wilaya Temeke ambayo kisheria haina uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji zaidi tu ya kufanya uchunguzi wa awali.
Lakini, kitendo cha mtuhumiwa mmoja kufunguliwa mashitaka ya shambulio na mwingine kujeruhi, na kwa kupewa dhamana haraka kinyume na maombi ya polisi, kimezidisha hofu kwa watetezi wa haki za binadamu kuwa huenda kuna jitihada za kuzuia haki kutendeka.