Vigogo wa EPA BoT wakata rufaa kwenye Jopo Maalum kamati ya Nidhamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vigogo wa EPA BoT wakata rufaa kwenye Jopo Maalum kamati ya Nidhamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Sep 2, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,169
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Vigogo wa EPA BoT wakata rufaa kwenye Jopo Maalum kamati ya Nidhamu
  Na Ramadhan Semtawa

  BAADHI ya vigogo wa Benki Kuu (BoT) wanaotajwa kuhusika katika ufisadi wa zaidi ya Sh133 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), wameanza kukata rufaa katika Jopo Maalumu la Kamati ya Nidhamu kupinga tuhuma na adhabu dhidi yao.


  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya gazeti hili kuripoti kuwa baadhi ya watuhumiwa, kujianda kutumia taratibu za kisheria kupinga adhabu ambazo zitatolewa na uongozi wa BoT dhidi yao.


  Gavana wa BoT. Prof Benno Ndulu alipoulizwa jijini Dar es Salaam jana kuhusu suala hilo, alisema rufaa ni haki ya msingi ya mtu na kuongeza kwamba, upo muda ambao ni wa mwisho kwa kila mtu kujitetea, lakini hakutaka kuutaja.


  Hata hivyo, Gavana Prof Ndulu alifafanua kwamba yeye ni mhusika mkuu katika mchakato huo, hivyo hawezi kuanza kuzungumzia undani wa mchakato huo.


  "Rufaa ni haki ya mtu, kila mtu anapaswa kusikilizwa ndiyo utaratibu, lakini sasa siwezi kuanza kuzungumzia kwa kina kuhusu hilo kwani mimi ni mhusika mkuu katika mchakato," alisema na kuongeza:


  "Wakati mwingine, huwezi kwenda mahakamani na kumuuliza hakimu kwamba rufaa imekatwa utatoa lini uamuzi, lakini kama ni kukata rufaa na kusikilizwa hiyo ni haki ya msingi watuhumiwa wanayohaki."


  "Ila ninachoweza kukwambia mchakato bado unaendelea, hili ni jambo ambalo linahitaji uangalifu na kuzingatia haki ya kila mmoja."


  Profesa Ndulu aliongeza kwamba, iwapo BoT itakurupuka au yeye kuanza kuzungumzia mchakato huo bila umakini kuna uwezekano wa watuhumiwa kwenda mahakamani.


  Profesa Ndulu alisema jambo hilo ni nyeti na zito, hivyo litaweza kufahamika vema baada ya kumalizika mchakato mzima na kutaka watu wavute subira.


  Wakati Prof Ndulu akisema hilo, taarifa kutoka ndani ya BoT zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema vigogo hao wamekuwa wakijitetea kwa nyakati tofauti baada ya kamati hiyo kutoa nafasi.


  "Mchakato bado unaendelea, kulikuwa na haki ya mmoja mmoja ya rufaa, wapo ambao wameitumia, wamejitetea katika jopo wakipinga tuhuma na adhabu dhidi yao," kilithibiitisha chanzo hicho.


  Kwa mujibu wa taarifa hizo, hadi sasa jopo hilo linaendelea kusikiliza utetezi kwa mtu mmoja mmoja kwa waliotajwa kushindwa kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao na kisha kulisababisha taifa hasara kubwa.


  Hata hivyo, kazi ya BoT katika kushughulikia suala hilo ni kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za utumishi na si kufungua mashitaka ya jinai mahakamani.


  Katika mchakato huo, kama kuna jukumu la kufungua mashitaka ya jinai mahakamani litakuwa chini ya Timu ya Rais, ambayo hadi sasa matokeo ya mwisho yanasubiriwa Oktoba 31.


  Taarifa hizo, ziliongeza kwamba jopo hilo la Kamati ya Nidhamu, kwa sasa linaendelea na mchakato huo ambao unatarajiwa kukamilika wakati wowote baada ya kutoa haki kwa mtu mmoja.


  Mwananchi wiki iliyopita, ilidokezwa kwamba vigogo hao walikuwa wamejiandaa kwa kutumia mawakili wao kuitikisa BoT iwapo itatoa adhabu dhidi yao ambazo ziko nje ya taratibu.


  Tayari baadhi ya majina ya vigogo hao yameanza kutajwa wakiwamo Wakurugenzi waliokumbwa na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Gavana Ndulu, Machi mwaka huu.


  Gavana aliweka bayana kwamba, mabadiliko hayo yalizingatia mambo matatu ya msingi kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji ili kuleta tija na ufanisi ndani ya benki.


  Mabadiliko hayo yaligusa idara karibu zote isipokuwa Idara ya Uchumi, Fedha na Masoko na tawi la Mwanza, matawi ya BoT nchini ukiacha Mwanza ni pamoja na Zanzibar, Mbeya na Arusha ambayo yamekuwa yakiongozwa na Wakurugenzi.


  Idara nyingine zilizowahi kukumbwa na mabadiliko zilikuwa ni Fedha, Benki, Idara inayoshughulikia Deni la Taifa na inayoshughulikia Zabuni.


  Katika mabadiliko hayo, baadhi ya wakurugenzi walipandishwa vyeo, wengine kuondolewa na baadhi kuhamishwa idara.


  Wiki mbili zilizopita wakati akihutubia Bunge, Rais Jakaya Kikwete, alisema BoT itatangaza hatua za kinidhamu ambazo imechukua kwa watumishi waliohusika katika kashfa ya EPA kwa kuwa hilo lipo chini ya mamlaka yao kisheria
   
Loading...