Mahakama imewaachia huru vigogo wa mradi wa mabasi ya mwendokasi, walishtakiwa kwa uhujumu uchumi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mahakama imewaachia huru vigogo wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi kwenye kesi ya kusababisha hasara ya Mil 83.5.
=========

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART), akiwemo mtendaji mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo na mwenzao.

Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano ni Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa upande wa utetezi ameona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao pasipo kuacha shaka.

Mbali na Mlambo wengine walioachiwa huru ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kusababisha hasara ya Sh 83.5 milioni.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Septemba Mosi na Oktoba Mosi, mwaka 2013 maeneo ya Kinondoni Dar es Salaam, Mlambo, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 83.5 milioni.

CHANZO: Mwananchi
 
Sasa gharama ya kuendesha haya makesi hewa nani wa lulaukiwa?. ninafikiri ifike mahali hii serikali yetu tuipigie hesabu na kuwashitaki mahakamani kwa kutumia madaraka yao vibaya na kusababisha hasara kwa pesa za wananchi wa Tanzania.
 
[HASHTAG]#Poise[/HASHTAG],
Awamu hii sijui mahakama na ofisi ya mwanasheria au DCI wanafanyaje kazi!

Any way, ngoja wasijesema nawashwa-washwa wakati mimi ndiye ninayewashawasha mrembo wangu huku kijijini Ntwara.
 
Mahakama imewaachia huru vigogo wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi kwenye kesi ya kusababisha hasara ya Mil 83.5.
=========

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART), akiwemo mtendaji mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo na mwenzao.

Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano ni Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa upande wa utetezi ameona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao pasipo kuacha shaka.

Mbali na Mlambo wengine walioachiwa huru ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kusababisha hasara ya Sh 83.5 milioni.

Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Septemba Mosi na Oktoba Mosi, mwaka 2013 maeneo ya Kinondoni Dar es Salaam, Mlambo, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 83.5 milioni.

CHANZO: Mwananchi
Hizo kesi achaneni nazo hamtashinda hata moja, maana kila moja ina mkono wa mtu ambaye analindwa na katiba asiguswe
 
Serikali mpk inafungua kesi ushahidi wao wanautoa kwny magazeti ya uhuru nini?mbn udaku mwingi kuliko uhalisia aseee?
 
Wangefungwa hawa watu mngesema ni maagizo kutoka juu. Wameshinda kesi badala ya kusema mahakama inatimiza wajibu mnaleta majungu kipi ni kipi sasa?!! Ndio maana mnapuuzwa na kuonekana wapiga majungu mitandaoni tu.
 
Tukisema huyu bwana ni msanii na anatengenezaga kick bin the lager,tutaambiwa tunatukana.

Masamaki wa TRA alikamatwa kwa kesi ya uhujumu uchumi,na wengine kibao,akakamatwa Rishard Bade kisa alikuwa UKAWA kwenye uchaguzi na kuambiwa sio RAIA ila Mkenya,Masamaki akaachiwa guru na serikali yenyewe huku ulisema haina shida naye,Mramba na Yona kwa hasara ya 11bikkioni wakaambiwa wakafagie tu hospital.

Manji akavurumushwa kila sina ya makes I,mara UDA,then wanakuja kuachiwa!!

Kama sio maigizo na kick ya the lager ni nini?!!
 
afadhali leo wakalale na familia zao, maana kuna mtu alisema anarara nao mbere
 
Kwenye hizi kesi watu wengi mno wanakutwa hawana hatia, wanaokutwa na hatia adhabu zao utacheka.

Mtu katia hasara ya milioni mia na zaidi adhabu yake ni faini milioni 20 hivi na kufanya kazi za jamii.

Mwingine kakutwa na hatia kwa kuinunulia kampuni magari shit adhabu yake ni ama aende jela miaka 4 au alipe mil 35.

Gharama za kesi vipi?
Muda uliopotea?

Mahakama ya mafisadi vipi?
 
Back
Top Bottom