Vigogo wa Chama cha Walimu (CWT) waburuzwa Mahakamani Kisutu kwa ufisadi

VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Hasara ya milion 13? au ni bilioni 13? Takukuru wanapoteza muda wao sasa
 
Wanaofungwa ni wale wanaoiba Nyanya Sokoni kina Kigwa no ni Waheshimiwa
 
Kila siku nasema CWT ni janga kubwa sanaaa, na kama ni aina ya ugonjwa basi ile CANCER ya moyo.

Halafu hicho kiwango cha billion13 nadhani kuna typing error, watakua wameacha sifuri moja.
Hao ni makada wa ccm,uwizi chamani ni sunna
 
VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Nilisha wah sema, Sjui walimu wanakwama wapi! Hichi CHAMA CHA WAPIGAJI (CWT), wakipinge, wanakusanya mabilion, nlishangaa kuona Mwalimu mmoja alifariki af CWT wakatoa bando mbili za bati, wakat mpaka anafaliki alikua na miaka 17 kazini anakatwa na CWT, chama hichi kifutwe na viongozi wakaguliwe, na hela zitakazo patkana zirudishwe kwa walimu kupitia akaunt zao, na wafanyakaz wote warud TUCTA, na ndio kiwe chama kimoja tu kwa wafanyakazi wote, af makato yawe 0.5%, na kiwe kinarudidha asilimia ya faida kwa wafanyakazi wachangiaji kila mwaka kupitia mirad itakayo buni, mfano kujenga majengo na kukodisha, na sio ujinga unaoendelea.
 
SASA 13m, si wangeitwa wajieleze.....then waambiwe walipe......nadhani kuna typing error hapa....only 13m...sio 130 kweli?
 
VIONGOZI WAWILI WA CWT KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA UCHEPUSHAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA.

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, imekuwa ikifanya uchunguzi dhidi ya baadhi ya Viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kwa makosa mbalimbali yanayoangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Viongozi hao, ambao wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yao kinyume na Kif. cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 pamoja na Uchepushaji – Kinyume na Kif cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 ni hawa wawili wafuatao:Bw. Deus Gracewell Seif (Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)Bw. Abubakar S. Allawi (Mweka Hazina wa Chama cha Walimu Tanzania CWT)

Ndugu WanaHabari,
Watuhumiwa hawa, walikuwa wakichunguzwa kwa kosa la uchepushaji pamoja na kutumia madaraka yao vibaya, kama viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania.

Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ulibaini kwamba mwaka 2018, viongozi hawa walitumia zaidi ya Shilingi Milioni 13.9 mali ya chama hicho, kwa ajili ya kulipia tiketi za ndege pamoja na kulipia gharama za malazi, kwa safari ya kwenda Cape Verde.

Kwa wakati huo – yaani mwaka 2018, Cape Verde kulikuwa na Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), waliokuwa wakicheza na Timu ya Taifa ya Cape Verde.

Kwa kufanya hivyo, watuhumiwa hawa wameenda kinyume na vifungu vya 29 pamoja na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007.

Ndugu WanaHabari,
Uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu dhidi ya tuhuma hii umekamilika na hivyo, kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, leo Jumatatu - Mei 3, 2021 watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu – Jijini Dar Es Salaam, ili kujibu mashitaka yanayowakabili.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

IMETOLEWA NA:

Doreen J. Kapwani

AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU

KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Kwani kwenda Cape Verde ni kosa? Au kosa ni kwa sababu kulikua na mechi? Bado maelezo hayako clear
 
TaKukuru niwakumbushe cha kuongezea na kwa kusaidia watumishi anbao ni walimu wetu, kuna magari used zaidi ya 210 yaliagizwa na kuingizwa nchini kutolea Japan,ili kutumiwa na makatibu wa cwt nchi nzima. Fuatilieni yalikuwa na ufisadi uliotukuka. Kuanzia kuagizwa kwake hadi ununuzi wake.
True! Af matumizi ya hayo magari. Si yakiofis, kwanza yanalala nyumbani kwa makatubu, na wanayatumia kifamilia zaid na sio kiofis, af mafuta nihela za walimu! Inasikitisha sana! Yana paki had bar !!
 
Jiulize kwa nini wakati wa CORONA shule zilifungwa mikutano kadha wa kadhaa ilizuiliwa isifanyike na ikawekwa masharti ya kujikinga. Ila CWT walikusanyika kiwilaya hadi kitaifa na ukapigwa mkutano mkuu chini ya ulinzi mkali hadi jamaa wa kitengo walikuwamo.
Kama sio kufaidika na rasilimali za CWT basi serikali ya CCM inanufaika na CWT inavyoendeshwa. Hapa ni ngumu hao jamaa kuonekana GUILTY na hata ikiwa kulipa faini wataipangua mapema mnoo hii kesi.
Af ukitaka kujua kua CWT ni kichaka! Jiulize tena kwanini hawakusitisha makato yao angalau kwa kipindi cha CORONA kama njia ya kuwapa pole Walimu kwa wakat huo mgumu.
 
Hii kesi ina walakini nimeshangaa Takukuru imekomaa na mil 13. Why wasivalie njuga ripoti za CAG
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom